Hatimae nimemkamata anayeninyea mavi mlangoni kwangu

Hatimae nimemkamata anayeninyea mavi mlangoni kwangu

Watu nao hawana huruma yaani hata kubwa jinga nae wanamfanyia hivi.

Jitu jinga namna hii bado tu unajisaidia mlangoni kwake [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent From Samsung S9 edge using JamiiForum mobile app
 
Haha haha atakua na matatizo ya akili ndio tabu ya kuishi mitaa ya kiswazi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Jamaaa ulitupa mbao na randa

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Kutomfichua kunaweza kukugharimu

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Yani we jamaa mpaka unatia hasira!
Hata kumkata mkono hakuna lol!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
salaam wana bodi
bila kupoteza muda nianze na mada moja kwa moja,ni kipindi kama wiki Mbili hivi kila nikiamka asubuhi nakuta mtu amejisaidia (mavi) mlangoni kwangu,na linakokera zaidi huwa anapakaza kwenye kitasa cha mlango,

mwanzo nilifikiri ni walevi lakini nikajaribu kuuliza kwa majirani nikagundua kituko hiki ni mimi tu nafanyiwa,nikaongea na mke wangu,nikamwambia labda ni hivi vitu vidogo ninavyomiliki ndivyo vinavyotuletea karaha zote hizi yaani hii geregi ya kuziba pancha boda boda,baiskeli na kuchaji simu, ndio naletewa mzigo wa mavi ya mtu mzima, wenye harufu kali ,hata sijui huyu mtu kama anakunywa maji jinsi kinyesi chake kinavyonuka duuh pukeeh wacha niteme mate kidogo

Basi nikashauriana na mama watoto, mimi wacha niweke dago matanga ya nyati kwa usiku ili nimpate anaekunya, lakini siku ya kwanza sikumpata,sikukata tamaa usiku wa jana sasa ndio ikawa tamati ya huyo mkorofi anaekunya mlangoni kwangu,

Nilipokua nimejibanza taratibu kunako usiku wa saa tisa si ndio namuona mwanamke wa makamo mkononi ameshika ndoo na jembe,kwanza nilifikiri ni mtu anakwenda shamba lakini nilipokisia muda ,nikajiuliza shamba gani usiku wote huu hata kama kuchota maji lakini hapana,akaendelea kusogea kuja upande wangu mpaka akanipita karibu yangu,nikamuangalia kwa umakini huyu mama duuuh sikuamini yaani ni mama gire jirani yangu basi akaweka vifaa vyake chini alivyobeba

Nikamuona anaangalia kushoto na kulia akaanza kuizunguka nyumba aliporudi akaenda moja kwa moja mlangoni nikasubiri je anataka kugonga mlango au anataka kufanya nini,ghafla bila kuamini nilichokiona nikamuona ameinua nguo zake akabaki kipande cha chini mtupu na akachuchumaa na kuacha mzigo wa haja wa mavi na kuondoka kwa kasi kufuata vile vitu vyake na kuja ule usawa wangu,kama mshare nikamrukia nikamshika mkono na kumuuliza nini alichofanya... kwa kweli alitaharuki na kuomba msamaha nikamwambia lazima twende kwa mtendaji wa kitongoji,akalalamika sana yeye ana watoto wakubwa wa kike na wakiume pale, anaheshimika kama mzee wa kitongoji na mzee wa baraza la kitongoji sasa utakuwa umenivua nguo,

basi nikamwambia nenda kalale mashauri tutayamaliza kwa mtendaji asubuhi,

lakini mpaka muda huu ninapowaletea hii habari bado sijamueleza mtu na maamuzi sijachukua

Jamani wadau nauliza nimfanyaje huyu mama nichukue hatua gani au nimkaushie
Kuna mti nasikia unaitwa mvuje, siujui ila kama unaujue muekee anapokunya, ataharisha mpaka kucha 😀
 
Samahani mkuu unaish wapi?Mimi naishi wilaya ya masasi mkoan mtwara kijiji cha Namakongwa kiukweli nimestushwa sana na habari hii kwa sababu mimi ni baba wa watoto wa tatu -john ,richard na grace (gire) arafu huu ni msimu wa panya uku kwe2 yani watu weng hupendelea kwenda mashambani kuchimba panya Wa kitoweo akiwemo mke wangu mama gire kiukweli usik wa juz kama kawaida yake aliniaga anaenda kutafuta panya lakn baada ya nusu saa niliskia akigonga mlango kwa taharuk baada ya kumfungulia mlango aliingia ndani hakutaka kuzungumza chochote nami sikumfosi sana ila cha kunshangaza asubuh ameniambia kwamb yeye anataka kwenda kumsalimia mama yake songea mim npo kazn sasa sijui nyumbn ameondoka au la! niambie waish wap tafadhar !
 
Kosa kumuachia,ushapoteza ushaidi,,Sasa hapo anaweza kukuua ili usimtangaze maana anaishi kwa wasiwasi haujui unachotaka kufanya ni nn?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Samahani mkuu unaish wapi?Mimi naishi wilaya ya masasi mkoan mtwara kijiji cha Namakongwa kiukweli nimestushwa sana na habari hii kwa sababu mimi ni baba wa watoto wa tatu -john ,richard na grace (gire) arafu huu ni msimu wa panya uku kwe2 yani watu weng hupendelea kwenda mashambani kuchimba panya Wa kitoweo akiwemo mke wangu mama gire kiukweli usik wa juz kama kawaida yake aliniaga anaenda kutafuta panya lakn baada ya nusu saa niliskia akigonga mlango kwa taharuk baada ya kumfungulia mlango aliingia ndani hakutaka kuzungumza chochote nami sikumfosi sana ila cha kunshangaza asubuh ameniambia kwamb yeye anataka kwenda kumsalimia mama yake songea mim npo kazn sasa sijui nyumbn ameondoka au la! niambie waish wap tafadhar !

Au sio
 
Back
Top Bottom