Hatimae mwamuzi Mike Dean anastaafu kuchezesha soka jumapili hii

Hatimae mwamuzi Mike Dean anastaafu kuchezesha soka jumapili hii

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Jumapili hii, msimu wa EPL utakuwa unaenda ukingoni. Bingwa wa EPL atajulikana siku hiyo, vita ya top 4 kati ya Spurs na Arsenal itajulikana siku hiyo lakini pia vita ya kushuka daraja itajulikana siku hiyo kati ya Burnley na Leeds nani ataungana na timu nyingine mbili kushuka daraja.

Msimu wa EPL ukienda ukingoni, Kuna waamuzi nao wanaenda kustaafu baada ya kuchezesha mechibza EPL kwa muda mrefu.

Waamuzi Jon Moss, Mikde Dean na Martin Atkinson wanastaafu rasmi.

Ila kubwa zaidi ni kustaafu kwa mwamuzi Mike Dean ambaye anashikilia rekodi ya kutoa kadi nyingi zaidi katika historia ya EPL.

Mike Dean ameanza kuchezesha mechi za EPL mwaka 2000 na mpaka sasa ameshachezesha miaka 22 ndani ya EPL na huku akiwa na miaka 53. Mike Dean ndio mwamuzi pekee wa EPL kutoa kadi nyekundu zaidi ya 100 .

Msimu huu kashatoa red card 9 mpaka sasa, amekuwa akikosolewa na baadhi ya makocha pamoja na wachambuzi mbalimbali kwa tabia yake ya kugawa kadi kama njugu.

Pia atakumbukwa kwa kupenda kwake kutoa penati hasa zile zenye utata. Ndio mwamuzi anayeongoza kwa kutoa penati nyingi EPL. Kiasi cha kwamba, watu walianza kukariri kuwa ukimuona Mike Dean anachezesha mechi kubwa basi kuna uhakika walau wa penati au red card au vyote viwili kwa pamoja.

Mike Dean atastaafu kuchezesha mechi lakini ataendelea kuwepo upande wa VAR walau kwa msimu mmoja zaidi. Hili jambo baya kwa timu mbalimbali EPL.

Tunakutakia mapumziko mema, sisi wapenzi wa EPL tutakumiss sana kwa ubabe wako lakini bila kusahau kipara chako kama utambulisho wako.

Pichani chini, kutoka kushoto ni Jon Moss, Mike Dean na Martin Atikinson ambao wote wanaenda kustaafu jumapili.

2C0BDA37-0F22-48AB-AA77-59EF114F6AF2.jpeg
 
Kila la heri kwao kwa mchango wao
Wabongo wajifunze kwa wenzao how to manage and deals with law of the game
 
Back
Top Bottom