Hatimae Mwezi huu (Agosti, 2021) nahamia kwangu ili niwe huru kupiga muziki kwa sauti ya juu

Mkuu iyo avatar picha yako ni kama umekalia mpini.
 
Itategemea nyumba yako imejengwa katika mazingira yapi, kama nyumba yako imebanana na majirani zako kiasi cha kinachoongelewa kwako kinasikika kwa jirani yako, basi uhuru huo unaotaka wakupiga muziki full volume, hautafanikiwa bado utapata complain za majirani.
 
Me bado nimepanga ila juzi nimenunua sofa kali nifanyeje ili majirani wajuee[emoji12][emoji12]
Fanya kashughuli hapo hata birthday ya mtoto wa dada yako fanya kama unamapenzi naye sana kuzidi hata Baba yake, alika watoto wa majirani, najua wazazi wao lazima wasogee watajua tu umeingiza sofa.[emoji3]
 
Kuna jamaa yangu alikua anakaa uswahilini nyumba ya udongo ila ina umeme Sasa akanunua mziki mkubwa kinyama akawa akipiga mziki ile mikito ya nguvu had udongo wa juu unadondoka mwenye nyumba alimtimua na radio yake[emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji2][emoji2] duu lazima akufurushe, humo panya lazima wakimbie
 
Samahani kwa watakao me.Suala la starehe ya music ni ya mtu binasi Sasa ukifungua suti ya juu Ina maana hisikilizi weee Bali unalazimisha na wengine wasilikilize kile inachotaka wewe na sio utashi wao na hiyo sisi kwetu HUIITA HALI HIYO USHAMBA
 
Maisha yalivyo , unaweza ukakuta unajipa target nyingine ya juu, ambayo nayo itakukosesha raha , hata huo muziki ulioupania unaweza usiupige sana ,
Hongera sana kwa kuhamia kwako , ila i guarantee you utapata jambo jipya la kufanya nalo litakuweka busy hata mziki hutatamani.
 
Achana nao, wewe ndiye unajijua ulikotoka na ulipo,fanya unachoona kinakupa Amani ya moyo.
 
Msimtabilie magumu, mpeni hongera jamani!
 
Samahani kwa watakao me.Suala la starehe ya music ni ya mtu binasi Sasa ukifungua suti ya juu Ina maana hisikilizi weee Bali unalazimisha na wengine wasilikilize kile inachotaka wewe na sio utashi wao na hiyo sisi kwetu HUIITA HALI HIYO USHAMBA
nashukuru mkuu ila nilishasema nimekulia kijijini na nimekuja mjini nimetimiza malengo yangu ya kumiliki dundo ssa ikiwa ushamba wangu unanipa kitu roho inapenda ushamnba mitano tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu iyo avatar picha yako ni kama umekalia mpini.
ndio mkuu hapo nimekalia mpini kipindi hiko nipo zangu kijijini nilikuwa nakalia mpini nikitoka shamban au nikichoka nakalia jiwe ila siku hizi mjini nakalia kochi yaani naejoy sana yale maumivu ya kukalia mjini ndio basi tena. #ukipanda bangi tegemea kuvuna bangi#

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…