Hatimaye jana uso kwa uso huyu Kicheche na cha moto kakipata

bigmind

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
12,457
Reaction score
12,689
Muda sasa takribani mwaka na miezi nasumbuana na huyu kicheche. Kicheche huyu bwana ni kama alikuwa anatumwa, amekula viranga na kuku wangu sana, huwa anafumua nyavu za banda na kutinga ndani usiku, anasomba vifaranga kimyakimya nikiamka mama kuku hana viranga.

Mara chache sana huwa inatokea mama kuku akistuka nitaamshwa na mayowe makubwa natoka nduki bandani mara mlango ukilia tu, huyo anasepa.

Sasa jana shetani wake kazidiwa ujanja na Mungu wangu akamtuma mapema sana, kabla ya saa mbili maana amezoea huwa anazamia mida ya wachawi usiku wa manane, jana nikiwa nipo nje napunga upepo natega nikaone taarifa ya habari nikasikia kelele za mama kuku, nikatoka nduki hadi bandani abadani USO KWA USO na huyo mbaya wangu kicheche, nilichofanya nikazima taa na kuwasha hivyo hali ile ili mchanganya sana KICHECHE akapotea njia yake aliyochonga kwa pesa ya makinikia.

Mungu saidia nikakimbilia upande alipo chonga njia, ile anataka apande nilimpa buti la haja, akatoa mlio kama simba, kidogo nijikojolee kujikaza kiume nikamuita mshikaji wangu njoo huku vita ni vita mura takenya mura waituuh..(hapa najua ni akina mwita na bhoke wameelewa).

Kicheche kanichimba biti, na Mungu saidia nikapata kipande cha ubao nikaenda naye SAKO KWA BAKO anakala rugu ya kichwa mara chini ila sema ukweli hii vita ilikuwa kubwa mno..! Mungu saidia nikawa nimeshinda vita na kicheche mwenyewe huyu hapa chini[emoji116][emoji116][emoji116]

Wataalam mnaojua vicheche njooni mtwambie huyu kicheche wa namna gani, na anawezaje kuishi mjini kabisa dsm, katikati ya mji maana sikai maeneo ya mashambani.

Nasubiri vita iendelee maana naamini atakuwa na familia niombeni nishinde vita hii.

ASANTENI .
 
Hongera Mkuu. Pia, shukuru huyo kicheche hajakudhuru. Huwa ana tabia ya kurukia naniliu. Mkuu, kicheche huweza kuishi popote panapopatikana chakula chake. Kwakuwa alikuwa akichukua vifaranga, atakuwa na watoto mahali. Angekuwa mwenyewe tu, angebeba hata kuku wakubwa.
 
Huhuhuhuh..!

Sasa kama angetaka vita iwe ya dunia aguse ubalozi wangu aone..![emoji137][emoji137][emoji137]
 
Duuh! Unanitisha mkuu.
 
Nilipomaliza kusoma, nikajikuta nawaza sana....... Nilipo kumbuka wewe ni wa Daslam, nikajiona mjinga sana...[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Huhuhuhuh..!

Sasa kama angetaka vita iwe ya dunia aguse ubalozi wangu aone..![emoji137][emoji137][emoji137]
Huo sio ubalozi mkuu. Hiyo ndo ikulu yenyewe...! Yaani hapo haruhusiwi hata kugusa geti..! [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Huo sio ubalozi mkuu. Hiyo ndo ikulu yenyewe...! Yaani hapo haruhusiwi hata kugusa geti..! [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
Aisei acha kabisa, hapo ndiyo mimi maana ndipo paliponipatia jina hili ninaloitwa leo..!
 
Hujasikia mtaa wa pili Kuna mtu kafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…