Hatimae Jombi kamaliza salama shahada uhandisi Mitambo (Mechanical engineering)

Hatimae Jombi kamaliza salama shahada uhandisi Mitambo (Mechanical engineering)

[emoji23][emoji23][emoji23]mbona wa2 wa jf wana jazba kias hik.....yaan ukileta habar nzur wanakasirika ukija kuwaambia umepigwa kibuti utatukanwa mpk ukome

Shida ni nn wanajf au ndo ugreat thinker???

Mkuu sio JF tuu ni social Media zote .
Watu wanapiga spana balaaa ..hahaha.
Changamoto kubwa watu wengi wanasumbuliwa na SONONA .Sasa kwa kuwa humu hatuonani basi makasiriko yako yote wanayamalizia kwako.
 
Wakuu wangu shikamoo zenu.

I'm super excited kwanza.

Mdogo wenu Jombi nimefanikiwa kumaliza Salama degree yangu ya uhandisi. Nakumbuka miaka 4 iliyopita mlinishauri vizuri sana Mdogo wenu kuhusu haya mambo ya shule .

Kwa kuwa na Mimi nimemaliza salama basi nitashare experience yangu ya maisha ya chuo ili ndugu zetu wanaoenda chuo wapate cha kujifunza pia kama ambavyo Mimi nilijifunza kutoka kwenu.

MY LIFE AT THE HILL(UDSM)

1. Coet Life.
Maisha ya Coet yanachangamoto zake kikubwa stress za masomo na wale wazee huwa hawacheki na kima ukikaa vibaya unaliwa kichwa kiutani utani.Mdogo wenu pamoja na kupata vi ONE vyangu huko nyuma nilikotoka(O level na A level) lakini pale mjini coet nilichezea sup za kutosha sana . First year nilipata Supp 1, second year 3(hapa ilibaki kidogo ninikajiongeza bana Watoto wazuri wa chuo year nilipata moja na hii 4th year alhamdullilah nimepita Salama.

2. Biashara na Shule.
Wakuu kama mjuavyo miaka hii ajira zinasumbua so ukiwa chuo lazima na wewe ufanye biashara kidogo ili ukimaliza chuo upate pa kuanzia ila kwa upande wangu mambo yaliniendee kombo biashara zilitaka kunitokea puani mana zilikuwa zinakula mda wangu sana ukijumlisha na madude Yale ya Mechanical basi tabu niliipata .Nikaaamua kuachana na biashara ya kununua na kuuza nikaamua bora nianze kukopesha pesa kwa riba(hapa kidogo nilipata faida ingawa changamoto zilikuwepo pia)

Ushauri wangu: Wewe kijana ambae ndo unaenda chuo kama unania ya kufanya biashara na shule basi hakikisha semester moja unaitumia kusoma mazingira ya shule kwanza na uzito wa masomo unayosoma na ujipime na kichwa yako.Je utaweza kuhimili mikimiki yake.. Ukikurupuka utakosa vyote .

3. Jombi na Mapenzi.

Oya chuo kuna watoto wazuri bana.

Miaka yangu miwili ya kwanza 1st and 2nd year nilitongoza mademu kinoma si unajua Mihemko ya advance(uboyzin ) bado ilikuwa haijaniisha na nilikuwa nakataliwa kinoma hadi nilikuwa najihisi Nina gundu ila baada ya kujua watoto wa chuo wanataka vitu gani basi mambo yakawa mpwito mpwito nikigusa tuu hii hapa.

Daaah nimechoka kuandika mazee.
umeacha punyeto?
 
Uzi upon sharp kwa injinia was miaka 4.Ameandika kitu cha kubaki JF kwa muda mrefu.
Hujasema professional competence yako in maeneo gani, Project ganu ulizifanya na mini matarji yako(vision).
Usipiangalia utaajiliwa na muhindi mshahara 5k, mashine zikikukata mikono unapewa kiinua mgongo cha m1,Ukafie mbele.
 
Uzi upon sharp kwa injinia was miaka 4.Ameandika kitu cha kubaki JF kwa muda mrefu.
Hujasema professional competence yako in maeneo gani, Project ganu ulizifanya na mini matarji yako(vision).
Usipiangalia utaajiliwa na muhindi mshahara 5k, mashine zikikukata mikono unapewa kiinua mgongo cha m1,Ukafie mbele.
Na wewe ndo umeandika nini hapa bwa shekhe .Kajifunze vizuri kuandika kwanza ndo uje kunishauri.
 
Safi karibu Diesel Locomotives Workshop Complex - Morogoro kuna Rehabilitation ya Tyssen Henschel Locomotives kutoka kutumia Hydraulic Transmittion na kutumia Electric Transmittion.
 
Back
Top Bottom