Hatimaye Hemed atangaza rasmi kuwa mtoto wa Mzee Majuto na kurithi pengo la marehemu Sharo Milionea

Hatimaye Hemed atangaza rasmi kuwa mtoto wa Mzee Majuto na kurithi pengo la marehemu Sharo Milionea

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Muimbaji na muigizaji na muigizaji wa filamu nchini, Hemedy PHD amesema anaamini amefanikiwa kuziba pengo la marehemu Sharo Milionea aliyeigiza kwenye filamu kadhaa kama mtoto wa muigizaji mkongwe, King Majuto.

Hadi sasa Hemedy ameshaigiza zaidi ya filamu tatu za komedi na Majuto na amesema wametokea kupatana mno kiasi cha kufanya filamu wanazoigiza pamoja zivutie kama zilivyokuwa filamu za Sharo Milionea na Majuto.

“Kwa upande mmoja nimekuwa kama mtoto wake mwingine ambaye nimetokea kumfariji kwasababu mzee napokuwa naye anakuwa na furaha sana na isitoshe tunashare vitu vingi sana,” Hemedy ameiambia Kikwetu Blog.

Hemedy amesema Majuto ameamuamini Hemedy kiasi cha kumwambia kuwa anaweza kuandaa filamu yake mwenyewe ambayo atashiriki kwa mikono yake miwili.

“Kwahiyo itakuwa ni kazi ambayo ipo kibaba na kimwana zaidi kuliko kibiashara zaidi which means ni mzee ambaye anakubali ninachofanya na anaappreaciate sana,” ameongeza.
 
Tatizo la Hemed kichwa maji sana hana akili ya kujichanganya kama Sharo, kujichanganya kwa Sharo kuliwafanya wapate kazi nyingi sana za matangazo zilizowaingizia pesa mingi. Hemed sizani kama ataweza kuziba pengo la marehemu Sharo hata kidogo labda abadilike sana huko ni kujifariji tu
 
Hawezi kuziba pengo la sharo, tatizo ana mashauzi sana, kwanza hizo movie alizoigiza nae sioni hata alichokifanya.
 
Hawezi kuziba pengo la sharo, tatizo ana mashauzi sana, kwanza hizo movie alizoigiza nae sioni hata alichokifanya.

hakuna kazi ngumu kama kumchekesha binaadamu mwenzako mwacheni mpoki aitwe mpoki tu.
 
Back
Top Bottom