Hati ya kiwanja ikipotea au kuungua kuna uwezekano wa kupata nyingine original?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Habari.
Miaka michache iliyopita nilipata mkasa wa kuungua nyumba niliyokuwa naishi na moja ya vitu vilivyoungua ni hati ya kiwanja. Je kuna uwezekano wa kuomba nyingine idara ya ardhi? Kwa sasa nimebaki na photocopy tu. Naomba kama kuna mwenye uelewa au aliyewahi kupatwa na mkasa kama wangu tupeane uzoefu.
 
Uwezekano wa kupata Hati nyingine Original haupo, isipokuwa utapatiwa "Duplicate Copy" ambayo utaitumia kama Original Certificate of Right of Occupancy.

Hati Miliki nyingine ambayo ni Original Copy utaipata baada ya Muda wa Uhai wa Miliki yako ya Ardhi (Land Tenure) iliyopo Sasa hivi kufika ukomo wake (expired) na kisha kuomba Tena upya ili upatiwe Miliki nyingine Mpya sambamba na kupatiwa Hati nyingine Mpya.
 
Shukran sana. Ngoja jumatatu ninyookee idarani. Unaweza kuwa unajua gharama yake? Hopefully haitakuwa sawa na gharama ya hati mpya.
 
Suala la kupata Duplicate copy ya Hati miliki baada ya Ile ya mwanzo kupotea au kuharibika ni Mchakato mrefu, gharama za Mchakato huo huwa zinabadilishwa mara kwa mara.

Nafikiri unapaswa kwenda katika Ofisi za Ardhi ili uweze kupata maelekezo kutoka katika Mamlaka hizo. Ila jiandae vizuri 'Kisaikolojia na kiuchumi.'
 
Shukran sana mkuu
 
samahani mkuu naomba na mm unieleweshe hili kama unafahamu mm hati imekosewa jina yaan jina langu limesahaulika wameweka jina la baba na la babu uwezekano wa kubadilisha upo au
 
Hayo majina ya baba na babu yako wao waliyapata wapi? Hao watengenezaji wa Hati miliki waliyajuaje hayo majina ya baba na babu yako???

Tuanzie hapa kwanza.
 
Uwezekano wa kupata Hati nyingine Original haupo, isipokuwa utapatiwa "Duplicate Copy" ambayo utaitumia kama Original Certificate of Right of Occupancy.

Hati Miliki nyingine ambayo ni Original Copy utaipata baada ya Muda wa Uhai wa Miliki yako ya Ardhi (Land Tenure) iliyopo Sasa hivi kufika ukomo wake (expired) na kisha kuomba Tena upya ili upatiwe Miliki nyingine Mpya sambamba na kupatiwa Hati nyingine Mpya.
Mkuu asante sana kwa elimu mujarabu,ubarikiwe sana [emoji1431]!! Hili swali nilikua najiuliza sana,mbona Aridhi wamenipa duplicate copy au wamenipiga!!??
 
samahani mkuu naomba na mm unieleweshe hili kama unafahamu mm hati imekosewa jina yaan jina langu limesahaulika wameweka jina la baba na la babu uwezekano wa kubadilisha upo au
We kaka majina ya baba yako na babu yako waliyapataje, Sema shida yako usaidiwe, go to the point, Vipi mnagombea urithi?🤣🤣🤣
 
hapana mkuu serious sio utani picha ni yangu na kiwanaja nmenunua mwaka jana hatai nimepata miez 2 mbele ila nlkua mbali na mji nkaja kuichukua hatj yangu kwez wa 6 ndo jina liko tofaut mkuu nmesahaulika ndo maana nauliza hvo sio kama nataka kutapeli mtu mkuu duh 🤣🤣
 
Hayo majina ya baba na babu yako wao waliyapata wapi? Hao watengenezaji wa Hati miliki waliyajuaje hayo majina ya baba na babu yako???

Tuanzie hapa kwanza.
wakat wa kuandikishiana majina ya mnunuaji na muuzaji nliandika majina yangu 3 kwa watu wa serikal ya mtaa maana hati sio ya kupata siku hyhyo ko nkaacha baada ya muda wa miez 2 nadhan ndo nkaja kupata hati yngu maana yake mm nlitakiwa kusaini tu maana sain za wajumbe na mashahid na wote yapo humo mkuu
 
Naomba kuuliza;
Iwapo wazazi wamefariki bila kuacha taarifa za hati miliki kwahiyo haijulikani ilipo,
Je,mrithi anatakiwa kufata taratibu gani ili aweze kupata hati miliki upya inachukua muda gani na inagharimu kiasi gani

Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom