Hatimaye HITS Tanzania wakubali kufulia...

Hatimaye HITS Tanzania wakubali kufulia...

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
313
Reaction score
7
Baada ya kushindwa ku-launch network kwa zaidi ya mwaka mmoja na waajiriwa wake wengi kutimka baada ya kuona hali ya kutoeleweka..leo hii mwenyekiti wa bodi ya Hits Tanzania Mh. Abdulah Mwinyi ametangaza kusitisha ajira za wafanyakazi hao kwa kutoa notisi ya siku 10 na malipo ya mwezi mmoja pamoja na kuahidi kulipa madai yote ya wafanyakazi hao ifikapo mwezi wa Disemba.

Kumekuwa na mkanganyiko kwa wafanyakazi maana pamoja na kusitishiwa ajira zao pia wameambiwa wanaweza kutuma maombi upya lakini kampuni itachukua si chini ya miezi 6 kusimama tena.....

Bado wafanyakazi hao wamechanganyikiwa maana it was a short notice na imepatika leo hii mchana....

POLENI NDUGU ZETU....KATIKA MAISHA YA BIASHARA KUFULIA IMO ....JIPANGENI UPYA
 
kwa mujibu wa kikao cha uongozi na wafanyakazi kilichofanyika siku ya jana ni kwamba wafanyakazi wapatao 96-100 wameshauriwa waandike barua/wajaze fomu za resignation ndani ya siku kumi kuanzia jana.

Ofisi zinazotarajiwa kufanya kazi ni mbili tu😱fisi ya C.E.O na ofisi ya HR.

dataz zinasema kwamba uongozi umetoa sababu moja kubwa kwamba kampuni inafanya reintrechment ili waone kama hela watakayosave kwa muda wa miezi mitatu inaweza kuwasaidia ku-take off by march.

dataz kutoka kwa mhanga wa hii kitu zinasema kwamba wafanyakazi hawa walioshauriwa ku-resign watalipwa mishahara yao ya miezi miwili tu,then biashara itakuwa imekwisha.

habari zaidi ni kwamba hela hiyo hawatalipwa kwa mara moja kama lump-sum.watalipwa kwa awamu.

habari mbaya zaidi kwa wenzetu hawa ni kwamba form zao za resignation HAZINA LEGAL AUTHORITY!na uongozi umesisitiza sana kwamba hakutakuwa na legal-authority kwenye hili swala.

naiomba jamii-media inc ifanye kinachowezekana tuone live fomu hizi za hits ambazo wenzetu wamezijaza.
 
Hii ni habari mbaya sana kwani wengi waliacha kazi zao na kujiunga kwa mema sasa mambo yanakuwa kama yakitapeli.

Hainingii akalini eti wanataka kusave pesa waone kama wanaweza kutakewoff, what kind of ubabaishaji is that, nafikiri nchi yetu inamianya mikubwa sana ambayo wawekezaji wanaitumia kufanya uhuni.
 
Something has to be done, hili swala lisigeuzwe si hasa, ni kama uhuni flani hivi, Je hawakufanya tathini kabla ya kuajiri watu wote hao?
 
Kama ni kweli basi ni balaa!! Hawa jamaa walichukua watu wazuri sana from the labour market!! Naamini hili pigo ni mtambuka!!

Ijapokuwa siamini investment kama hiyo ilikosa business plan ambayo inawaonyesha wazi kwamba pengine miaka mitatu mpaka mitano ya kwanza mapato yanakuwa chini sana kuliko gharama. Given the level of investment and the industry, you just can not expect to break even in five years.

Labda watuambie GFC ndo imewaathiri in terms of inflow of capital from the holding company!!! Lakini hata kama hivyo ndivyo, wasingeweza kusema eti waangalie kama wanaweza kupunguza costs kwa lay off, afu March 2010 wa take off!! That is ridiculous, tujiulize gharama ya kulipa staff wao kwa miezi 2 (kabla ya March, toa pia miezi 2 watakayolipwa) ni kiasi gani??

Staff 100 assuming kila mmoja analipwa sh. 5mil kwa miezi 2 ni 1 billion. Je Hits wanataka kutuambia sh. 1 bill (kumbuka industry waliyomo) inaweza kuwafanya wa take off??? Labda kama wanataka kufungua supermarket mikocheni!! Kinyume na hapo, kwa nini wasikope kwenye taasisi za fedha???

Hapa lazima kuna kitu lakini hawataki kutuambia ukweli watz! Poleni watz wenzangu, msijali tutagawana umaskini na kusonga mbele tukisubiri majanga mengine kama haya!!
 
imagine wasomi 100 wanakuwa out of employment COUNTING TEN DAYS from jana!
 
DAh kuna jamaa alikuwa Meneja ninakofanyia kazi, akaacha akapewa u sales manager kanda ya kaskazini, dogo akaona ameula sasa duh mambo yenyewe ndo haya balaa tupu jamani, hawa wawekezaji uchwara watatuua
 
Huyu mwenyekiti ni yule mtoto wa Mwinyi ambaye ni mbunge wa EAst Africa? Inawezekana hii kampuni mmoja wa wawekezaji wake ni Jeetu Patel kwani alikuwa mfadhili wake mkubwa wakati wa uchaguzi wao!! Hela ya EPA hiyo walitaka kulaunder through HITS!!
 
Duh!!! Poleni sana Wadau wote mlifikwa na janga hili... Mlango mmoja unapofungwa mingine mingi ufunguliwa... Mdau Tusker Bariiiidi!!!
 
Huyu mwenyekiti ni yule mtoto wa Mwinyi ambaye ni mbunge wa EAst Africa? Inawezekana hii kampuni mmoja wa wawekezaji wake ni Jeetu Patel kwani alikuwa mfadhili wake mkubwa wakati wa uchaguzi wao!! Hela ya EPA hiyo walitaka kulaunder through HITS!!
It may be true!
Unajua biashara ya mawasiliano sasa hivi kuingia sokoni inabidi ujikaze kweli kweli. Sasa tel waliingia muda, Lakini mapaka leo sijawahi kupokea simu ya mtu aliye kwenye matandao huo!! Tigo wanauwa.....
 
Hapa kuna dalili za dhuluma, najua ukijiuzulu unapoteza baadhi ya severance pay. Nawashauri waongea na lawyer kwanza, lakini bongo labda bora uchukue chochote uanze mbele unaweza ukapoteza muda tu.
 
Game ya mawasiliano kwa sasa ni ngumu sana na dalili kwamba HITS ingechomoka ni ndogo sana.Kampuni zote zinaangahika sasa kuwa na wateja wa kudumu.Tena huku tunakoelekea na usajiri wa namba watu wanaweaa ku-stick kwenye network moja kwa muda mrefu kuliko ilivyokuwa kwa hiyo inakuwa changamoto kwa makampuni mapya.

Wakati SASATEL wanaanza nikajua watakuja na mambo mapya sana lakini wapi bwana naona gharama zao ziko pale pale.Kwa sasa naona mtandao nafuu sana kuliko yote unabaki kuwa ZANTEL...mtandao huu bwana kwa kweli umekuwa safi sana kwa wengi yaani ukiwa unatumia huo mtandao basi local calls,international calls unafanya bila wasiwasi kwa kweli...gharama ni nafuu sana ukilinganisha na mitandao mingine.

Poleni ndugu zetu wa HITS ila najua hii inatokana na mianya ambayo wawekezaji wamekuwa nayo na ndio wanayotumia kutupotezea.Poleni tena na tena....siku hizi hata umekuwa na makaratasi mazuri na ujuzi wa kutosha kupata kazi bado ni changamoto kubwa...goodluck...!
 
Kama ni kweli basi ni balaa!! Hawa jamaa walichukua watu wazuri sana from the labour market!! Naamini hili pigo ni mtambuka!!

Ijapokuwa siamini investment kama hiyo ilikosa business plan ambayo inawaonyesha wazi kwamba pengine miaka mitatu mpaka mitano ya kwanza mapato yanakuwa chini sana kuliko gharama. Given the level of investment and the industry, you just can not expect to break even in five years.

Labda watuambie GFC ndo imewaathiri in terms of inflow of capital from the holding company!!! Lakini hata kama hivyo ndivyo, wasingeweza kusema eti waangalie kama wanaweza kupunguza costs kwa lay off, afu March 2010 wa take off!! That is ridiculous, tujiulize gharama ya kulipa staff wao kwa miezi 2 (kabla ya March, toa pia miezi 2 watakayolipwa) ni kiasi gani??

Staff 100 assuming kila mmoja analipwa sh. 5mil kwa miezi 2 ni 1 billion. Je Hits wanataka kutuambia sh. 1 bill (kumbuka industry waliyomo) inaweza kuwafanya wa take off??? Labda kama wanataka kufungua supermarket mikocheni!! Kinyume na hapo, kwa nini wasikope kwenye taasisi za fedha???

Hapa lazima kuna kitu lakini hawataki kutuambia ukweli watz! Poleni watz wenzangu, msijali tutagawana umaskini na kusonga mbele tukisubiri majanga mengine kama haya!!
mkuu huu ni utapeli tu how do you expand your business with only CEO & HR? hawa HR wanaachwa ili waweke sawa mambo then na wao wanakwenda mtaani.

Sijawahi kusikia eti kampuni inataka kutakeoff kwa kufukuza wafanyakazi labda wanataka ku settle-off...🙁
 
Ngoja tuwekane sawa hapa;

Is HITS = SASATEL? au ni vitu viwili tofauti?
 
Ngoja tuwekane sawa hapa;

Is HITS = SASATEL? au ni vitu viwili tofauti?
ngoma mbili tofauti hii ya SASATEL ni ya PROF MMOJA MTANZANIA YUKO SOUNT AFRICA ANAFUNDISHA TELECOM ENGEENERING NA MWANAHISA MWINGINE NI MAMA LWAKATARE NA WENGINE.

HIYO YA HITS ILIKUWA NA MTOTO WA MWINYI AMBAYE NI MBUNGE AFRICA MASHARIKI KAMA SIKOSEI...
 
wanajamii, kweli bwana Mwinyi, Abdullah sio mwema.... na hana mapenzi na watanzania wenzake kama ambavyo Mzee Ruksa alio nayo kwa Watanzania,
Hivi inawezekanaje mtanzania mwenzako umuachishe kazi na uumpe mshahara wa mwezi mmoja tu, na ana familia na watu wanaomtegemea..!!!!!!
Hii sio sahihi, mimi ninawashauri waende kwenye vyombo vya sheria ili waweze kudai haki yao..., ndugu zangu hao walioachishwa kazi ni ndugu zetu.....
 
Ndugu zangu mliokuwa wafanyakazi wa HITS nendeni katika vyombo vya sheria tena mtumieni Mwanasheria Tundu Lissu... anajua ku-fight...
Kingine kuna Chama cha kutetea wafanyakazi wa sekta za Mawasiliano TEWUTA mnaweza kupata msaada...
 
watu waliacaha kazi zao nzuri wakakimbilia huku...kumbe siyo kila king'aacho ni dhahabu
 
Heri ya HITS kuliko GTV. ila mwisho wa HITS ulionekana siku nyingi sana, baadhi ya waajiriwa walioona mbali walishaanza siku nyingi. Poleni ndugu, ila kama mlipata kazi HITS kwa njia ya halali, mwaweza kupata kazi sehemu nyingine pia!
 
Hatimaye uongozi wa Hits umekubali kusitisha kwa muda zoezi la kuwalazimisha wafanyakazi wake kusiani fomu za kuachishwa kazi, hii inatokana na wafanyakazi kufuata na kuhoji njia za kisheria za kudai mafao na hoja nyingine zinazohusu kuachishwa kazi katika muda wa siku 10 tu ikifuatana na malipo ya mshahara wa mwezi mmoja kama kifuta jasho.....
 
Back
Top Bottom