Uchaguzi 2020 Hatima ya Uchaguzi wa 2020

Uchaguzi 2020 Hatima ya Uchaguzi wa 2020

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Posts
1,203
Reaction score
1,422
Nini hatima ya uchaguzi wa mwaka huu? Mwaka 2015 CHADEMA walikuwa wakisema wakiingia madarakani, watafufua Shirika la ATC, watafanya shule bure, n.k. Magufuli ameyafanya hayo, na zaidi. Sasa wanageuka na kumkosoa kwamba kununua ndege siyo kipaumbele cha Taifa. Wanapotosha zaidi kwa kukariri out of context aliyoyasema Mwalimu kwamba maendeleo siyo vitu. Hivi ni kweli kusambaza vituo vya afya nchi nzima, kupeleka umeme na maji vijijini, n.k. kote huko siyo kuwaletea maendeleo wananchi? Wiki jana mvua zilinyesha Dar ikafurika. Mwingine akaandika humu JF kwamba yuko kwenye foleni kwa saa 10 kwa sababu ya ubovu wa miundombinu. Magufuli akijenga flyovers zinazoondoa adha ya kupoteza muda na mafuta kwenye foleni mnasema maendeleo siyo vitu.

Kwenye mikutano ya kampeni Lissu amekuwa akitumia robo tatu ya muda kumlaumu Magufuli na muda kiduchu tu kusema atafanya nini akishinda. Anajaribu kuwahadaa wapiga kura kwa kila mbinu. Kwa mfano anajaribu kuwateka Waislamu kwa kusema kwamba atawaachia mashehe walioko kizuizini ndani ya siku 100 za kuwa Rais. Ni dhahiri kwamba anaingiza mambo ya dini ambapo kushikwa kwa mashehe hao kulifanywa na Rais Kikwete ambaye ni Muislamu.

Ingekuwa ni suala la dini, Kikwete asingefanya hilo. Lissu anakosoa pia wamachinga kuwa na vitambulisho ambapo wao wenyewe wanasifia hilo kwani sasa hawasumbuliwi na watendaji wa manispaa wakionyesha kitambulisho. Kila nchi ina masharti yake ya kufanya biashara. Hata London au New York huwezi ukaanza kujifanyia biashara kivyako tu bila kufuata sheria za manispaa. Anatafuta kura kwa kuchochea ghasia nchini.

Aidha, Upinzani umekuwa ukipiga kelele kuhusu Katiba. Wiki jana kulijitokeza wanachama wa ACT wakilalamika kwamba viongozi wao Zitto na Maalim Seif wamekiuka Katiba yao. Mtoa mada mmoja hapa JF akajitokeza na kuuliza uanachama wa hao wawili ulianza lini, kama vile kuwa mwanachama wa muda mrefu zaidi kunakufanya kuwa mwanachama zaidi kuliko aliyejiunga hivi karibuni. Anasahau kwamba Maalim Seif na Membe wamejiunga ACT miezi michache tu iliyopita na tayari wamewekwa wagombee Urais wa Zanzibar na wa Jamhuri bila kuangalia lini walijiunga na Chama. Ni dhahiri kwamba kutetea ACT ni kwa minajiri ya kutetea tu na si kwa sababu kuna hoja ya msingi.

Wanachama hao wawili waliokosoa kuvunjwa Katiba ya Chama chao walikariri hata vifungu vilivyovunjwa. Sasa ni nini hasa anachopinga mtoa hoja wakati mambo yako wazi hivyo? Mtu ujiulize hata hiyo Katiba ya nchi inayopigiwa kelele na upinzani kwamba iandikwe upya, jee itakuwa ya kuweka kabatini tu isitumike kwani ndivyo hivyo ilivyojidhihirisha kwa Katiba ya ACT? Hao wanaopiga kelele kuhusu Katiba ya nchi, wengi wao wala hawajui Katiba ina vifungu vingapi. Ukimuuliza mmoja akutajie kasoro za vifungu vitano tu ni wachache sana watakaofanya hivyo.

Na bado mtu anapiga kelele kwamba Katiba iandikwe upya na si kurekebisha tu. Ni dhahiri kwamba zote hizo ni kelele tu za kuonyesha kukosoa. Hata hapa JF upinzani wakizidiwa kwa hoja wanaishia kusema njaa tu inamsumbua mtoa hoja anayemtetea Magufuli; au anataka kuteuliwa kwenye wadhifa fulani; au amenunuliwa na CCM. Wenyewe walioshiba hawawezi wala kukosoa hoja zilizowekwa na mtoa mada.

Shime Watanzania. Tumebakiwa na saa 24 tu. Tufanye la maana kwa kumpa kura Magufuli amalizie aliyoyaanza na mengine zaidi. Kama binadamu, naye ana mapungufu yake. Lakini ukilinganisha kwenye mizani mazuri na mabaya yake, mazuri ni mengi zaidi. Tusidanganywe na porojo za upinzani ambazo zimejitambulisha wazi kuwa ni porojo tu. Tuchague mtendaji na si mtoa porojo. Magufuli Oyee! Miaka mingine mitano.
 
Back
Top Bottom