Hati ya nyumba

Unaponunua uwanja ukapewa offer.je ukijenga nyumba kwenye ule uwanja unapewa tena offer?
...kiwanja au nyumba ni kitu kimoja kisheria, so ukinunua kiwanja halafu ukapewa offer/hati then ukajenga nyumba, hakuna kitakachobadilika kwenye hiyo hati yako
 
Wadau wa sheria nisaidieni sana,nilinunua kiwanja wakati Nina mgogoro na wife,nikaandika jina language maana nilijua muda wowote anaweza ondoka na ikawa hivo,akauza samani za ndani na kuondoka,nikabaki na watoto tukajenga,akarudi na sasa kaanza kelele anadai nyumba ni yake pia hivo iuzwe apewe chake,
Sasa basi kwa hali km hiyo nikiamua kuhamisha umiliki wa nyumba kuja kwa watoto na baadae tukatengana na akadai nyumba iuzwe mahakama inaweza kufuta umiliki nlowapa watoto wangu na kuamuru iuzwe
NB.watoto sikuzaa nae ila tumeishi nao muda wote,yy Nina mtoto mmoja nae,nataka niwape umiliki hawa alonikuta nao kuepusha kuporwa nikiwa sipo hai
 
...kiwanja au nyumba ni kitu kimoja kisheria, so ukinunua kiwanja halafu ukapewa offer/hati then ukajenga nyumba, hakuna kitakachobadilika kwenye hiyo hati yako
Mkuu Nina swali langu hapo juu naomba kamsaada nimekwama
 
Mkuu Nina swali langu hapo juu naomba kamsaada nimekwama
...okay, 1. ningependa kufahamu kama mmefunga ndoa?
2. je mlipeana talaka wakati mnaachana, au aliondoka tu kiaina then amerudi?
3. na unaposema amerudi, unamaanisha karudi muishi au kudai mali?, na kwa sasa anaishi wapi?
4. kwa sasa anaishi na mwanaume mwingine?
5. ni muda gani umepita tangu alipoondoka?
6. vipi kuhusu hivyo vitu vya ndani alivyouza, thamani yake, na je mlikubaliana aviuze?.

naomba unijibu hayo maswali, nitakusaidia, lakini pia kwa hivyo vichache ulivyovieleza hapa, ana nafasi ndogo sana ya kushinda kesi endapo ataenda mahakamani, na kama umeandika majina ya watoto, kwa utashi wa mahakama hawataweza kuhamisha huo umiliki kwenda kwa mtu mwingine, kwa kuwa mahakama inalinda zaidi haki za mtoto.
karibu
 
Tulifunga ndoa kanisani,na wamenipa barua ya kwenda mahakamani,wakati anaondoka hatukupeana talaka maana alitoroka na hata baadhi ya samani za ndani alizouza alivizia sipo akaiba na kuuza,nilitoa taarifa polisi na nna rb,aliporudi palipita suruhu ya kidini,lkn ujeuri wake umerudia vile vile,
Kinachonikwamisha sana ni muda wa kufuatilia kesi,maana mwenzangu anajua nimebanwa na muda hivo analeta usumbufu sn ili kukwamisha,nimewaza kuwamilikisha Mali zangu pamoja na nyumba wanangu ili km shortcut ya mgogoro lkn sijui baada ya kuwamilikisha nyumba watakuwa na mamlaka full juu ya nyumba na je wanaweza kumuondoa yy ili waipangishe?,maana nnawaza kuchukua watoto wote nikakae nao kazini kwangu maana mdogo ana miaka 7wakubwa wana 17,napo sijajua sheria imekaaje kwa hilo,lkn kwa kifupi nimekamatika balaa
 
Unawaachia urithi (mjifunze kuandika wosia) ila mahakama huwapa watoto.

Nje ya mada..... mwandiko wako umenikwaza....kama maliiii na nduguuuu ndio kitu gani???
Maliii = mali
Nduguu = ndugu
Inakuwajeeee= inakuwaje
Hapooo = hapo
Atakuwa Chalii Huyoo
 
Bado hujamjibu swali la huyo mwanamke anaishi wapi kwa sasa na ana mwanaume anayeishi naye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…