Msumbiji : Kumtenga Mondlane katika mazungumzo ya baada ya uchaguzi itakuwa "kosa kubwa"
10 Januari 2025
Picha: DW
- Rais Nyusi jana alikutana na vyama vilivyopata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa kitaifa, lakini Venâncio Mondlane kwa mara nyingine aliachwa nje. "Kumtenga Mondlane ni kosa kubwa," mwanahabari Luís Nhachote aliiambia DW.
Hatua hiyo ilitangazwa kama sehemu ya mazungumzo ya kitaifa ya kutafuta suluhu ya mzozo wa baada ya uchaguzi unaoikumba nchi. Hata hivyo, mkutano huo kwa mara nyingine ulimtenga Venâncio Mondlane, mgombea wa pili maarufu zaidi katika uchaguzi wa Oktoba 9, 2024 na kusababisha ukosoaji na maswali kuhusu uhalali wa mchakato huu.
Katika mahojiano na DW Africa, mwandishi wa habari wa Msumbiji Luís Nhachote alikariri kukosoa kutokuwepo kwa Mondlane kwenye mazungumzo. Kwa Nhachote, kutengwa huku kunawakilisha hitilafu ya kimkakati: “Lazima wamjumuishe katika mjadala. Kumpuuza Venâncio Mondlane ni kitendo cha ujinga mkubwa,” alisema Nhachote, akisisitiza jukumu la mwanasiasa huyo kama mmoja wa washikadau wakuu wa mgogoro wa kisiasa nchini.
Nhachote pia alisisitiza kuwa Mondlane amekuwa ishara ya sauti za kijamii zisizojiweza. "Yeye ndiye kinara, mwanga unaowaongoza wananchi wa Msumbiji katika matatizo yao makubwa, kama vile afya na elimu. Kutokuwepo kwake kunadhoofisha jaribio lolote la kusuluhisha mzozo huo vilivyo,” mwanahabari huyo alisema.
DW Afrika: Je, ina mantiki kwa Venâncio Mondlane kuendelea kutengwa kwenye mazungumzo kuhusu mgogoro wa baada ya uchaguzi?
Luís Nhachote (LN): Ni muhimu kumjumuisha kwenye mjadala. Mtu makini yoyote hawezi kumpuuza mwanasiasa kaliba ya Venâncio Mondlane kama mpatanishi katika suala hili la mgogoro wa kijamii, na hasa zaidi sana katika mgogoro huu wa baada ya uchaguzi. Venâncio Mondlane aneendelea kuwa msemaji wa matatizo ya kijamii ambayo wananchi wa Msumbiji wanakabiliana nayo. Kwa hivyo, katika Venâncio wanaona mwanga wao wa tumaini, mwanga wao kiongozi wao mtetezi, yule anayeweza, kwenye meza ya mazungumzo, kuibua masuala ambayo ni muhimu kwa maisha ya raia wetu, kama vile afya, elimu, na kadhalika.
DW Afrika: Je, Venâncio Mondlane hangekuwa tayari kuwa katika hali mbaya, ikizingatiwa kwamba hakuwahi kujumuishwa kwenye mikutano na kwamba washiriki wengine wamekuwa wakijadili masuala haya kwa muda mrefu?
LN: Anapingana ili jambo hili lizingatiwe. Zoezi tu alilofanya leo [Alhamisi], akiondoka uwanja wa ndege, akijitangaza mwenyewe, ikifuatiwa na maandamano hadi soko lisilo rasmi ambalo linaleta pamoja kundi la raia wa Msumbiji, ambao ni kikundi kilichotengwa kiuchumi, na anaenda katikati ya jiji. Kwa hivyo, alitafuta tabaka za kijamii zenye hali mbaya zaidi ili kupaza sauti yake. Nadhani, kwa sababu tu ya maandamano haya kwamba ana msaada, msaada kwa tabaka la chini ambao ni wengi , hivyo hatuwezi kupuuza ukweli kwamba yeye ni muhimu la kuitwa kama meza ya mazungumzo. Labda waliweza kuwa wanapuuza ukweli wa kutokuwepo kwake kimwili nchini akiwa uhamishoni , lakini sasa yuko nchini.
DW Afrika: Kwa hivyo sura mpya katika mazungumzo iko kwenye upeo wa macho. Je, Venâncio Mondlane hangeweza kushawishi kwa kiasi kikubwa mijadala kwenye meza hii ya mazungumzo?
LN: Sidhani hivyo. Mpinzani wake katika uchaguzi kwa kweli yuko katika kundi moja la umri kwa rika, lililotenganishwa na miaka michache, na wanaweza kufanya mazungumzo zaidi au kidogo kwa nia moja. Tofauti sana na mhusika wa sasa, ambaye tayari anaondoka na hana chochote, wala kutoa au kuleta mezani kwa mazungumzo. Sielewi, kwa mfano, aliwezaje kuwakutanisha watu hao wanne wakati anamaliza muda wake wa kutumika katika serikali. Inaonekana kwangu kuwa kuna jambo hapa ambalo tunahitaji kufichua au kujua anakusudia kufanya nini.
DW Afrika: Nini maana ya kiapo cha Venâncio Mondlane Alhamisi hii? Je, alikuwa anajaribu kufikisha ujumbe gani kwa kitendo hiki?
LN: Uimara wake na imani yake, vinaonekana kuwa ni mfano. Alhamisi tuliona mfano wa kile kilichotokea Nairobi, sio kwa kiwango sawa, na Raila Odinga miaka michache iliyopita. Hali hii ilikuwa tayari imeandaliwa. Haina athari ya kisheria, lakini ina athari ya kisaikolojia, katika suala la kuhamasisha umma mkubwa wa raia wengi. Na ni mtaji huu wa kisiasa ambayo aliuoneshasha Alhamisi hii ambayo pia inamfanya achukuliwe kuwa mtu muhimu, mtu wa kupendeza. Alithibitisha kwa kitendo hiki kwamba hawezi kupuuzwa, na yeyote anayejaribu kufanya hivyo atakuwa anafanya kwa ujinga mkubwa.
Chanzo : Deutsche Welle