Hati ya nyumba Imechanwa alafu ikatengenezwa nyingine

Habari Wana Forum!

Naombeni wataamu wa haya mambo ya Hati za Nyumba wanisaidie kisheria hili limekaaje na je kuna msaada gani unaweza patikana ili haki itendeke!?...
Dah mkuu pole sana.

Yaani mambo uliyoyaelezea yote ya kwenye familia yenu pia yapo kwetu pia.

Naamini wajuzi watakuja kukusaidia,pia majibu utakayoyapata yatanisaidia na mimi huko mbeleni.
 
Mlifanya kikao cha familia kumpata msimamizi wa mirathi?! Tuanzie hapo.
 
Nasubiri majibu kwa wana sheria, nimegundua kitu kumbe hati inaweza kubadilishwa uhusika bila kuwepo pande zote mbili kwa makubaliano.
 
Yaani kaka hata mimi nimeshangaa sana kwamba kama hali inakuwa kirahisi hivyo, watu wenye hali duni si watakuwa wanadhulumiwa kirahisi sana.. yaan mimi sikutegemea Huyu Mama angeweza kubadilisha na sijui hawakumuuliza kama ana watoto wakiume au sababu za yeye kubadilisha ziliwaridhishaje mpaka waka badilisha Hati kwa kauli ya Mtu mmoja.? familia tuko watu 9 ila mwanamke ambaye niwakuja tu hajui ata nyumba ilivyojengwa leo anapewa hati ya jina lake bila ndugu kujua..! hivi kweli ndio serikali inavyofanya kazi hivyo??
 
Mlifanya kikao cha familia kumpata msimamizi wa mirathi?! Tuanzie hapo.
Kile kikao kilomchagua Kaka mkubwa ndio awe msimamizi wa Ndugu zake na Mali zao.. na yule mama Aliambiwa akae tu ndani ila nyumba ni ya watoto na tukakubaliana hivyo so miaka yote tunajua hivyo.. Ajabu Juzi yule kaka mkubwa kafariki.
 
Yaan kaka ata mm nimeshangaa sana kwamba kama hali inakuwa kirahisi hivyo, watu wenye hali duni si watakuwa wana zulumiwa kirahis sana.. yaan mm sikutegemea Huyu Mama angeweza kubadilisha na sijui hawakumuuliza kama ana watoto wakiume au sababu za yeye kubadilisha ziliwaridhishaje mpaka waka badilisha Hati kwa kauli ya Mtu mmoja.? familia tuko watu 9 ila mwanamke ambaye niwakuja tu hajui ata nyumba ilivyojengwa leo anapewa hati ya jina lake bila ndugu kujua..! hivi kweli ndio serikali inavyofanya kazi hivyo??

Yaani hata mimi sielewi hapo ilikuwaje
 
Kwanza hiyo hati yake huyo mama itakuwa ya kufoji, otherwise labda awe ameshirikiana na msimamizi mliyemteua (kaka yenu ambae ameshafariki)
Na kama msimamizi wa mirathi amefariki inabidi wana familia mnaohusika mrudi tena mahakamani mumchague msimamizi mwingine miongoni mwenu mnaemuamini na atakae wasimamia , mkishamchagua na akapewa hati ya usimamizi wa mirathi na mahakama, hapo sasa huyo msimamizi ndio mwenye wajibu wa kufuatilia hiyo hati ya nyumba iwe ardhi au halmashauri.
Mimi sio mwanasheria ila nimejifunza vitu vingi kuhusu mirathi baada ya kufariki mzee wangu na kukutana na mikikimikiki.
Kama una swali jengine uliza.
 
Nenda halmashauri ofisi za ardhi,waambie unataka kufanya kitu kinaitwa "official search" ya nyumba yetu ( uwe na utambulisho wa nyumba kama plot number na block no )...watakutafutia file la nyumba yenu....kupitia hilo file utaona mwenendo wa umiliki wa nyumba yenu..kama kulibadilishwa umiliki utajua
 
Asante kaka.. huwa unalipia kiasi Gani? na Je! kama itakuwa kweli ilibadilishwa.. nikakuta jina lake huyu Mama kuna njia gani naweza ifanya kupata haki yetu?
 
Kwanza hiyo hati yake huyo mama itakuwa ya kufoji, otherwise labda awe ameshirikiana na msimamizi mliyemteua (kaka yenu ambae ameshafariki)
Na kama msimamizi wa mirathi amefariki inabidi wana familia mnaohusika mrudi tena mahakamani mumchague msimamizi mwingine miongoni mwenu mnaemuamini na atakae wasimamia , mkishamchagua na akapewa hati ya usimamizi wa mirathi na mahakama, hapo sasa huyo msimamizi ndio mwenye wajibu wa kufuatilia hiyo hati ya nyumba iwe ardhi au halmashauri.
Mimi sio mwanasheria ila nimejifunza vitu vingi kuhusu mirathi baada ya kufariki mzee wangu na kukutana na mikikimikiki.
Kama una swali jengine uliza.
Unajua sisi hatukuchauga msimamizi aliye kuwa approved na mahakama . ilikuwa ni kauli tu za Ukoo kisha zikapita na kwa kuwa tulikuwa wadogo sana hatukujua haki zetu na Yule Msimamizi wa Ukoo aliyesimamia kile kikao alikuwa upande wa huyu Mama tapeli.. na kwa bahati mbaya alishafariki, na yule Kaka mkubwa aliyepewa kazi ya kusimamia ndugu zake kama kiongozi wa Familia naye kafariki mwaka Jana July. Hata ule muhutasari wa kikao haupo tena hatujui uko wapi .
 
Kile kikao kilomchagua Kaka mkubwa ndio awe msimamizi wa Ndugu zake na Mali zao.. na yule mama Aliambiwa akae tu ndani ila nyumba ni ya watoto na tukakubaliana hivyo so miaka yote tunajua hivyo.. Ajabu Juzi yule kaka mkubwa kafariki.
duh huyo sio mtu mzuri kabisa.
Huyo mwanamke ni kabila gani aisee?
 
duh huyo sio mtu mzuri kabisa.
Huyo mwanamke ni kabila gani aisee?
Yaan kwa aliyo yafanya kwenye familia yangu ya kuangamiza ndugu wa baba, baba yangu, Kaka yetu, na kuwafanya wengine vichaa ata sina muda kabisa wakumjua kabila lake.. ninachopambania sasa ni kulinda roho za ndugu zangu na ya mama yangu tusi angamizwe maana Kuna gonjwa moja alituma juzi kwa mama yangu lakutaka kumpofusha na kumfanya aparalize asifuatilie haki za watoto wake. nikaona hii imekuwa Too much.. alafu kuna baba mdogo moja tu kabaki kwenye ukoo ambaye alisomeshwa na baba yangu alikaa na kulelewa na mama yangu yeye ndio anajua siri ya ujenzi wa ile nyumba.. ndio anatupigania.. lakin juzi kafanyiwa jambo laajabu kwenye miguu hawezi kuinuka kutoka ndani anaumwa siyo kawaida.. ndio maana nina waza jinsi ya kumuwahi huyu Mama asiendeelee kuangamiza watu.
 
duh mkuu pole sana.
Matatizo yako na yangu yanafanana sana,hata mimi pia nina vita nzito sana ya kuwapigania ndugu zangu na bado napambana.
Yote yanawezekana ili mradi tu uwe vizuri kiuchumi
Yaan kwa aliyo yafanya kwenye familia yangu ya kuangamiza ndugu wa baba, baba yangu, Kaka yetu, na kuwafanya wengine vichaa ata sina muda kabisa wakumjua kabila lake.. ninachopambania sasa ni kulinda roho za ndugu zangu na ya mama yangu tusi angamizwe maana Kuna gonjwa moja alituma juzi kwa mama yangu lakutaka kumpofusha na kumfanya aparalize asifuatilie haki za watoto wake. nikaona hii imekuwa Too much.. alafu kuna baba mdogo moja tu kabaki kwenye ukoo ambaye alisomeshwa na baba yangu alikaa na kulelewa na mama yangu yeye ndio anajua siri ya ujenzi wa ile nyumba.. ndio anatupigania.. lakin juzi kafanyiwa jambo laajabu kwenye miguu hawezi kuinuka kutoka ndani anaumwa siyo kawaida.. ndio maana nina waza jinsi ya kumuwahi huyu Mama asiendeelee kuangamiza watu.
 
Kumuwahi ni yeye aanze kufaa tuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Ni kweli aisee,watu kama wale wakiendelea kuwa hai kuwashinda ni ngumu sana kwa sababu huwa wana plan nyingi sana na huwa wameandaa mitandao yao ya ushirikina kwa hiyo wakihisi kuna kitu hakipo sawa wanapiga simu tu mahali ndani ya masaa 12 wanarekebisha jambo.
Kumuwahi ni yeye aanze kufaa tuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ni rahisi, nenda halmashauri ya wilaya au manispaa uliyopo uwaone watu wa idara ya ardhi. Omba kufanya upekuzi rasmi(official search) ambayo inagharimu shilingi elfu kumi. Utapata print out ya jina la current owner.

Lakini ili upate suluhisho la kudumi, itisheni kikao cha familia, na mpendekeze msimamizi wa mirathi. Andaa muhtasari alafu nenda mahakamani. Atakayetuliwa na mahakama ndiye atakayekusanya mali zote za marehemu na kuzigawa kwa warithi wa marehemu.

Hivyo, hata kama kuna forgery au fraud, msimamizi wa mirathi ana anauwezo wa kwenda mahakamani kudai ownership ya mali za marehemu.
 
Inavyoonekana mko watoto nyomi mnaogombea mali ya urithi.. Hata mkiachwa wenyewe akaondoka huyo mama bado mtauana.
Kama marehemu kaamua kumgawia mama wa kambo nyumba na nyie mlifukuzwa ina maana marehemu hakuwahitaji kwenye mali zake, so ni bora mpambane na hali zenu mtafute vya kwenu kuliko kugombea mali za urithi.
 
Kuna ukweli mzito hapa
 
Back
Top Bottom