Kweli, most likelyKang asemayo ni sahihi. Ila hao serikali hawajui kwamba kuna kundi kubwa sana nyuma ya DECI, sio ajabu chama chao serikali kikajikuta katika wakati mgumu kama wananchi wataitumia vema silaha ya kuporwa na serikali kupitia mgongo wa DECI. Wapo watakaoitumia kama silaha katika kuwashikisha adamu majitu yanayojiita serikali.
Kwanza DECI haikushindwa kuwalipa wanachama wao, serikali ndio imevuruga taratibu za DECI na kuwafanya wasiweze kulipa. Mie sijasikia hata mtu mmoja anayelalamika kutapeliwa pesa zake na DECI hadi pale serikali yenyewe ilipoamua kuwatapeli watu, tena ati kwa maelezo kwamba DECI ingeua taasisi za fedha kwa watu kumiminikia kwake na kujiondoa kwenye mabenki, FINCA, nani sijui yule wa Mr Simba? nk.
Ndiyo EPA ya ndani sasa. Hata wanasheria wataifanyaje serikali ambayo ikishindwa hukimbilia bungeni kutengeneza rubberstamp ya mswada wa kuipa kiburi zaidi? Hukumbuki Mtikila na Mrema wameishinda serikali ikang'ang'ania ujeuri wake?
Leka