Hatimaye dvc-academic/finance wang'olewa rasmi chuo kikuu cha nelson mandela-arusha

Hatimaye dvc-academic/finance wang'olewa rasmi chuo kikuu cha nelson mandela-arusha

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Posts
4,582
Reaction score
2,783
Wanajukwaa,

Katika mambo yaliyoteka jamii ya wasomi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia katika siku za karibuni ni ubadhirifu mkubwa na uongozi mbaya. Malalamiko ya wafanyakazi na wanafunzi yalikuwa yanaelekezwa kwa DVC-Academic na DVC- Finance, Prof. Shemweta na A. Dubi kwa pamoja.

Habari za uhakika kutoka ndini ya chuo hiki zinasema, HATIMAYE HAWA JAMAA WAMENG'OLEWA RASMI. Pia taarifa zinaonyesha kuteuliwa kwa Maprof. wawili kutoka SUA na kuchukuwa nafasi zao na wataanza kazi hapo jumatatu ijayo.

Taarifa hizi zilianza kuzagaa baada ya wanafunzi kugoma kwa sababu ya viongozi hawa kufisidi hela zao za tafiti. Mgomo huu ulisababisha ziara ya ghafla ya Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Prof. Mbalawa na ambayo ilileta sintojua nyingi. Inasemekana, aliita mkutano na wakuu wa Idara mbalimbali na kuzungukia chuo pamoja na hostel ambapo inasemekana alikuwa anaingia hata kwenye vumba vya wanafunzi.

Juzi na jana, imetaarifiwa kuwepo kwa kubadirisha mikataba mbalimbali ndani ya chuo hicho hasa ya Ulinzi na Usafi wa mazingira.


Nini cha kujiuliza:

kwanini kuwepo na mabadiliko katika mikataba hii wakati wahusika wa mikataba hii wanaondoka?
 
Naona nguvu ya wanafunzi imesaidia. Uongozi wa hicho chuo ulishawahi lalamikiwa humu JF. Huyo DVC-Academic nafikiri aliwahi shika post hiyo hiyo Open University of Tanzania (OUT).
 
Chanzo ni jamaa waliopo ndani ya chuo hicho, wanafunzi na wafanyakazi.
 
Back
Top Bottom