Chief Kumbyambya
JF-Expert Member
- Jun 16, 2022
- 719
- 2,408
Wasalaam.... Nawasalimu kwa jina la upendo wa dhati....
Kwanza wataalam wa mambo ya genetics naomba mnisaidie kuhusu hili jambo.
Sijui ni kwa nini hawa madogo waliozaliwa kuanzia miaka ya 2000 wanakuwa haraka mno na wana vimo vikubwa kuliko sisi kaka zao.
Na jambo hili ndilo linawafanya wajenge dharau hasa kwa sisi kaka zao wa 1900s kwa sababu wengi wetu tuna vimo vya maandamano "Vimo vya utendaji kata na ubalozi wa nyumba kumi".
Juzi tulikuwa tunamalizia matanga ya msiba wa mjimba wetu pendwa sana na kila mmoja wetu huu msiba ulimgusa kwa ukaribu mno kiasi kwamba mpaka wafiwa tukawa tunazunguka huku na kule katika harakat za kugawa vyakula msibani ili wageni waliokuja kuhani msiba wasiondoke kinyoge "yaani wasiondoke kabla ya kula"
Huyu dogo tumefuatana ingawa ni kwa zaidi ya miaka mitano. Sasa Jana jioni mida ya saa 12 hivi jioni wakati sisi kaka zake tunazunguka huku na huko kugawa vyakula Kwa wageni huku kina dada na kina mama wamekazana kulia kwa uchungu huko ndani.
Na kama mnavyojua wanawake wa kinyakyusa wanajua sana kulia misibani......Tena wanalia kwa kufuata zile ala za muziki "yaani kama kwaya vile kumbe watu wanalia humo ndani"
Kumbe dogo wakati huo yeye ameketi tu na machekibobu wenzie wamekoka moto wa kuni wanota pale na stori kibao za chuoni "Tukuyu ni baridi sana kipindi hiki"
Nikamkata jicho nikaendelea kusambaza msosi kwenye bonge moja la sinia huku likiwa na sahani kama 14 hivi za msosi pamoja na mabroo wengine, zilipoisha ile narudi kuchukua lisinia lingine nikamuita.... Dogo vipi mbona kaka zako tunagawa msosi huku wewe unaota tu moto na wenzio hapo, au huu msiba haukuhusu?
Dogo si akanijibu kunyaa........ Wenzie wakamshauri nenda bana ukimaliza njoo tuote moto fresh.. dogo akasema.. Aargh.. broo anazingua tu huyu. Nikamwambia dogo unasemaje....?
Huku anasimama anaelekea migombani nikamvuta mkono akageuka eti Kwa hasira apigane na mimi hahahahaha..
Nikaweka sinia chini anazid kunifata nilifurumusha bonge moja la konde kwa mtindo wa Peek A Boo style ile aliyokuwa akiitumia Mike Tyson "Maana ile style ni dozi Tisha sana dhidi ya majitu marefukama yeye?
Wajomba wadogo na wageni wengine ikabidi waingilie kati huku dogo akitema damu nyingi mdomoni baadae nikaja kugundua meno magego mawili ya upande wa kushoto yameng'oka yote.
Hapa nasubirua kikao cha bodi ya familia, wajomba pamoja na wanandugu wengine kuhusu hili swala la sisi kupigana msibani. Hili kosa ni la dogo sio langu.. kwa nini alikuwa hasambazi vyakula kama sisi kaka zake "Yani ankaa kibosi msibani?"
Kikao kinaanza saa kumi jioni hii na nimeshaandaa nondo zangu kali za kukabiliana na haya mashtaka dhidi ya bodi ya familia.
Eti wazee kuna kosa lolote nimefanya hapo?
Hawa madogo wanazingua kinoma mpaka inafika hatua mtu unajisahau kuwa uko msibani......
R.I.P mjomba............