Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Moja ya kitu kinanitoa machozi mpaka sasa ni watoto wangu. Ila nimeamua acha nikubali lolote litakalojili juu yao angalau kwa hii miezi 6 ya mwanza mpaka mwaka. Kila jambo linahitaji muda, hayawez yote kuwa resolved kwa wakat mmoja.
Nitapata ufumbuzi tu bila shaka. Acha akae nao kwanza maana si ndio anachotaka, wala sitashindania watoto.
But after sometime najua nitakapowataka ,atakua ame learn a lesson na nitawapata kirahis bila nguvu wala shuruba.
Ujue wawili ni wawili tu, hata asiposema akaendelea kukomaa like she handles everything bila tabu, ila najua kuna somo atajifunza tu
 
nakuelewa sana, mimi nilihama kabisa nikaanza mji kwingine nijue watu wapya.
yu need kuhama yes!
ENEO JIPYA huja na mengi mapya!
USIIINGIE KWENYE MAHUSIANO sasahivi.
Unahitaji kujiponya ndani kwanza kabla ya kujiponya nje.

Ngumu but with time utakuwa sawa!
ALL THE BEST!
 
Kesi nyingi ni za ndoa na ardhi katika mahakama zetu,asante umepunguza moja hio.
Hongera sana,trust me Leo maisha yake ya majuto yanaanza rasmi.
Ahahahah..yule bidada hakimu mwenyewe niliona jinsi alivyo furahi kiasi kwamba anashindwa kujizuia akasema "dah hii kesi imeenda vizur sana, kiasa kwamba kuna utata wife alikua akitaka kuanzisha akawa anampa facts like amekaa upande wangu. Kuna time yf akataka kuanzisha utata wa gharama za matibabu, hakimu akasema wewe ni mtumishi wmwenzagu wa serikali, hao watoto wana bima na ulipia automatically , heb acha hizi bwana, halaf mbona umechukua gharama ndogo sana kuliko mwenzako." 😂😂
 
Duh ubaya ubwela
 
HII NATAKA KUKUASSURE!
utakuwa sawa, watoto watakuwa sawa.
Jitengeneze kwanza ili hata USIJE KULEA WATOTO UKIWA A WOUNDED PARENT!

Miezi sita mwaka mbali na kila kitu kila mtu will make it!
Baada hapo rudisha mpira mezani kuhusu namna ya kulea wanao.
 
Kama hayajakufika utaona kawaida
Ila ndugu yangu alipelekeshwa saaaana na mambo haya. Yani swala lako ni copy and paste na lake sema kwenye mgawanyo bi dada aliangukia kamasi na vile la saba la mkoloni hakujua afanye nini amebaki kugomea kwa mume. Waliokuwa wanamdanganya na kumuona mzuri na uzee ule kwamba watamuoa wamemkimbia
Hana hata geto la chumba kimoja
 
Shukram sana mkuu
 
Daah! Umetumia hekima... ungeanza ubishi tu!! Angeona kakuweza angezidi kukusumbua hadi ungeona dunia chungu..

By the way,,,,, alikutafuta au kukutumia ujumbe baada ya kutoka mahakamani?
Hatuwasiliana toka siku kaondoa mguu nyumbani mkuu. Mama huyu ni jeuri kupita maelezo. Nilipata tabu kuzoea hii hali
 
Aliyekiukwa haki, ndiye amekubali yaishe.
hamna kesi hapo,
Kuna msimamo mmoja wa kisheria ulitolewa kwenye moja ya kesi maarufu unasema ''sio tu haki itendeke, bali ionekane ikitendeka'' sasa kwenye kesi ya jamaa hayo hayajafanyika, kama siku moja Hakimu Mfawidhi akikutana na hilo jalada na uhakika atalifanyia marejeo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…