Habari Wana Forum!
Naombeni wataamu wa haya mambo ya Hati za Nyumba wanisaidie kisheria hili limekaaje na je kuna msaada gani unaweza patikana ili haki itendeke!?
Ni hivi.. kwenye Familia Yetu Baba yetu alifariki miaka ya 2003 na akawa ameacha mke kule ndani Vikaao vya ukoo Vikasema kwa kuwa kimeachwa mtu mule ndani tumvumilie mpaka atakapo kuwa hayupo.
Nyumba hii alijenga Baba yangu na Mama yangu ila baadaye wakawa wamegombana na Baba baada ya kichonganishwa na huyu mwanamke aliye kuja kivamia ndani na kuanza ushirikina na hatimaye aka mteka akili mzee na sisi tukawa tumeondoka kwenda kuishi na Mama yetu.
Sasa baadaye Baba akafariki Ndio kule ndani akabaki yule mama.. tulipo dai nyumba yetu Ukoo ulisema tumuache akiwa hayupo kwa kuwa ni mzee watoto wata amua na nyumba yao. basi sisi kweli tukaendelea kupangisha mitaani na mama yetu.. hatimaye leo tumegudua Yule mama kachana ile hati ya Awali ya nyumba iliyokuwa imeandikwa jina la Baba yetu akachana na akaenda kutengeneza nyingine yenye jina lake.
Juzi ndio wamegombana na mwanawe wakike yule mwanawe akaropoka majirani wakasikia ndio sisi tukaambiwa kuwa kumbe hati ilisha badilishwa.
Tulipo mbana mtoto wake aliye mropokea mama yake kweli akasema mbona ilisha badilishwa tangu 2004 baada ya baba kufariki 2003.. Ambapo kwa sasa ina jina la huyu Mama.
Kiukweli tumeshangaa sana alitumianjia gani mpaka akapata yenye jina lake wakati Hajui ata tofali ya nyumba wala hakuwahi jua imehengwaje na walio jenga ni mama yangu na baba yangu tena kwa shida sana miaka hiyo wanafanya miradi ya kusambaza kuku na mayai ya kisasa kwenye mahotel miaka ya 1980 ndio wakaja wakajenga miaka ya 1983 sasa huyu mwana mke alipotuvamia tukaondoka baba akaanza kukaa naye.
Leo hii Hati isha badilishwa na jina kaweka lake.. Je sheria hapo imekaaje ndugu zanguni.. nifanyaje? Maana mwenye kujielewa kidogo aliye baki ni mm wengine huyu mama kawaharibu akili wamekuwa kama machizi.
Msaada wenu tafadhali.
Sent from my SM-N910C using
JamiiForums mobile app