Hati ya usalama wa moto

Newland

Member
Joined
Oct 20, 2012
Posts
29
Reaction score
6
Naomba msaada wa kisheria hapa. Hawa jamaa wa kikosi cha zima moto wanapita katika maduka hapa babati na kuwalazimisha watu watoe hela Tsh 40,000/= kwa ajili ya certificate ya usalama wa moto. Wanadai wanafanya hiv kulingana na sheria ya jeshi la zima moto na uokoaji Na 14 ya 2007, kifungu cha 32(g).

Pia wanasema ada rasmi ni Tsh.100,000/= ila wao wamepunguza kulingana na mazingira halisi ya watu.

Hii ada wanadai ni fomu ya maombi ya hiyo hati. Ila swala la mtungi wa gesi ni juu yako. Hata hivyo wanadai pia hii ada ni kila mwaka.

Naomba msaada tafadhali.
 
ndg yangu huo ni wizi wa kulazimisha.wenye magari kadhalika tunalazimishwa kulipia hiyo kitu tunapohuisha road license. hii Nchi bwana we acha tu.
 
Tunaomba sana Serikali iingilie kati suala hili. Walikuja kwenye hoteli yangu wakadai niwalipe Tshs.500,000 nilipowauliza nini nitapata kutoka kwao wenyewe wakasema kuwa wanatoa tu cheti cha kujisajili. namwomba Mhe. Waziri ya mambo ya ndani aingilie suala hili kabla haijaleta madhara makubwa kwa watumishi wake kwa sababu tunauonekama wizi wa mchana. Unatoa Tshs. 500,000 hupati hata mtungi wa gesi wa kuzuia moto eti wanasema kuwa tunakupa cheti. WEZI WAKUBWA HAO.
 

Jamani acheni kulalamika amkeni!
Tena wafanyabiashara kwa kuichangia Serikali (CCM) iliyokwishachoka mnaongoza!

Hiyo ni zimamoto tu 500,000/12=41666.6@Month.Bado jamaa wa Afya na TFDA,OSHA na wengine
Kinachokera ni hakuna huduma yoyote ukipata majanga unakufa na majanga yako bila Msaada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…