Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kaitaba, bado una imani ya kupata pesa ulizopanda DECI? kwa sasa hakuna kinachoendelea hiyo ndo imeshatoka hivyo,fikiria njia nyingine za kupata pesa uweze kuendeleza maisha yako,wala usiruhusu DECI ikuchukulie muda wako kwa kuwaza kuwa ni nini kinachoendelea.
Kwa wale wote waliokuwa wanashiriki mchezo wa upatu wa kupanda na kuvuna DECI Mabibo, tupeane mawazo nini cha kufanya, hivi pesa zetu zipotee hivi hivi kweli!!!?
Kwa wanaojua kinachoendelea tujulishane basi,
ThinkPad, pole kuna mtu kaelezea amount inayoshikiliwa na serikali ni kidogo kuliko deni mnalodai. Mi naona ushauri wangu wana DECI wangeungana na kutafuta mwanasheria awashauri nini wafanye;
wakubali kugawanywa pungufu ya madai yao ili wote wasiowahi kuvuna walipwe. waandike makubaliano hayo na kuyapeleka serikalini kama itakubaliwa.
ni ushauri tu maana naona wanasota sana na wengine kuchanganyikiwa kwa madeni