Ponjoro wa Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2024
- 3,771
- 10,311
Mchezaji tishio wa club ya Simba Elie Mpanzu ameiandikia club hiyo kuomba kuachana nayo baada ya kupata timu nyingine.
Ameikumbusha club hiyo makubaliano ilikuwa ni kusajiliwa kwa mwaka 1 kwa milioni 330 na ikitokea offer kubwa kwenye timu nyingine basi mchezaji atailipa Simba milioni 330 hata kama mkataba wake uko ukingoni.
Viongozi wa Simba walipotaka kujua timu anayokwenda mchezaji alijibu (na kuambatanisha mkataba) kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote ya mchezaji kutaja timu anayoelekea na kwamba ataondoka kama mchezaji huru baada ya kurejesha fedha hiyo.
Ameongeza kuwa endapo Simba itaona vema yuko tayari kubaki kwa dau la milioni 986 na si vinginevyo na kwamba fedha hiyo ni lazima ilipwe kwa mkupuo na mshahara usiopungua milioni 31.3 kila mwezi.
Viongozi wameahidi kumpa jibu kabla ya ijumaa.