Hatima ya elimu yetu bila suluhisho la kudumu

Hatima ya elimu yetu bila suluhisho la kudumu

MNYOO JOGOO

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
195
Reaction score
94
Mengi yamezungumzwa kuhusiana na kuporomoka kwa elimu yetu nchini. Zaidi, yote haya yanatokea tukiwa hatujapona vidonda vya kupotezewa na ndugu zetu walioathirika na matokeo ya hivi karibuni. Wengine walijinyonga, wengine walikunywa sumu,wengine wamejiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa kukata tamaa, wengi wao wakipoteza kabisa matumaini ya kuwa na maisha bora n.k.
Nilipata fursa ya kuzungumza na rafiki wa kijana aliyeamua kuweka rehani uhai wake kwa sababu ya kufeli mtihani wa form IV, Inasikitisha sana kwani nimekuja kufahamu kuwa kumbe kijana yule aliyafanya haya kwa sababu maumivu makubwa aliyopata baada ya matokeo hayo. Kijana huyu alikumbuka jinsi alivokuwa akiamka saa 11 aljiri kwenda shule iliyokuwa umbali wa 20km, alikumbuka pia alivyokuwa analazimika kushinda njaa shuleni kwani asingeweza kurudi mapema nyumbani ili apate fursa ya kujisomea shuleni hapo, akirudi nyumbani alilazimika kuwasaidia wazazi kazi za bustani na usiku aliwasha kibatari na kuanza kujisomea japo wazazi walimuomba kutowasha kibatari kwa mda mrefu sana kwa mafuta yangeisha na kama ilivyo kwa watanznia wengi hawakuwa na kipato cha kudumu zaidi ya kuhangaikia hela ya kuweka chochote tumboni.

Maisha ya familia hii yalikuwa ni duni kama tulivyo watanzania wengi, hivyo matumaini makubwa yalikuwa ni kwa huyu kijana kuwa Mungu akimsaidia angeweza kuja kuwasaidia wazazi wake.

Nikajaribu kutafakari hili kwa jicho la tatu na kujiuliza: sawa kijana huyu alikuwa akipenda shule kiasi hiki nampongeza sana. Sawa kijana huyu alikuwa na matumaini makubwa na aliipenda shule akijua ingemkomboa baadae, nampongeza pia. Kijana huyu kadri nafasi ilivyomruhusu alijitahidi kuwasaidia wazazi wake kwa kazi za hapa na pale kadri alivyokuwa akipata fursa, nampongeza zaidi. Kijana huyu alifanya mengi ambayo yanafaa kuigwa katika jamii hii ambayo tumekumbwa na kasumba ya vijana kujiita sharobaro, sista duu, wakinyoa viduku n.k.

Nilapata fursa ya kutembelea shule hii ambayo naambiwa ndio kwa mara ya kwanza imetoa form four, wengine wanaziita shule za kata. Shule hii inawaalimu wanne wakifundisha kuanznia form I - IV. Nimeenda mbali zaidi na kufuatilia profile ya walimu hawa nikagundua kuwa kati yao hakuna hata mmoja mwenye matokea ya Div III hata ya point 25, wote wameanzia Div IV - 27.
Walimu hawa wenye matokeo dhaifu ndio ambao tumewakabidhi majukumu ya kuandaa rasilimali watu ya baadae.

Vidonda hivi vya kuwa na walimu waliofeli huku tukitarajia kupata ufaulu mzuri vimetoneshwa juzi nilipoona watu mbalimbali wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano huku pakiwa na upungufu wa wanafunzi walifaulu kujiunga na kidato cha tano zaidi ya 10,000. Wengine wakipangiwa vyuo mabalimbali kadri wizara ilivyoona wanastahili.

Chumvi katika kidonda iliniumiza nilipoangalia watu waliopangwa kwenda vyuo vya ualimu, wizara imeendeleza kasumba ileile ya kuchukua watu waliofeli kuendelea kuwa msingi wa elimu yetu Tanzania.

Nakumbuka nikiwa nimemaliza form six mjomba wangu alihakikisha ananikatisha tamaa ya kuwa mwalimu japo nilikuwa naweza kufundisha na nikiwa na Div I - 5. Alikuwa akiniuliza Je, ni mwl yupi ambaye umeshawahi kuliona shati lake ukalitamani? Kwa swali hili nilivunjika moyo sana na kuamua kwenda kusoma Telecom. Baadae nikwa nakumbuka swali la mjomba wangu nikangudua kuwa kuwa; Inawezekana nisiweze kutamani shati alilovaa mwalimu LAKINI je? Mwalimu huyu anwezaje kuwa na sharti la walau Ts 25,000?= wakati kununua shati hilo anakuwa ametumia asilimia 20% ya mshahara wake?

Serikali inatakiwa ione umuhimu wa hii sekta ukizingatia hakuna taifa lolote duniani ambalo linaweza kuendelea bili kuwa na rasilimali watu na rsilimali watu huandaliwa kwa mazingira mazuri, mfumo mzuri na watu walimu sahihi.
 
wanafunzi waliofeli ni baadhi tu, watoto wamekuwa na maisha magumu miaka mingi

ushauri kwenu vitu viwili tu baasi

  1. Fanyeni hima wahusika wasihangaike wawalipe walimu pesa na za watoto kama hao wenye mazingira magumu, mbona wabunge wanalipwa mfuko wa jimbo?
  2. Wanaokwenda ualimu wawe na ufaulu wa Div I na II , mshahara ukiwa mnono lazima watagombea kwenda education, na wale waliokazini watafanyakazi usiku na mchana.

NB Mengine yoote ni kujisumbua, serkali na wadau wake watapiga kelele hadi ardhi ipasuke endapo hawatatoa mtisha wa kipato kwa walimu na kuihuisha kazi kuwa yenye thamani na kuwekeza vipaji vya watoto vyuoni

kwa nini walimu wasilipwe fedha ya kuvumbua vipaji vya watoto na kuviendeleza, je nani hajui ushauri ndio eneo pekee la kumkomboa kijana anaekua? anaebalekhe?
mnajifanya hamjui mpaka tume ziunde,

Nisaidieni nijue tume ya pinda iliyolipwa mapesa imekuja na faida ipi ya suluhisho la haraka/mapema na muda mrefu kuhusu elimu na mazingira ya elimu.

Eti wamechukua wakuu wa shule kama sehemu ya tume nani aliwaambia wakuu washule wanajua matatizo kuliko walimu walau walimu wa malezi na nidhamu? Kudanganyana kutatupelekea vitani Tanzania

Fumbeni macho, mjue mkijafumbua vita inapiganwa, wanafunzi wasioelewa mbinu na taratibu mbalimbali ni dhahiri watalipeka Taifa hili katika fujo na kutoelewana, watakuja kupambana kwa njia zote kwa kuwa wanajua walidanganywa, aliekuwa madarakani au tajiri au mkubwa asidhani kwamba atapona, zaidi ya kushuhudia wananchi maskini waliowengi wakiamua kujiunga na vikundi mbalimbali kutetea watakachokiamini wakati ukifika.

Tanzania ni nchi yenye watu wanaoishi kwa matumaini.
 
wanafunzi waliofeli ni baadhi tu, watoto wamekuwa na maisha magumu miaka mingi

ushauri kwenu vitu viwili tu baasi

  1. Fanyeni hima wahusika wasihangaike wawalipe walimu pesa na za watoto kama hao wenye mazingira magumu, mbona wabunge wanalipwa mfuko wa jimbo?
  2. Wanaokwenda ualimu wawe na ufaulu wa Div I na II , mshahara ukiwa mnono lazima watagombea kwenda education, na wale waliokazini watafanyakazi usiku na mchana.

NB Mengine yoote ni kujisumbua, serkali na wadau wake watapiga kelele hadi ardhi ipasuke endapo hawatatoa mtisha wa kipato kwa walimu na kuihuisha kazi kuwa yenye thamani na kuwekeza vipaji vya watoto vyuoni

kwa nini walimu wasilipwe fedha ya kuvumbua vipaji vya watoto na kuviendeleza, je nani hajui ushauri ndio eneo pekee la kumkomboa kijana anaekua?

Ni ukweli kinene
 
Back
Top Bottom