MHADHARA MAALUM WA UMMA (PUBLIC LECTURE)
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kupitia College of Business and Economics (CoBE), kwa kushirikiana na Public Private Partnership Centre (PPP Centre), kinakukaribisha kwenye Mhadhara Maalum wa Umma utakaowasilishwa na Mhe. David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji, Public Private Partnership Centre (PPP Centre) – Wizara ya Fedha
MADA KUU.
“Kubadili Miundombinu na Utoaji wa Huduma za Umma Tanzania: Nafasi ya Kimkakati ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika Kufanikisha Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Ni Tarehe: 03 Juni, 2026 Muda: Saa 4:00 Asubuhi – Saa 8:00 Mchana Ukumbi: CBSL_CT 1, CoBE – UDOM
Kwa nini usikose?
✅ Ufafanuzi wa kina kuhusu Dira ya Taifa 2050
✅ Nafasi ya PPP katika maendeleo ya miundombinu na huduma za umma
✅ Fursa za uwekezaji na ushiriki wa sekta binafsi
✅ Majadiliano ya moja kwa moja na wataalamu wa sera na maendeleo
Wanafunzi, wahadhiri, watafiti, viongozi wa umma, sekta binafsi na wananchi wote mnakaribishwa kushiriki.
Jifunze. Jadili. Changia Maendeleo ya Tanzania kuelekea Dira 2050. 🇹🇿