Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hali ilivyokuwa awali ~ Singida: Baadhi ya mitaa gari la taka halipiti kwa wakati, wiki ya 3 uchafu umezagaa mitaani
Awali, Mdau alidai Wananchi wanatoa taka nje siku ya kubeba wahusika hawaji kuchukua na kuwa hiyo ilikuwa ni wiki ya tatu hawajafika, taka zimezagaa kwenye mitaa tu.
Alisema hali hiyo inasababisha harufu kali mitaani, uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha usalama wa afya za Watu kwa kuwa inaweza kuchangia maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Leo Wananchi wengi wameonekana wakitoa taka na kuweka kwenye gari la kubeba taka ambalo lilikuwa halijapita takribani mwezi mmoja.