Hatimae nimemkamata anayeninyea mavi mlangoni kwangu

kubwa jinga jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2017
Posts
292
Reaction score
309
salaam wana bodi
bila kupoteza muda nianze na mada moja kwa moja,ni kipindi kama wiki Mbili hivi kila nikiamka asubuhi nakuta mtu amejisaidia (mavi) mlangoni kwangu,na linakokera zaidi huwa anapakaza kwenye kitasa cha mlango,

mwanzo nilifikiri ni walevi lakini nikajaribu kuuliza kwa majirani nikagundua kituko hiki ni mimi tu nafanyiwa,nikaongea na mke wangu,nikamwambia labda ni hivi vitu vidogo ninavyomiliki ndivyo vinavyotuletea karaha zote hizi yaani hii geregi ya kuziba pancha boda boda,baiskeli na kuchaji simu, ndio naletewa mzigo wa mavi ya mtu mzima, wenye harufu kali ,hata sijui huyu mtu kama anakunywa maji jinsi kinyesi chake kinavyonuka duuh pukeeh wacha niteme mate kidogo

Basi nikashauriana na mama watoto, mimi wacha niweke dago matanga ya nyati kwa usiku ili nimpate anaekunya, lakini siku ya kwanza sikumpata,sikukata tamaa usiku wa jana sasa ndio ikawa tamati ya huyo mkorofi anaekunya mlangoni kwangu,

Nilipokua nimejibanza taratibu kunako usiku wa saa tisa si ndio namuona mwanamke wa makamo mkononi ameshika ndoo na jembe,kwanza nilifikiri ni mtu anakwenda shamba lakini nilipokisia muda ,nikajiuliza shamba gani usiku wote huu hata kama kuchota maji lakini hapana,akaendelea kusogea kuja upande wangu mpaka akanipita karibu yangu,nikamuangalia kwa umakini huyu mama duuuh sikuamini yaani ni mama gire jirani yangu basi akaweka vifaa vyake chini alivyobeba

Nikamuona anaangalia kushoto na kulia akaanza kuizunguka nyumba aliporudi akaenda moja kwa moja mlangoni nikasubiri je anataka kugonga mlango au anataka kufanya nini,ghafla bila kuamini nilichokiona nikamuona ameinua nguo zake akabaki kipande cha chini mtupu na akachuchumaa na kuacha mzigo wa haja wa mavi na kuondoka kwa kasi kufuata vile vitu vyake na kuja ule usawa wangu,kama mshare nikamrukia nikamshika mkono na kumuuliza nini alichofanya... kwa kweli alitaharuki na kuomba msamaha nikamwambia lazima twende kwa mtendaji wa kitongoji,akalalamika sana yeye ana watoto wakubwa wa kike na wakiume pale, anaheshimika kama mzee wa kitongoji na mzee wa baraza la kitongoji sasa utakuwa umenivua nguo,

basi nikamwambia nenda kalale mashauri tutayamaliza kwa mtendaji asubuhi,

lakini mpaka muda huu ninapowaletea hii habari bado sijamueleza mtu na maamuzi sijachukua

Jamani wadau nauliza nimfanyaje huyu mama nichukue hatua gani au nimkaushie
 
Umekosea sana mkuu ungetakiwa palepale anapomaliza "KUNYA" na ww ungekunya mbele yake alafu unamfungia kinyesi chako anaondoka nacho akakipake kwake ngoma droo alafu unaingia zako kulala
 
Haya makubwa umejua lengo haswa la yeye kufanya hivyo?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Dah Mbona makubwa haya. Weka Picha kwanza maana kwa isawa uo ulitakiwa umrekodi japo gizani.

Kama yeye hana heshima wewe unampa heshima ya nini.

Vinginevyo ungemtisha kiwa mavi ulikuwa umeyaifazi ulikuwa unatafuta tu jina la mhusika ukamalize shughuri. Hivyo aende tu ku lala. Hapo ungemuua kwa kihoro maana angekaa anasubiri kipapai muda wote. hata unyasi ungemgusa angeshtuka
 
Hahaha hiyo kitu mbaya sana ....Hapo lazima hatorudi tena ...tena saiv nakujua kuwa wew mchawi [emoji23][emoji23][emoji23] ....Nakushauri uachane nae tu ...Ila ka mwambie nimekusamehe ...ili awe huru ....Kusamehe ni kitu ya Msingi sana Ndg samehe 7 Mara 70 kwa siku ...... Kama wewe ni Mkristo sala ya Baba yetu ...ulie mbinguni ..... Utupe Leo Riziki yetu ... UTUSAMEHE MAKOSA YETU KAMA NASI TUNAVYO WASEMEHEE WALIOTUKOSEA .... Hiyo sala itakufunga usiposamehee imeandikwa kasome "Mathayo 6:9-13"


Mungu akutie Nguvu

Fursa2017
 
Haiwezekani umwache hivi hivi lazima mtakuwa mnajuana

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Daah mkuu mara kidogo hivyo na bado wanakuonea wivu.Pole sana mkuu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Alivyomaliza kunya alijitawaza huko chini[emoji23]

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Una huruma unamwachaje kirahisi namna hiyo
 
Mkuu umekosea alvyomaliza kunya tu ungechukuwa maji ungemchambisha nyerolake

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Daah Mama Gire noma sana



Post sent using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…