Ndugu zangu mimi ni mtazania wa kawaida na najaribu kupambana na ugumu wa maisha ya hapa bongo ambapo pengo kati ya maskini na tajiri linazidi kuongezeka siku hadi siku. Nilisikia habari ya kusajili ardhi na manufaa yake kwamba naweza kuitumia hati miliki kama dhamana ya kupata mkopo hivyo kujiimarisha kiuchumi na nilifanikiwa kusajili ardhi yangu na kupata Hati Miliki ya Kijiji. SWALI: Hati miliki za vijiji ni kweli zinapokelewa na mabenki kama dhamana ya mikopo? Na kama hazipokelewi ni kwa nini? Nitashukuru kwa msaada wenu.