Hatimae jackline wolper afunguka baada ya kubadili dini kwa mara ya pili na kuwa mkristo tena

Hatimae jackline wolper afunguka baada ya kubadili dini kwa mara ya pili na kuwa mkristo tena

shida za kuhama dini kumfata mwanaume.......

anatafuta justification tu
ruthu: 1:16 Naye Ruthu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu;17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe nami.

infact hayupo kiimani zaidi ni kuwa hakupata sapoti kwenye dini aliyoamia hivyo amerudi kwenye imani aliyokulia mwanzo
 
tatizo wa kiislamu akihama ndugu zake wote watamchukia sana!
Si mumpende ila muendelee kuongea nae kwa upendo hadi aone mwenyewe anastahili kurudi?

huyo naimani harudii tena upuuzi wake wa kubipu dini za watu.atakuwa amekuwa sasa
 
huyo ni wa No Money,No Love,hana jipya.

mwanamke yeyote anayejitambua lazima awe na mwanaume mwenye fyucha. sio tu anatoka na kijana wa bongofleva kavaa mlegezo mara kesho kamfumania. kimsingi jamaa alipoteza direction wakashindwana hivyo wakaachana. thats normal.

hana wakumpa spoti na kumkremisha kaswida tena, inabidi angalie ustaarabu wake. that too is normal.
 
Bahati mbaya tuu haiwezekani kubadili kabila, angeshsbadili kitaambo.

sure. kimsingi inaonyesha dhahir kuwa alibadili dini kwa lengo zaidi la kuolewa lakini baada ya ndoto za ndoa kufutika hakumpata mwenye imani ile tena, amekuwa mpweke baada ya hapo na kwa sasa hana cha kupoteza inabidi arudi kwenye imani yake ya awali.
 
Hatimaye mwanadada Jacqueline Wolper ameamua kuweka wazi kilichotokea
mpaka kuamua kubadili Dini yake ya Uislamu na kurudi kwenye ukristo tena. Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada huyu wa bongo movies ametoa ujumbe ufuatao kwa mashabiki wake.

“…mambo mashabiki zangu.sikua na njia nyingne yakulikwepa hili nanaamini kua kwa wale mashabk zangu waislam amtomaind maana akuna mtu wakumsikiliza chin ya hanga zaidi yawazazi so imenipasa kurudi kanisani kwakauli yawazazi wangu.naamin kama aujaolewa ata uwe na miaka mingap bado unatakiwa kua chin ya imaya ya wazazi ata ukifa ujue unazikwaje na mimi ni binadam sijui saa wala dakika.muhm nikuwajuza nakuwaelewesha mashabk zangu stak maswal nawapenda wote…”

Hapo awali iliripotiwa kuwa mwanadada huyu ameamua kuwa mkristo tena baada ya penzi lake lililosababisha abadili dini na kuwa muislamu na jamaa aitwaye 'Dallas' kuvunjika hivi karibuni.

Swali ni je, atabadili dini tena akitokea mwingine wa dini aliyo tofauti na sasa?

.....amtomaind.....akuna.....aujaolewa... ata....
Duhhhh kumbe mastaa kuandika mbinde ehhh?
 
atahangaika sana mwaka huu, bado kwenda kuwa m-budha tu
 
mkishaharibikiwa ndo mnawasikiliza wazazi!!!
 
hakuna kitu ninaboa kama mtu asokua na H e.g. Imaya = Himaya, ujambo = Hujambo, Ela = Hela, Ujaolewa = Hujaolewa etc etc... au asoweza kutofautisha R na L, tena hii inaboa zaidi unakuta mtu ni wa pwani, kiswahili kilipoanzia lakini ni Lafiki = Rafiki, Rete = Lete, Habali = Habari, inaboa mpaka hata kusoma au kusikiliza inanitia uvivu. Mwingine anaongea vizuri kabisa, sasa kuandika anachanganya herufi.... Mwingine utakuta ni mtangazaji wa TV au Radio, hua nabadilisha station sitaki hata kumsikiliza....
 
Mmmh star wetu wa kibongo...! Vihiyo vihiyo....! Kiswahili tu kuandika taaabu! So bogus ......!
 
loh, dada ame "restore status," ready for the next move.
 
Back
Top Bottom