...okay, 1. ningependa kufahamu kama mmefunga ndoa?
2. je mlipeana talaka wakati mnaachana, au aliondoka tu kiaina then amerudi?
3. na unaposema amerudi, unamaanisha karudi muishi au kudai mali?, na kwa sasa anaishi wapi?
4. kwa sasa anaishi na mwanaume mwingine?
5. ni muda gani umepita tangu alipoondoka?
6. vipi kuhusu hivyo vitu vya ndani alivyouza, thamani yake, na je mlikubaliana aviuze?.
naomba unijibu hayo maswali, nitakusaidia, lakini pia kwa hivyo vichache ulivyovieleza hapa, ana nafasi ndogo sana ya kushinda kesi endapo ataenda mahakamani, na kama umeandika majina ya watoto, kwa utashi wa mahakama hawataweza kuhamisha huo umiliki kwenda kwa mtu mwingine, kwa kuwa mahakama inalinda zaidi haki za mtoto.
karibu