JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo, Septemba 11, 2024 imesikiliza pingamizi lililowekwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambalo limeiomba Mahakama kuiondoa kesi hiyo kwa sababu Katiba za TFF, CAF na FIFA zinazuia masuala ya mpira kupelekwa Mahakamani.
Kesi hiyo Namba 14708 ya Mwaka 2024, awali ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi, Anna Magutu lakini leo imesikilizwa na Hakimu Mkazi F. S Kiswaga kwa sababu ya taratibu za kikazi kuingiliana.
Hata hivyo, pingamizi hilo lilipingwa na Wakili Peter Majanjara anayemwakilisha, Kocha Liston Katabazi ambaye aliiambia Mahakama kuwa si kweli kwamba suala la mteja wake halipaswi kupelekwa Mahakamani kwa hoja kwamba pingamizi lililowasilishwa sio la kisheria.
Majanjara alisema pingamizi hilo linataka kuleta ushahidi kwa sababu ibara zote zilizowasilishwa na TFF ambazo ni 64, 66 na 67 zinahusu Wanachama wa TFF kwa hiyo utahitajika uthibitisho iwapo Katabazi ni mwanachama au sio mwanachama wa TFF.
Pia, aliendelea kuieleza Mahakama, Katiba ya TFF sio Sheria ya nchi iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inawahusu watu waliopo ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tofauti na Katiba ya TFF inayohusu wanachama wake saba ambao wametajwa kwenye katiba ya TFF ibara ya 12.
Pia aliiomba Mahakama isikubali pingamizi hilo la TFF kwa sababu hata katiba yenyewe ya TFF inabishaniwa uhalali wake katika kesi ya msingi ya Katabazi.
Soma Pia:
Katika kesi hiyo, Katabazi anaidai TFF shilingi milioni 700 kutokana na chapisho lililotolewa kwa umma, Juni 24, 2021 ambalo lilitangaza kumfungia kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu, ndani na nje ya nchi maisha yake yote.

- TFF yaiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuiondoa kesi ya Liston Katabazi Mahakamani
- Liston Katabazi kuiburuta TFF Mahakamani na kuidai Sh Milioni 700