Hatimaye Anti Ezekiel afunga ndoa

huyo mume amekosa kaz ya kufanya.
 
Huyo jamaaa aliyemuoa kaliwa pedeshee john Mangi hapo huwa anajigongea any time
 
Nahisi jamaa aliyemuoa ni baada ya kuona ile Kufuli pale jukwaani akavutiwa naye!
 
kama ni kweli (if not photoshop) namtakia maisha mema katika changamoto za maisha. Welcome to the adult world aunt ezekiel.

naona kavaa ki-islam kumbe amebadili dini???? Haya dada maisha mema ila usichome makanisa yetu tafadhali kama wenyeji wako.
 
inaweza kuwa kweli au igizo
ikumbukwe ndoa zetu zinafungwa bibi harusi akiwa chumba tofauti na bwana harusi
kweli huyu binti ana matukio mabaya lakini ikumbukwe kumhukumu si sawa kwani anawezapata anayependa vibweka vyake!!
Waswahili wanasema - Kila shetani na mbuyu wake
 
ndoa inafungwa kitandani duu! ni dini gani hiyo wakuu

labda kaolewa na muislam sababu nasikia waislam anayetakiwa kuwa msikitini ni muoaji na baba wa bint..

au labda wameamua tu kuifanya kimya kimya chumbani ..

au labda....

hongera anti
 
Hilo litakua ni filamu anaigiza mbona mume haonekani wala hakuna watu wanaomzunguuka hata huyo shehe anaeozesha hayopo inakuaje?
 
Ndoa ni muunganiko wa watu wawili na wenye jinsia tofauti, hapo naona muunganiko wa watu watatu wote wana wake!

Mtoa mada umeondika ndoa lakini hapo hakuna ushahidi wa ndoa! Mume haonekani kwa nini?

Hiyo lazima ni film
 
ule msanii wa filamu ambaye alitikisa sana kwenye anga za tamasha la SERENGETI FIESTA 2012, kwenye mikoa mbalimbali kwa kufanya show ya nguvu akiwa na mwingizaji mwenzake Wema Sepetu, Aunt Ezekiel jana saa mbili usiku amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu ambaye alilitinga jiji kwa kutanga zake kutaka mrembo huyo Mr Demonte. Hebu somazaidi
 
Kaolewa na jike jenzake? maana muoaji(mwanaume) simuoni kabisa pichani................!
Aliyeoa kaoa kichefuchefu..............................!
 

Asante mama D kunisaidia kujibu hili kwa ufasaha
 
Last edited by a moderator:
ndoa gani isiyo na mume?mleta maana twaomba utuletee picha za pamoja na muoaji,wakati wa shughuli,ilifanyika wapi na hao mashoga zake ni kina nani.
Mgaya D.W

Nakujibu wewe kwa niaba ya wenzio wooote mliouliza kuhusu muoaji.

Mumewe ajaitwa Sunday Demonte. Usibabaishwwe na jina, ni Muislamu na anaishi Dubai. Wakati ndo ikifanyika, mume yuko Dubai na hapa kawakilishwa na nduguze ambao wameoa kwa niaba yake. Waislamu wanaruhusiwa hata ndugu kuoa kwa niaba ya mume kwahiyo sio issue sana kwao.

Hata kama mume angekuwapo Dar kwa sasa na kuwapo eneo la tukio, Bibi harusi na Bwana harusi huwa wanakaa sehemu tofauti na hawakai pamoja siku ya kufunga ndoa. Kila mmoja anaulizwa akiwa sehemu ya peke yake.

Sio lazima shigongo atoe kwanza ndio muamini, hata humu JF kunaweza kuwa sehemu ya kwanza ku-break news. By the way, sherehe maalum ya mke na mume itafanyika Dubai hivi karibuni. Nitakuleeteeni Picha.

Stay Tuned
 
Last edited by a moderator:
Bado Utetezi wako haujibu utata uliopo hapo. Hicho kitu Ni cha kisaniii kabisa.

*Cheti cha ndoa lazima kisainiwe na wahusika wote wawili yaani mke na mume mwenyewe na sio kwa niaba.
Picha inamwonyesha mwanamke pekee.

*Kwenye uislam hakuna kitu kinachoitwa kuoa kwa niaba ya mtu mwingine. Zipo mila za makabila fulani ndio zina hicho kitu lakini sio kwenye uislam wala kiserikali.

*Yote kwa yote, mbona upande wa waoaji hatuuoni hapo, yaani huo ''uwakilishi wa
mwanaume'' kama ulivyodai? Yaani hata upande wa mwanamke(Mzazi wa kiume) na Sheikh(Ustaadh) anayefungisha ndoa hawapo hapo!!
 
Last edited by a moderator:

Mkuu,

Hebu tafuta muislamu hapo anayejua taratibu za kiislamu katika kuoa atakupa taarifa I wish ningekujua nikueleze kwa mdomo labda ungenielewa UNLESS kama unatoka Kigoma mwiso wa reli.

Mwislamu anaweza kumtuma rafiki yake akaoe kwa niaba yake na ndoa hiyo ikawa halali kabisaaaaa. Nakushangaa hilo unalopinga wewe.

Ni tofauti sana na ndoa zetu tulizozoea kwa wachungaji, mapadiri ama serikalini. Wenzetu hawa waislamu wako tofauti sana katika kuoa.

Aftarall unajua kama mahari kwa muislamu anapewa Mke na sio wazazi?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…