Ta Kamugisha
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 3,541
- 2,187
Hutaki tu kuutambua ujinga wako!
Bora yako wewe unayetambua ujinga wako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hutaki tu kuutambua ujinga wako!
Hoja dhaifu huletwa na watu dhaifu!! Tunataka sababu za kiuchumi katika ujenzi was uwanja was chato sio utuletee ngonjera za kwene kanga hapa!
Just imagine ingekuwa ndo Lowassa Rais (angalizo ni mfano tu sina mapenz naye kiasi hicho)alafu akajenga Monduli international Airport badala ya kuendeleza Arusha Airport ungeyaongea haya? Ingepaswa kuuliza monduli sio Tanzania? Ingepaswa kuulizwa kwani wamasai ni nyani?
Just imagine...
***Nimesoma mada kwa marefu na mapana yake,bahati mbaya wapo baadhi ya wachangiaji wana viwango vidogo sana vya uchangiaji.Hatuna namna ya kuwaondoa labda mods wangeweza kusaidia.
Mfano mleta mada kaeleza vizuri kwanini ujenzi wa uwanja CHATO ni kukosa mwelekeo,anakuja mtu utadhani kalazimishwa kuchangia "Eti kwani Chato ipo Sudani" mwingine mbona KIA ilipojengwa Bomang'ombe kulikuwa na nini.Unabaki kushangaa na kujiuliza maswali kibao ni jinsi gani shule,college... vimezalisha watu wa hovyo kwa kiwango hiki.Watu hawapendi kushughulisha bongo zao wanasema hovyo hovyo.
Nirejee kwenye mada.
Mosi,Ujenzi wa uwanja wa CHATO ulikuwepo katika mipango tangu mwanzo au uliibuka baada ya Dr Magufuli kuchaguliwa ?.Katika ilani ya CCM ujenzi wa viwanja vya ndege kiwanja cha ndege cha Chato kipo ?.
Pili,Ujenzi wa uwanja wa ndege unaambatana na sababu za kiuchumi,kijamii,kiusalama na nk.Kabla ujenzi haujaanza mambo yote yalingatiwa au tuliamua kwakuwa Rais anatoka eneo hilo,ikiwa ni hivyo maana yake tutakuwa tunafanya maamuzi kwa kuangalia maeneo wanakotoka viongozi na si kuangalia sababu za kiuchumi ?.
Tatu,Suala la kujenga miundombinu based on wanakotoka viongozi si jambo geni Afrika.Ukisoma historia ya kijiji cha Yamoussoukro alichozaliwa kiongozi wa mwanzo wa taifa la Ivory Coast Mh Felix Houphouet Boigny ambacho baadae kiligeuzwa makao makuu ya serekali badala ya Abdjan.Mh Felix Houphouet Boigny alianza na ujenzi wa kanisa kubwa dunia Basillica of our Lady of peace,ujenzi wa uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutua ndege aina ya Concord (Afrika wakati huo vilikuwa viwili tu Gbadolite na Yamoussoukro Airport) na majengo ya kisasa kwaajili ya shughuli za kiserekali.Ukienda kule Zaire sasa Congo aliyekuwa Rais wake Marehemu Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga hakuishiwa vituko alijenga uwanja wa ndege mkubwa kuliko wowote Afrika wakati huo Gbadolite International Airport,Jumba la starehe na miundombinu ya kisasa kijiji alichozaliwa leo ni mahame kabisa hakuna kinachoendelea kwakuwa wakati wa ujenzi hawakuzingatia masuala ya uchumi,jamii,usalama na nk.
![]()
![]()
Control tower ilivyosasa.
![]()
![]()
![]()
Baadhi ya majengo yamegeuzwa madarasa.
![]()
Hotel ya kifahari leo haina wageni hata kiduchu.
![]()
Hata Mbuzi hawapatiki.
![]()
Bwawa la kuogelea lilivyo sasa.
![]()
![]()
Ulevi wa madaraka ulivyoteketeza mabilioni ya fedha za walipa kodi katika uwekezaji wa kijinga.
Lizaboni anaweza?Naanza kuwaelewa wanaotaka JF isiwepo. Humu kuna watu wana information hatari. Binti Forogo au bintishomvi hawezi kuelezea kwa weledi hivi.
Mawazo mabaya sana haya!Kwa jinsi wachaga walivyo wezi na wabinafsi hawatakaa watoe rais.
KabisaaaKwa jinsi wachaga walivyo wezi na wabinafsi hawatakaa watoe rais.
Wadanganye wajinga Mimi nimekuwa nikienda Chato mara nyingi toka katikati ya miaka ya tisini hadi mwaka huu nimefika tena. Ngoja nikupe details kidogo halafu nipinge,, zamani tulikuwa tunafikia Guest ya DINGI pale Makufuli, baadaye tukahamia Marine A lodge, chafu chafu hivi, au Ludomya Lodge then ikaja Marine B ambayo at least unaweza kuilinganisha na baadhi ya lodge pale Buselesele, ingawa nayo huwezi kuilinganisha na lodge za Muleba au Biharamulo na hata Ushirombo. Mji wa Masumbwe pale Mbogwe unakuwa kwa haraka kuliko ChatoChato ni Mji unao kua sana ndio maana umejengwa uwanja wa maana, pia Migodi ya Geita watumishi wake watatumia huu uwanja, Ya kaisali mpe kaisali na ya Mungu mpe mungu
Nawashangaa sana wabongo, what economic potentials are you referring and leave away Rubondo game reserve.Mwaka Jana mheshimiwa Raila odinga alitumia sikukuu ya mwaka mpya kwenda kupumzika kama mtalii yeye na familia yake.Lakini jiulize alifikaje huko? Alitumia Helicopita ya kukodi ambayo gharama zake kurudi Tena mana ziko juu. Kibiashara feedback tunapata kutoka kwa customers wetu.Hatuwezi jua feedbacks za wateja zinasemaje.Lakini tu nadhani kuna with kutoka kwa wateja wa high rank like Raila wameshauri uboreshaji. Tumezoea kusikia traditional mbunga za wanyama Kama serengeti, ngorongoro, Lakini Rubondo Nani anajua? Ambako tunaambiwa kuna ndege adimu duniani wako kule huwezi kuwapata popote duniani.Acha cha to internaltional airport ijengwe bana tukaone ndege adimu duniani. Raila kaanza wengine tufuate
Mkuu umeongea point nzuri na yenye manufaa kwa taifa iwapo ikifanyiwa kaziMkuu barafu. Nikushukuru kwa kuanzisha mada.
Hilo la uwanja kujengwa chato binafsi sioni kwanini usijengwe huko. Labda kama ungeonyesha ni kwanini chato panastahili uwanja mdogo kuliko unaojengwa kuliko sababu ulizotoa.
Hoja yangu inahusu kuboresha uwanja wa Mwanza kuhudumia mbuga ya Serengeti.
Ki mantiki. Sehemu kubwa ya mbuga ya serengeti ipo mkoani mara na si zaidi ya kilometa 110 kwa barabara kutoka makao makuu ya mkoa hadi kuingia mbugani kwa kupitia barabara ya Musoma - Arusha na haifiki kilometa 70 kwa kupitia barabara ya Musoma - Mwanza. Mbuga hii ipo kwenye wilaya za Serengeti Tarime na Bunda. Ambapo Wilaya ya Serengeti inamiliki eneo kubwa zaidi.
Sehemu ndogoya mbuga hii iliyobaki ipo mkoani SIMIYU katika wilaya za Itilima na Bariadi. Mkoa wa mwanza ulikoma kumiliki mbuga hii baada ya kuanzishwa mkoa wa simiyu.
Mipango ya kujenga kiwanja cha ndege kuhudumia mbuga ya serengeti ni ya muda mrefu ambapo awali ilikuwa uwanja mkubwa wa kisasa ujengwe Musoma au Bunda ili kuhudumia mbuga hii. Na uwanja mdogo wa Mugumu uboreshwe. Eneo la uwanja lilibainishwa na juzi kati enzi za Utawala wa Kikwete lilipimwa upya. Mpango huu uliambatana na kuboresha air strip ya mugumu iwe na viwango vya sasa vya uwanja kama wa Arusha na pia kujenga barabara kutoka Musoma hadi Arusha.
Utekelezaji wake unapigwa figisu hadi leo ambapo hakuna kiwanja. Air strip wala barabara iliyojengwa. Sababu mojawapo ni hoja zilizotolewa na wana kaskazini kwamba bora kuijenga KIA ili ihudumie mbuga zote zilizoko kaskazini mwa nchi.
Uwanja wa KIA UKAJENGWA. Na tagu wakati huo mbuga ya serengeti ikajulikana kwamba ipo arusha kama ambavyo tunaambiwa mlima kilimanjaro upo nchini Kenya. Mkoa wa mara ukakosa mapato ya utalii kwa maana ya viingilio vya wageni mbugani na uwekezaji wa miundombinu kama taasisi za utalii mfano hoteli, vyuo majengi ya taasisi za umma nk. na miundombinu hii kwa wingi imeendelea kujengwa Arusha tangu wakati huo,na kuhalalisha mkoa wa arusha kumiliki mbuga ya Serengeti.
Awamu ya pili ya kujenga uwanja mkoani mara ni huo uwanja wa Serengeti ulioutaja kwenye andiko lako.
Hii ilikuwa zaidi inachochewa na maombi kutika kwa mwekezaji aliyewekeza pale Gurumeti.
Kama ulivyogusia. Uwanja huu pia haukujengwa kutokana na figisu za wanaharakati wa ndani na nje ya nchi. Ambapo jamaa zetu wa kaskazini waliungana na Wakanya kukwamisha ujenzi.
Hivyo badala ya kupugia debe uwanja wa Mwanza kuhudumia serengeti ungesema ukweli kwamba uwanja wa kuihudumia mbuga hii ujengwe ndani au karibu na mbuga hii. Nani ya mkoa wa mara au wa sumiyu.
Lengo hapa ni kuonyesha uhalisia. Sote tunakubali uwanja wa ndege wa mwanza unahitajika na ulitakiwa uwepo kabla ya ule wa KIA.
Suala la kuhudumia mbuga ya serengeti ama kutokea KIA au uwanja wa ndege wa Mwanza hakuta tofauti kubwa maana bado usafiri wa magari wenye kuchukua muda mrefu njiani utatumika.
Tuseme tu kwamba lazima kuwe na uwanja wa ndege wa kisasa unaokidhi mahitaji ya sasa na baadae NDANI YA MKOA WA MARA au MKOA WA SIMIYU ili kuihudumia hii mbuga.
Wenzetu wa-kenya wanajenga viwanja vya ndege vikubwa vilivyi katika umbali usiokuwa mkubwa ilimradi kuna sababu. Mfano angalia umbali wa viwanja vya Nairobi Kia na Taveta. Pia Nairobi Nakuuru Masai Mara na Kisumu. Au hapa Tanzania kuna Kia Arusha na Moshi.
Basi ni halali kujenga na kuboresha viwanja vya Mwanza Kigoma Simiyu Tabora Singida Shinyanga Chato Bukoba na MUSOMA kwa ukubwa tofauti kulingana na vigezo vya kiuchumi kijamii na kijiografia.
Msisitizo ni kwamba mbuga ya serengeti italeta faida kwa taifa hili kama serikali watanzania wote na wakazi wa mikoa ya Mara na Simiyu wataona umuhimu wa kuwekeza kwenye miundombinu ya kuihudumia mbuga hiyo. Kama maji barabara hoteli uwanja wa ndege nk. ndani ya mikoa husika.
Umeona hapo ametajwa Nyerere? We wa wapi wewe?Tulia dawa ikuingie wewe!!! Any way kanani kanani makali yasitutoe kwenye hoja!!
Heshima kwako ndugu yangu hata kwa kuchukua muda wako kuchangia mada na kutoa changamoto....binafsi najushukuru nyerere hana hatia hapa naomba atendewe haki
Wadanganye wajinga Mimi nimekuwa nikienda Chato mara nyingi toka katikati ya miaka ya tisini hadi mwaka huu nimefika tena. Ngoja nikupe details kidogo halafu nipinge,, zamani tulikuwa tunafikia Guest ya DINGI pale Makufuli, baadaye tukahamia Marine A lodge, chafu chafu hivi, au Ludomya Lodge then ikaja Marine B ambayo at least unaweza kuilinganisha na baadhi ya lodge pale Buselesele, ingawa nayo huwezi kuilinganisha na lodge za Muleba au Biharamulo na hata Ushirombo. Mji wa Masumbwe pale Mbogwe unakuwa kwa haraka kuliko Chato
Pale juu ghorofani alijengewe mkuu wa Wilaya kuishi kaogopa kukaa na nyani ikabadilika gia kuwa ofisi ya Takukuru, Nyumba za NHC hazina wapangaji ila pale kwa Mheshimiwa kwa nyuma kuna apartment za bei poa watu wamezikimbilia. Kwa kifupi Chato kwa sisi tuliotembea Tanzania nzima tunaojua kuwa mji wa Makambako umejengeka sawa Geita mjini tunaona kabisa Chato ilistahili uwanja wa ndege kwa ajili ya raisi ila ule wa kiwango kama wa Bukoba kwa ajili ya raisi na wageni wake na hata commercial flight ya abiria 50 ambayo labda inaweza kuwa na safari moja kwa wiki au kwa mwezi. Lakini haujazi abiria 150 kwenye ndege kwenda Chato, never ever
Any way nyenyere ni weye unayejitia kujua kila kitu!!!! Ubungo uko ila ufahamu ndio ziro kwa sababu mpaka anajenga pale hujui kuna mipanho gani mpe muda amalize...na hamwezi jua uwanja unao jengwa uko na ukubwa gani maana hamna taarifa rasimi...Umeona hapo ametajwa Nyerere? We wa wapi wewe?
Mheshimiwa wakati wanaopiga kelele kwenye mitandao watakaponyamaza jenga barabara ya mabasi yaendayo kasi kati ya Chato na Geita.
Achana nao, hivi wanadhani wewe ni Nyerere aliyekataa asiwekewe barabara ya lami iendayo nyumbani kwake lakini ikawekwa wakati amefariki?
Baelezeee maana wao wanataja majiji yajengwe kwao kwa wengine ndo wanataka sijui principle za uchumi zifuatwe...stupid.Kumbe unakujaga kutembea! Mimi naishi hapa hapa mkubwa, hayo ni mambo ya forecasting. Na utaumia sana tu soon as posible unakuwa Mkoa wa Lubondo, mwaka huu mtaonge sana