Hatimaye Erick Shigongo Atajiunga na chuo mwaka huu

Huyu jamaa ni kichwa cha hatari.kumbe hajawahi kukusanya course work.hivi angekuwa hata na diploama ingekuwaje.nadhani akimaliza wambakize afundishe Entrepreneurshi a.k.a somo la ujasiria mali.atawakomboa wengi.kwa sababu mimo namuona tayari anastahil Phd
 
Amesoma vitu tofauti na vinavyofundishwa mashuleni ndiyo maana hana vyeti
 
Amefuzu kusoma namba kwanza pale lumumba, sasa anataka kwenda chuo kabisa
 

Dunia ujanja kupata sio kuwai,...
 
Bill gate mwenyewe aliacha chuo akaenda kupiga dili zake mambo yalivyomnyookea akarudi tena chuo! Vyeti ni heshima tu lakini sio chanzo cha kukufanya ufanikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
asilimia 100 ya wanaomdhihaki erick shigogo kwenye uzi huu,ni "mapumbafu na malofa" in mkapa's voice.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mbele kwa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Elimu haina mwisho utashi wa kujiendeleza ili kupata maarifa zaidi ni hitaji la muhimu kwa ustawi binafsi wa mtu. na ikumbukwe lipo kinafsi zaidi na hujengwa na msukumo wa mtu husika kufuta ujinga. Sioni sababu ya kumshupalia Shigongo bali ni vema kumpongeza kwa kupambana na hali yake! Elimu hujenga ila kukuza maarifa ni haja yako binafsi wadau.
 
Apewe hongera sana na pia atumike kuhamsisha v9ijana siyo tu katika ujasiliamali, bali pia katika elimu formal. Nakumbuka mwalimu wangu mmoja aliyenifundisha darasa la nne mwaka 1972 akiwa na cheti cha grade C alipata Ph.D mwaka juzi baada ya kujiendeleza kukamua Dip.Ed(Chang'ombe), B.A (OUT), MA(Scotland) baadaye hiyo Ph.D pia huko huko nje ya nchi. Elimu haina mwisho!
 
Mkuu mbona jamaa ana nyota ya kufeli,ccm alifeli,la saba alifeli akarudia akafeli,mahotel yamefeli,mtihani wa kujiunga chuo amefeli sasa huko anakoenda si ndo atafeli zaidi na kujikamua uhai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…