Hati ya nyumba Imechanwa alafu ikatengenezwa nyingine

Uchawi upo na waganga wapo wazuri wachache waliobaki. Hakika huku jamvini kama una uhakika na mtaalam wa kusaidiwa hii familia tafadhali wasaidie ili wajikomboe. Mkishapata haki yenu mpumzisheni huyo mama maana ataendekea kuwatesa sana. Tit for Tat. Nimesikitika sana.
 
Kesi za kishirikina zina malizwa kishirikina au ki lokole,chagua moja hapo.
Ukiimaliza kwanza kwa njia moja wapo,hilo la hati halitakuwa gumu.
Anza na kushugulikia mzizi wa tatizo na sio matokeo ya tatzo..

Pili hata ww hauko salama sana,
Cha msingi tafuta nguvu kubwa zaid ya kukulinda na balaa la huyo mama,kama ni kuokoka okoka kweli kwa kumaanisha.
Ndo uweze kupambana nae.

Mark 3:27
[27]No man can enter into a strong man's house, and spoil his goods, except he will first bind the strong man; and then he will spoil his house.
Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuviteka vitu vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.

Kama ulozi uwe mlozi kweli kweli.
 
Mambo ya $$ tu. In tanzania, kwa mambo mengi sana pesa ndio ina-win. Kwa hio kama haujakaa vizuri kifedha sasa hivi, jipange. Huku ukiendelea kufuatilia kwa uwezo ulio nao ofisi mbalimbali. Ila ujue itakuwa ngumu bila pesa kutatua hilo. Na kama bado huyo mchawi ana pesa vizuri, kila ukimfunga bao, atalirudisha na kukuongezea mabao mengine. Hapo sasa ndio atalayeishiwa na $$$ mapema anasalim amri na ku-surrender. Japo unaweza bahatika bila pesa. Ila ni ngumu.
 
Nadhani hujaisoma post yangu ukaelewa chanzo cha ugomvi .. mpaka baba anafariki Hati ya nyumba lisha andikwa ni nyumba ya mama yangu na watoto wake ila alipofariki tu yule mwanamke aliyebaki ndani maana alikuwa anaishi ndani akachukua ile hati alali akaichana akaenda tengeneza yenyr jina lake .. ila kimsingi haijui hiyo nyumba imejengwaje maana mama yangu na baba yangu ndio walio ijenga na tuazaliwa hapo na maisha yalikuwa salama mpaka miaka ishirin baadaye alipokuja kuingilia huyu mama ndio maelewano kati ya baba na mama yangu yakaanza kuvurugika mama akaeondoka na sisi mm nikiwa na miaka3 tu. leo hii am 29.
 
Kama una mjua mtaalamu nguli kweli kweli njoo inbox unisaidie maana sijawahi kupractice hii.. maana naambiwa waganga wengi ni matapeli.. sasa kama kutakuwa na gwiji wakurudisha hii haki yetu nakuzuia ndugu zangu wasiendelee kuangamizwa nitashukuru sana.
 
Basi peleka kesi mahakamani.
 
kulipia ni elfu kumi ..

kapate kwanza uthibitisho wa hizo fununu then ndo uangalie hatua inayofuata,unaweza ukakuta jina wala halijabadilishwa kama ulivyoskia fununu
Asante kaka.. huwa unalipia kiasi Gani? na Je! kama itakuwa kweli ilibadilishwa.. nikakuta jina lake huyu Mama kuna njia gani naweza ifanya kupata haki yetu?
 
achukue na hii itamsaidia
 
Hili linawezekana lakini lazima awe na hati ya usimamizi wa mirathi.
Ukifika tu halmashauri au wizara ya ardhi swali la kwanza watakuuliza mhusika wa hiyo nyumba yuko wapi?
Ukijibu amefariki mimi ni mtoto wake, hapo ndio watakuomba hiyo hati sasa ya usimamizi.
Ndio maana kwenye comment yangu ya mwanzo nilisema kama hiyo hati ni Original basi itakuwa ameshirikiana na msimamizi wa mirathi waliyemteua otherwise basi itakuwa hati fake.
Cha msingi wakae kikao kama familia pamoja na wanaostahiki kurithi waandae muhtasari wa kikao cha kufungua mirathi halafu wamchague msimamizi,
Baada ya hapo huo muhtasari upelekeni ofisi ya s/mtaa au kata ukagongwe muhuri.
Bila kusahau muwe na cheti cha kifo cha marehemu (certificate of death) mnaambatanisha na muhtasari ambao umegongwa muhuri s/mtaa,kijiji au kata mnapeleka mahakamani.
Ukimaliza kufungua mirathi mtapewa hati ya usimamizi kwa mliyemchagua, yeye sasa ndio atafuatilia huko ardhi. Kwamaana nyingine msimamizi wa mirathi ndie mbadala wa marehemu.
 
Dah! Mambo gani sasa! Uchawi!!! Hakuna kitu hicho - ACHANA NA IMANI POTOFU! Nendeni ofisi ya ardhi ya wilaya baada ya kumpata msimamizi mirathi wa huyo kaka mkubwa- msianze kujiwekea vizingiti! Achaneni na uswahili!
 
Dah! Mambo gani sasa! Uchawi!!! Hakuna kitu hicho - ACHANA NA IMANI POTOFU! Nendeni ofisi ya ardhi ya wilaya baada ya kumpata msimamizi mirathi wa huyo kaka mkubwa- msianze kujiwekea vizingiti! Achaneni na uswahili!
Amini usi amini yanayotokea kwenye maisha yetu kama siyo uchawi basi ni Muujiza kutoka sayari inayo ishi kwa sayansi nyingine... kama huamin uchawi niulize mm niliyekuwa napinga sana ila sasa yamenitokea kwenye familia imebidi nielewe kuna uchawi dunian
 
Sisi tumeptia mchakato Huo ila
Tulidai mahakamani Mali(mchango wa mama Yetu katk nyumba Ile )

Zilifanyk tathamin ya mchangoz wa mama Tukapewa (mahak ilitoa umilik wa 40% wa nyumba ambako badae bab mzaz alitulpa Pesa)

NB
kumbuka hyo baba Yupo Hai KwahYo lilifanyik angalia Hai na Bado Yupo hai Sasa uko mbelen sijui itakuwaje

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 

Fanya kazi acha kugombania mali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…