Hatimae Hawa wa Nitarejea afanyiwa operation ya moyo salama.

Hatimae Hawa wa Nitarejea afanyiwa operation ya moyo salama.

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Kwa mujibu wa Meneja wa Diamond Platnumz,Babu Tale,msanii Hawa aliyeshirikishwa kwenye wimbo wa nitarejea wa Diamond amefanyiwa operation ya moyo salama kwa masaa matano,Tale ameandika kupitia kwenye akaunti yake ya instagram kuwa msanii huyo amezinduka na anaendelea vizuri,mambo yakienda sawa watarejea Dar es salaam baada ya wiki moja.

Hawa alisafirishwa kwenda India kwenye matibabu kwa msaada wa CEO wa wa WCB Chibu Dangote,ambapo safari hiyo pamoja na matibabu yamegharimu shilingi za Kiganzania Milioni 50,awali ilidaiwa kuwa dada huyo anaugua ugonjwa wa ini kutokana na athari za madawa ya kulevya na pombe lakini madaktari nchini India walibaini kuwa ugonjwa unaomsumbua Hawa ni moyo unaopelekea mwili na timbo kujaa maji.

Kwa niaba ya members wote wa Celebrity forum na Jf kwa ujumla,napenda kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Media Nasib Abdul kwa moyo wa kufanikisha matibabu ya Hawa🙏.
Screenshot_20181024-150001.png
Screenshot_20181024-150015.png
 
Allah amjaalie uzima na afya njema..bila kusahau allah amfanyie wepec zaidi diamond na team katika utafutaji wao wa rizki...hii ndo maana ya ninachokipata nagawana na wenzangu.

pamoja na mambo mengine ila diamond ana utu sana aise,nazani ndo maana Mungu amekuwa akimyooshea sana upande wake aliouchagua katika kujitafutia mkate wake.
 
Kuna watu hawapendi hii jambo,na hutawaona kwenye huu uzi,ila ndo Ruge angekua amegharamikia hiyo matibabu ungeona wanavyomtusi kijana wa watu,so SAD !!
 
Power of social media bila hivyo hawa asingepata msaada
 
Bongo kweli nyoso!
Hospitali za huku kwetu si ndio walimuaminisha kuwa anaumwa ini?
Leo ndio naamini kuwaa wengi wetu Tz tunazikwa tukiwa hai. Mungu ampe nafuu Hawa ili aje aendelee namajukumu yake ya kila siku, awazidishie wale wote waliofanikisha hili pia.
 
Kuna watu hawapendi hii jambo,na hutawaona kwenye huu uzi,ila ndo Ruge angekua amegharamikia hiyo matibabu ungeona wanavyomtusi kijana wa watu,so SAD !!
Tatizo hata hapa umeandika kiteam zaidi hii ishu jamaa kafanya vizuri kujitolea sio lazima ashukuriwe na wote kwasababu hata msaada kapata Hawa na hajafanya kwa ajili ya watu so Ruge anaingiaje hapa?

Samahani lakini mimi sio team Ruge wala Diamond!!
 
Mungu mwingi wa rehema, mjalie mja wako,

Hawa apate kupona, kwa heri na nema zako,

Alejee kwa salama, muweke mikononi mwako,

Twakuomba maulana, timiza mapenzi yako.
 
Tatizo hata hapa umeandika kiteam zaidi hii ishu jamaa kafanya vizuri kujitolea sio lazima ashukuriwe na wote kwasababu hata msaada kapata Hawa na hajafanya kwa ajili ya watu so Ruge anaingiaje hapa?

Samahani lakini mimi sio team Ruge wala Diamond!!
hujanielewa
 
Hondera Mondi ndio ubinadamu, Pia kijana huyu ana akili sana hatoi msaada kifala, kahakikisha anamkabidhi mtu anaemwamini asimamie zoezi lote. Turudi kwa Wastara michango anapewa yeye, kanula anaweka mwenyewe anapiga picha halafu ananunulia biasharafedha za michango, anakuja kuwauzia waliochangia. Ndio maana wenye akili hawampi hata sumni.
 
Wastara bana daah😂😂😂
 
Back
Top Bottom