Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Hatimae hukumu imetoka tayari, siku ya kwanza tu ya kesi kusikilizwa

Wakuu heshma kwenu.
Habari za jioni.

Nimeona ni vyema kuwa update kuhusu mwenendo wa suala ambalo nilileta hapa jukwaani siku ya jumatatu katika uzi huu ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡


"Samansi" ya mahakama ilielekeza nifike mahamani siku ya leo tarehe 12 Feb 025 nami nikafanya hivyo.
Katika kesi hii mimi kama mdaiwa na aliyekua mke wangu kama mdai.

Niseme tu kitu, katika mfumo wa serikali na personally katika suala hili, nimekuja kugundua, wanawake wame occupy sana nafasi nyingi serikalini, sasa sijui sababu ni nini?
Maana ;
- nilipoitwa dawati, incharge pale alikuwa mwanamke.
  • nilipoitwa baraza, kikao chote kilijawa na wazee wa baraza wanawake
  • leo hii mahakamani, hakimu alikua mwanamke.
Hakika wanawake wametaradadi everywhere, tukiendelea kwa mwendo huu, wanaume twafaaa
๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜.

Anyway,.

Kama ambavyo nilikua nimeamua kuwa natamani hili suala liishe tu, na pia kwa kuzingatia ushauri wa baadhi yenu ndugu zangu wana JF, sikupemda kesi iwe na mambo mengi.

Tulipoitwa chamber na hakimu, alianza kwa kusema "hii kesi leo mmeitwa ili iweze kutajwa tu na kipangiwa siku nyingine, hivyo, mdaiwa utasomewa tu charges zako kisha kama una neno utatamka"

Akasoma,kama ilivyo ainishwa kwenye "samansi" niliopokea ,kuwa mdai anataka
1. Talaka
2. Mgawanyo wa mali
3. Kuishi na watoto
4. Matunzo ya watoto

Akauliza "unasemaje?"

Nikamjibu, "nimesikia na sina pingamizi juu ya lolote katika hayo, na kwasababu sina pingamizi naomba mahakama kama inaweza, hili suala tulimalize hapa hapa na leo leo mheshimiwa hakimu"

Akauliza "umekubaliana na haya yote?"

Nikamjibu "ndiyo, nakubaliana na dai lake la talaka, pia nakubaliana na dai la mgawanyo wa mali, japo nitaomba kujua muongozo wa mahakama unasemaje kuhusu hilo , pia muongozo wa mahakama unasema nini kuhusu matunzo ya watoto na kuishi ma watoto, maana yote niko tayari ku comply"

Akasema "kama ni hivyo, basi hii kesi ni nyepesi na itakwenda vizuri, kuhusu mgawanyo wa mali, mahakama ina suggest 50% 50%, unless kama kama mmoja wenu hajaridhika na mtahitaji tuingie katika ushahidi wa kuthibitisha mchango wa kila mmoja kwa vithibitisho.

Pia matunzo ya watoto yamejikita katika chakula, malazi, afya, na ada. Jukumu hili ni la baba kikawaida, lakini mahakama inaangalia kama mama naye anajiweza, basi jukumu hili wote mtagawana.

Na mwisho kuhusu kuishi na watoto, maadam wako chini ya miaka 18, wataishi na mama, ila baba una ruhusa ya kuwaona . Kama unahama mkoa, maana yake watoto watakuja kwako likizo ambapo, mama atagharamia nauli za kwenda likizo na baba atagharamia nauli za kurudi.

Hivyo basi , ndugu mdai nitakuuliza na utajibu hoja moja baada ya nyingine.

1. Talaka.

Hapa nikawaambia sina pingamizi, niko tayari mke wangu apewe haki yale kama anavyo hitaji. Hapo, wife nikaona kashusha pumzi ndedu nzito. Na muda mwingi alikua anajifuta jasho ingawa ndani pana feni. Katika session yote honestly, sikumtazama usoni. Na hatukusalimiana.

2. Mgawanyo wa mali.

Nikasema, kwakua kesi hii imeshanigharimu suala la muda , nakubaliana na pendekezo la mahakama la fifty fifty, kama mwenzagu, mdai anaona amebanwa naomba apewe uhuru wa kuchagua ratio itayompa comfort. Akasema mimi nataka 60%. Hakimu akauliza, mdaiwa (mimi yani) uko tayari, nikasema SINA PINGAMIZI, mahakama impe hiyo 60% anayotaka.

3. Matunzo ya watoto

Hapa nikasema, always nimekua nalipa ada miaka yote, hivyo hili nitae delea nalo, na pia nitawahudumia gharama ya chakula isiyozidi 150,000/= kwa mwezi kwa kuanzia kwasababu, suala hili limeniathiri biashara zangu pia nahitaji ku settle na kuanza upya maisha, hivyo nikitulia nita adjust.

4. Kuishi na watoto.

Nikasema, nakubaliana na pendekezo la mahakama hapo juu.

Hakimu akasema, aisee, hii kesi imeemda vizuri sana.

Wife akaomba "mheshimiwa naomba kidogo niongee na baba .... pembeni, kuhusu suala la mgawanyo wa mali"

Nikajibu "hakimu, sihitaji kuzungumza private , maana sioni kama kuna suala lolote ambalo kwasasa naweza ongea nae tukaelewana, kama ana jambo lolote aliseme hapa mbele yako"

Wife muda woote alikua anafuta jasho sijui maana yake ni nini, lakini katika vitu naamini, ni kwamba alitegemea confrontation na mimi labda nimuwekee kauzibe na vikwazo vya kukubali ombi la talaka, lakini akaona kila kitu nimekubaliana nae kama alivyotaka. Na kila alipotaka kuibua malalamiko, hakimu akawa anasema, naomba tusiguse sababu za mgogoro wenu kwakua sio sehemu ya madai yako mdai, yote uliyodai, tujikite hapo.

Hakim, akayasoma maandishi aliyoandika kisha akaita kila mtu asaini, nikasaini na yeye akasaini, lakini anaposaini akawa anajilalamisha chini chini, hata sijui anaongea nini.

Basi baada ya hapo tukaambiwa , baada ya siku 45 hati ya talaka itatoka na taratibu za utathmini zitaanza, hivyo tutakiwa kufika.

PIa nikatumia fursa hiyo kueleza kuhusu uharibu wa wa wizi uliotokea nyumbani kuonyesha RB ili ifahamike kuwa mali imeharibiwa na wezi.

Pia , ikafamika pale katika shauri kuwa mimi nilishahama nyumbani, na hii nikaona imem suprise mdai wangu, na sijui sababu ni nini!.

Baada ya yote, hakimu, akasema tumemaliza.
Nikanyanyuka na kutoka, japo niliona yf anaaga huku amekaa ana delay kutoka, like she was exhausted with the proceeding that ended.

Sijajua sasa kama walikua wanayapanga yao mengine au lah!!

Ikaisha hivyo.

Sasa baada ya siku ya 45 days ndio mengine yatafuata.
Kifupi nimefurahi hili suala halijawa extended, ngoma imeitwa leo na imetamatika leo, maana wengi walikua wanasema hii kitu inaweza ikaenda 2 months.

ADDITION:
Wakuu, kesi za kuvunjika ndoa ni nyingi sanaa nimekuatana nazo leo mahakamani. Hali sio nzuri kwenye hii taasisi ya kwanza kuanzishwa duniani

SHUKRANI WAKUU.
Usiku mwema
Hongera sana mkuu umetua mzigo mzito sana Nina Imani utakuwa huru sasa maana tulikuwa tunakaribia kukukosa.
 
Picha lilipoanza ulionyesha ni jamaa Lia Lia + kulalamika .

Demu utombewe, ukute na picha za utupu, alafu wee ndio ulielie.
Ilinipa wakat mgumu sana kukubaki ukweli na uhalisia. Sikua nimetarajia. Ikanipa tabu
Anyway , X Mkeo alijua utazungusha suala la Talaka, Sasa haamini ndo Ivo Kawa mtalikiwa.
Yahp, alifikiri hivyo, na nili notice hilo kwenye session
Mchepuko wake hawez kumuoa sababu keshazaa watoto wengi, Engine imechoka , na sababu kubwa kabisa ya kutomuoa ni kwamba kashuhudia demu anavunja ndoa yake mwenyewe .
Sijui kwann huwa hawafikirii kuwa wanatazamwaje na wanaodhan wanawahitaji. Kama umeweza mfanyia mwanaume mwenzake hiv , ataanzaje kukukuamini kuwa huwez mfanyia na yeye??
Mwisho, Hongera , kuanza Upya Si ujinga.

Muda mfupi ujao, jiandae Ndugu zake na viongozi wa Dini kuanza kukubembeleza.
Shukran mkuu. Ila kuhusu wao kunitafuta sidhani. Wale ni viburi mnoo. Wana ego za hatari. Kilichotufkkisha hapa na wife n ego yake tu, nilikua tayar kumsamehe nkkawa nambembeleza
 
Speechless ... Ngoja nikaangalie mikeka yangu inaendaje!

Asilimia 50 50? Aje tugawane mikeka iliyochanika!

By The way umenifanya nilifikirie swala la ndoa mara mbili mbili
Hatari sana. Kila mmoja ana bahati yake kwenye maisha, ndio maana hata mali wapo wenye nyingi na wapo wenye chache. Kikubwa kumuomba Mungu sana.
 
Sikusoma Uzi wa kwanza ila niseme tu umekutana na vita!
Muktadha wa madaraka uliosema ni matokeo ya woman empowerment hata hivyo Hilo ni tone tu baada ya miaka 50 kutoka Sasa wanaume watakuwa kwenye ujenzi na kuchimba mitaro plus labda u driver
Something must really be done. Ouer young men must really take this a serious note
 
Picha lilipoanza ulionyesha ni jamaa Lia Lia + kulalamika .

Demu utombewe, ukute na picha za utupu, alafu wee ndio ulielie.

Anyway , X Mkeo alijua utazungusha suala la Talaka, Sasa haamini ndo Ivo Kawa mtalikiwa.

Mchepuko wake hawez kumuoa sababu keshazaa watoto wengi, Engine imechoka , na sababu kubwa kabisa ya kutomuoa ni kwamba kashuhudia demu anavunja ndoa yake mwenyewe .

Mwisho, Hongera , kuanza Upya Si ujinga.

Muda mfupi ujao, jiandae Ndugu zake na viongozi wa Dini kuanza kukubembeleza.
Anaetembea na mke wa mtu hawezi kumuoa akiachwa na mumewe.

Kale kamtelezo na ule usumbufu wote wa mwanamke anampelekea mumewe, mchepuko kwako ni burudani na kufurahi tu.

Siku mke akiachwa, yule mchepuko atamkimbia miguu inagusa kisogo.
 
Aiseee kwanini akitaka 60% kwamba yeye amechangia sana kwenye hizo mali?
Hapana, katika uharibu uliofanyika juZ kat pale home, mija ya vitu vimechukulia ni a pile of my diaries, za toka mwaka 2014 (mimi napenda sana kuandika na ku keep records). Hivyo mbali na kutopenda ku prolong hii case, pia yf alijua amefanya nini, ndio maana naamini kabisa ule wiz pale nyumban ni yeye aliwatuma. Nahis alijua kuhsu kupoteza records zangu ikiwemo receipts za manunuzi. Hivyo ingenmgharim nguvu kubwa sana ku justify my contribution kwa ushahidi wa documents
 
Yaani hapo kwa akili ya aliyekuwa mke
Yaani hapo kwa akili ya aliyekuwa mke wako alitamani kuona unagoma kutoa talaka ili psychologically afurahie kuwa anakuumiza na bado unampenda sana kwake huna mwingine. Sasa hapo yeye amejiona hana lolote kwako.
Hongera sana mkuu hivi ndivyo hizi kesi zinatakiwa kuamuliwa siyo mwanaume unateseka na ndoa eti kisa mna watoto au unaogopa kugawana mali.
Ni kweli mkuu. Japo haikua rahis kukubali kuchukua huu uamuzi. Ila nashkuru limetokea hili
 
sina maneno au mawazo mengi kiufupi hoja ni zile zile.

KATAA NDOA LINDA UHURU WAKO
KATAA NDOA LINDA UCHUMI WAKO
KATAA NDOA LINDA MAISHA YAKO
KATAA NDOA MKATABA WA KITAPELI
th (8) (1).jpeg
 
Back
Top Bottom