Hatimaye Jubilee team Nairobi imekamilika, Sonko ameshinda

Wakenya nawaaminia,hamna mchezo ktk masuala ya maslahi ya Taifa ndio maana mmeendelea.

Vijana bado wapo mkuu,wanachapa kazi na maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tanzania hii isikieni tu,ni nchi ya hovyo sana.
Dada yangu nifah rudi madale ukapike maubuyu huku achana nako
 
safari hii nimepitwa sana na siasa za kenya.naomba utupe darsa dogo kuhusu uchaguzi huu unaondelea sasa.

Raundi hii hata sisi tunaojifanya magwiji wa siasa za kwetu imebidi kukaa maana Wakenya hawatabiriki tena, hizi line up za sasa hata makampuni ya kutabiri yameishia kubwagwa na kushangazwa. Watu wa karibu wa rais Uhuru na wale wa Raila wengi wamepigwa chini akiwemo hata ndugu wa damu wa Raila kule Bondo.

Hawa Wakenya wa leo hawatabiriki kabisa, line up iko tayari, kijijni kwetu mbunge na swahiba wangu amepigwa chini yaani nina jazba na wazee wa kwetu.

Nairobi tunaye Sonko atachuana na Kidero na pia kuna wale wa kujitegemea kama Miguna Miguna.
 
Acha kuongea ujinga kaka.sio vitu vya kuombea hivi.tofauti zetu za kwenye mitandao na wakenya,zisifanye tuwaombee mabaya.
Kila mtu ana mtazamo wake, mimi mtazamo wangu naiombea Kenya waingie kwenye machafuko, izo ni sara zangu kwa Wakenya
 
Dadeki...miguna kweli mbishi,kumbe mpaka Leo bado anafukuruta kwenye siasa za kenya.

kwa hiyo hawa akina sonko walioshinda chaguzi za ndani ndio wataenda kupambana ktk uchaguzi mkuu August?.
 
Mbona swali jepesi unajibu kwa jazba mkuu?

Hehehe!! Mkuu Azarel, huyo jamaa humjui, ndio zake na huibuka na mada za kujifanya kuijua Kenya kumbe ndio mweupe, sasa leo hii anauliza swali kama hilo. Hebu ichukulie jinsi mimi huja na mada za Bongo, halafu kesho niulize kama Dar ipo ndani ya mkoa wa Morogoro....nina uhakika hamtonijibu kwa kucheka.
..... Hilo swali angeuliza mtu mwengine asiyejifanya kuijua Kenya na kubishana na Wakenya kuhusu Kenya yao angejibiwa vizuri tu.
 

Unapoulizwa jibu swali acha longolongo
 
Dadeki...miguna kweli mbishi,kumbe mpaka Leo bado anafukuruta kwenye siasa za kenya.

kwa hiyo hawa akina sonko walioshinda chaguzi za ndani ndio wataenda kupambana ktk uchaguzi mkuu August?.

Miguna mwenyewe anajua dynamics na hatopata, ila hupenda kutajwa tajwa kwenye magazeti.
Ushindani wa Nairobi sasa hivi ni baina ya Sonko na Kidero, wataburuzana nyumba kwa nyumba, mlango kwa mlango aki ya nani patachimbika maana wote wajeuri kupita maelezo.

Japo nina uhakika Sonko atashinda maana maboys wote mitaani wanampenda balaa maana jamaa hujua jnsi ya kujimix, amewasaidia sana vijana na akina mama. Kidero atapata kura za elites ambao hawapendi sana kupiga foleni za kura na hushawishika na vijimaneno vya nadharia.
 
Sawa mkuu,
 
sonko sina shaka naye,lazima atatoboa.yule jamaa ni mtoto wa mjini (born town).

kidero kama ulivyosema,ataisha kupata kura chache za wadosi wa lunda na Karen.ila kura za githurai,roysambo,mathare,kibera na maeneo mengine zitaenda kwa born town sonko.
 
Sio mbongo ,ila ni mzee wa kukamata fursa kwa sana na madili kibao.

Anaamsha sana kwenye kampeni

Nina uhakika anaenda kushinda u-governor wa Nai

Naona mnatumia jina moja naye, ila jamaa ni fighter balaa, king'ang'anizi mwanzo mwisho na tunamtarajia kama rais wetu wa Nairobi.
 
Naona mnatumia jina moja naye, ila jamaa ni fighter balaa, king'ang'anizi mwanzo mwisho na tunamtarajia kama rais wetu wa Nairobi.
hata wewe mwenyewe sir name yako ni very common huku tz Miongoni mwa koo za mkoa wa Kilimanjaro.[emoji23] [emoji23]
 
hata wewe mwenyewe sir name yako ni very common huku tz Miongoni mwa koo za mkoa wa Kilimanjaro.[emoji23] [emoji23]

Nimewakuta kadhaa kwa jamii ya Wapare na Wachagga, kwanza kuna mmoja Mpare japo anaishi Tabora, juzi niliposikia akiitika baada ya kuitwa nikidhani ni mimi naitwa, nikashangaa na kumhoji, jamaa ni Mtanzania kabisa mwanzo mwisho ametokea Upareni.
 
Tuhuma zipi, mbona alianika vyeti vyake vyote tena kwenye mitandao. Cheti cha shule ya msingi, shule ya upili na hata chuo.
Huyu sio kama huyo Bashite wenu ambaye hadi leo ameuchuna, kazi kulia lia makanisani.

Hehehehe kaka pata Tuskee 3 baridi ntatuma kwa safaricom. Huku Bashite king'ang'anizi kama kupe na ni brainless
 
SONKO NI MTU WA WATU KULIKO KENETH - ILIKUA NI LAZIMA SHINDE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…