Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Natamani ningejua sababu za kuachana kwanza

Hakunaga binadamu mkamilifu mkuu
Huyo unayetegemea kuja kumuo baada ya huyu mida hii watu wanajisevia tu

Kwa maelezo yako inaonekana wote bado hamja move on
Inaonekana ego zenu ndio ziliwagombanisha
 
Mkuu, pole sana kwa yaliyokukuta.


Mungu akupe nguvu. Natamani kujua baada ya miezi mitatu kupita nini kinaendelea
 
HAmna mkuu, sio plan yangu kwasasa chief
Sema na moyo wako peke yako mkuu...... hakuna anayekujua vizuri hisia zako zaidi ya wewe unavyozijua kwenye hii issue yako.

Binafsi niliwahi kumuacha mwanamke wa maisha yangu kwasababu za KIPUUZI kabisa, nikatumia muda mwingi kujishawishi na kushawishi wengine kwamba yule alikua HAFAI...... Lakini deep down kwenye uvungu wa moyo wangu nilikua NATATIZIKA kwa puuzia ukweli
Nilizika yote na sasa tunaishi pamoja.
Kwenye mahusiano EGO ni mbaya sana, lazima awepo mmoja wa kui balance

BTW mwisho wa siku kama hamta rudiana basi utakuja kuoa tu, huwezi kukaa single forever
Hapa sasa utakuja kukutana na mwanamke ambaye muda huu unapuyanga tu kazoea kuruka ruka, unakuja kumuoa β€œuzeeni” unakuja kujitafutia presha bure..... bora mlioanza naye ujanani mkuu

Sema na Moyo wako mkuu
 
Wewe umeongea maoni yako...ila jamaa kafanya kitu safi kabisa...mali inamdrive mwanamke kuvunja ndoa..wakati huo anategemea scuffle kali sana! Sasa ukifanya tofauti unamsuprise...akili ikija kukaa sawa wewe uko mbali mno!
 
Nimekuelewa chief. Ila not after all what happened. Probably sababu zilizokufanya muachane na kurudiana hazilingani na za kwangu.
Ila i appreciate your concern Sir.
 
Wewe umeongea maoni yako...ila jamaa kafanya kitu safi kabisa...mali inamdrive mwanamke kuvunja ndoa..wakati huo anategemea scuffle kali sana! Sasa ukifanya tofauti unamsuprise...akili ikija kukaa sawa wewe uko mbali mno!
Mkuu tatizo ni kwamba tunasikia ugonvi huu kutoka upande mmoja tu....... Kwa namna yoyote ile jamaa at play a victim card
Usikute yeye ndio tatizo

Ndio maana namshauri ASEME NA MOYO WAKE, mwisho was siku huu ni mustakabali wa maisha yake na mkewe na watoto...... Sio ndugu zake Wala washkaji Wala mahakama
Hakuna anaye ijua hi issue Kwa UKWELI zaidi yake
 
Nimekuelewa chief. Ila not after all what happened. Probably sababu zilizokufanya muachane na kurudiana hazilingani na za kwangu.
Ila i appreciate your concern Sir.
Mkuu Kama maamuzi yametoka chini ya uvugu wa moyo wako naamini utakua umefanya kitu sahihi

Wish you all the best

Kuhusu hukumu ya kesi acha ubahili mkuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mtie hata 20k karani kesho yake ukapewe hukumu yako maisha mengine yaendelee...... Hi ndio Bongo unaweza kujikuta unatumia milioni kufuatilia
 
Ni kawaida kuwa ni mtazamo huu. Ni balanced view. Sema sasa ndio hivyo huwez pata habari ya upande wa pili na mimi pekee ndio nakupa hii habari ndio maana utaona kabisa mimi na wewe hatuwez kubaliana.

Ni kama niseme kuwa wewe kwenye csse yako probably ndio ulikua tatizo may be ndio maana ukaona umeze ego. Sasa hapo nitakua na sound too irrational, kutaka taarifa ya upande wa pili ambayo sina hivyo niishie kuku judge. It doesnt work that how
 
Mkuu niliapa sitoi 100 yangu kupambana na kesi ambazo sikuanzisha mimi. Niliamua kupita through kila alichonifa yia ili niu feel ule uchungu vizuuuri ili nijue kile alichokimaanisha kunipitisha barabara ,ndio maana hata aliponiweka ndani siku hangaika kuhonga kama ambavyo yeye na ndugu zake walivyotumia pesa kuniendesha japo nilikua naiona mianya ua kupigwa pesa.

Hivyo haya ishu ya hukumu walaa, nilijua tu ni pesa inatafutwa, nikawa na push ile kawaida tu maana mpaka wao wenyewe wamenipigia kua hukumu imetoka. Next week Natimba Dar kuifuata.

Nilisha apa, situmii 10 yangu
 
Mkuu, bila kinyongo wala lengo baya, binafsi I'd like to differ...
Hatuezi kuishi kwa kutegemea binadamu. Mfano, wapo wengi tulifanikiwa sababu wazazi wetu walikua hai. Hio haimaanishi walofiwa na wazazi hawakufanikiwa pia. Na je, kuna jambo jema kwa mtoto kupita kuwa na mzazi hususan baba? Huenda likawepo...
Lakini, yupo tabibu wa mioyo, yupo mhukumu wa haki... kikubwa kutenda nafasi yako tu mkuu...
Isitoshe, sisi si bora kuliko watoto walokufa na malaria kabla ya miaka mitano...
Tuishi mkuu, tumeumbwa kula, kunywa, kufurahia kazi, chini ya jua.
Na siri ya nguvu pekee, ni ""wapi tunapoelekeza nguvu zetu za kiakili, kihisia, kimwili, na kiroho""
 
Vipi hamjarudiana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…