Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Mpira una njia na taratibu zake, hakuna maajabu yanayoweza kutokea tena baada ya uongozi wa Yanga kurudia kosa kwa mara ya pili mfululizo. Timu ilifanyiwa mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kuja Ramovic, timu ili struggle kwa mechi kadhaa ila ikaja kutulia baadae, bahati nzuri mechi za klabu bingwa ndizo zilizotangulia kuliko ligi kuu hivyo ligi kuu ilichezwa wakati Yanga ikiwa imeanza kurejea kwenye kiwango chake.
Timu ilishakaa sawa na tuliona Yanga ikiwa inapata ushindi mnono wa magoli 3+ mnakuja kuleta kocha mpya nae aanze na upya kabisa kuweka falsafa zake huku timu ikikabiliwa na mechi back to back za ligi kuu.
Kuna shida kubwa sana katika mambo ya kimkataba kwa huu uongozi wa Yanga, kocha anaondoka kirahisi tu kisa kapata timu nyingine yenye maslahi zaidi yaani ni ovyo sana katika mambo ya sheria za kimkataba na ndio maana kesi zote uongozi unashindwa hovyo hovyo.
Kwa hapa Simba apewe tu kombe la NBC Hersi hayuko serious kabisa na njia za mpira kwa msimu huu.