GE2025 Hatima ya watia nia CCM waliopenya, kuliwa kichwa kuwekwa hadharani kuanzia Julai 19, 2025

GE2025 Hatima ya watia nia CCM waliopenya, kuliwa kichwa kuwekwa hadharani kuanzia Julai 19, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Hatima ya wagombea waliopenya, kuliwa kichwa kuwekwa hadharani!

CCM inatarajia kutangaza majina matatu ya wagombea ubunge na udiwani kwa kila jimbo na kata ndani kuanzia leo, baada ya kikao cha Kamati Kuu Julai 19, 2025. Mchujo umehusisha maelfu ya watia nia, huku viongozi wakisisitiza subira na kufuata taratibu rasmi.

Watia nia wako kwenye hali ya tumbo joto, wakisubiri kwa presha kubwa kujua kama majina yao yatakuwa miongoni mwa yale matatu yatakayopitishwa rasmi kupigiwa kura.

Kwa ubunge, jumla ya makada 4,109 walitia nia kugombea majimbo 272, huku wagombea wa udiwani wakiwa zaidi ya 30,000 kwa kata 3,960. Mchujo ulianza katika ngazi ya kata, kisha wilaya na baadaye mikoa, ambapo kamati zilipendekeza majina matatu kwa kila nafasi na kuyawasilisha kwa ngazi ya Taifa.

Tangu Julai 14 hadi 18, 2025, Sekretarieti ya CCM Taifa chini ya Katibu Mkuu Dkt. Emmanuel Nchimbi imeendelea kuchuja majina hayo.

Hatua ya mwisho ni kikao cha Kamati Kuu ya Julai 19, 2025 kitakachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya kufanya uteuzi rasmi.
 
Back
Top Bottom