Movic Evara
Senior Member
- Jan 31, 2018
- 197
- 431
Pole sana mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shukran chief. Maendeleo si mabaya katika kuponaPole sana mkuu
Yani mimi nimekuelewa mnoo!Inauma sana, unapimaaaaaa unaona maumivu ya kushikilia ni makubwa kuliko ya kuachilia vipoteee. Japo ukiwaza nguvu yote ya ujana unaiona ileee inakwemda na maji uanze upya, aisee maumivu yake sio madogo ila unaona sawa tu
TRUST ME!Sina cha kuongezea mkuu.
Ujue nimekuja kugundua kwenye maisha huna haja ya kujiua kwasababu unapitia shida flan, maana kila unachopitia wewe sasa, kuna watu wameshapita huko kitambo, exactly the same au more morse than yours ,so kikubwa ni kufunguka ili usaidiwe. Utajiona mbona wewe yako madogo???
Mkuu hongera sana na big up japo nakuonea wivu wewe tayar una 5 yrs wakat mimi ndio naanza kuhesabu miezi 😂😂.
Nitazoea tu na mimi
Well done..Tusubiri Karma..Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.
Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu
Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali
Wakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu. Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana. Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya...www.jamiiforums.com
"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.
Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
- nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
- leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
😁😁😁😁😁.
Anyway,.
Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.
Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"
Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto
Akauliza "unasemaje?"
Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"
Akauliza "umekubaliana na haya yote?"
Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"
Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.
Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.
Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.
Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.
1. Talaka.
Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.
2. Mgawanyo wa mali.
Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.
3. Matunzo ya watoto
Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.
4. Kuishi na watoto.
Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.
Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.
Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"
Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"
Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.
Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.
Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.
PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.
Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.
Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.
Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!
Ikaisha hivyo.
Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.
ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani
SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema
Umesema ukweli hapo kweli Dawati la jinsia nilimshauri jamaa akiitwa hasiendeMkuu kama ulivyoeleza kuwa haufahamu masuala ya kisheria sikulaumu hata kidogo.
Taratibu za kesi za ndoa/talaka zinaanzia Baraza la usuluhishi.wa ndoa ambap kunaeza kuwa Baraza la kata au Bodi chini ya taasisi ya kidini, huko mnachukua Fomu namba 3 tu.
Sasa hii Fomu namba tatu,inaelezea jambo moja tu kuwa barazalimejaribu kusuluhisha lakini limeshindwa. Baada ya hapo ndio mnaenda sasa Mahakamani moja kwa moja sasa hii maana yake ni kuwa Mahakamani hamtakuwa na habari ya usuluhishi tena bali ni kesi moja kwa moja yaani ni kutoa ushahidi na kupokea utetezi.
Sasa tukirudi kwenu, utaona mmeenda mkaanza usuluhishi tena Mahakamani, na ukiangalia Mahakama imegeuka kama sehemu ya nyie Wadaawa adala ya kuwa kimya ipokee ushahidi na utetezi wa Mdai na Mdaiwa.
Hapo ndio shida imeanzia na kuivuruga kabisa kesi nzima. Na hili lote naelekeza lawama kwa Mh. Hakimu husika sababu amefanya asiyotakiwa kufanya na kafikia hitimisho bila kupokea ushahidi rasmi na utetezi rasmi.
Yaani kaendesha hiyo kesi kama mpo ofisi ya kijiji 😂. Bado tuna safari ndefu sana kwenye huu mhimili.
Si umeona hata wewe umeamini kuwa utaratibu wa kushuhulikia kesi ya mgogoro wa ndoa unaanzia sijui dawati la jinsia na hizo ngazi zingine ulizozitaja hapo juu. Hii sio kweli na huo sio utaratibu uliowekwa na sheria. (Bado sikulaumu sababu haukua unafahamu hili)
Utaratibu wa kufungua kesi ya mgogoro wa ndoa/talaka ni hatua mbili tu;
1. Baraza la Usuluhishi wa ndoa Kata au Bodi ya usuluhshi wa ndoa chini ya taasisi za kidini
2. Mahakama.
Hizo njia nyingine zote hazipo kisheria na hazitambuliwi na sheria zinazosimamia masuala ya ndoa.
Axactly... japo kwa mfumo wa barafu kuwa ya moto!We grow by going through stuffs