Hatimaye Kenya wamempata Magufuli wao

Hatimaye Kenya wamempata Magufuli wao

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Nakumbuka kipindi fulani Magufuli akiwa Rais basi tukasikia habari kuwa Wakenya wanamfagilia mbaya na wangetamani kuwa na Rais wa aina hiyo. DP wao ndio Magufuli, sio Ruto kama wengi walivyodhani

Sasa kuna huyu jamaa, Kaimu wa Rais, Rigathi Gachagua, ndio wakenya wana experience Magufuli wao

Jamaa anatiririka bila kuchuja maneno, yaani ustaarabu wa uongozi ni zero
Ukisikia akiongea ni burudani tu 😁😁

Picha lilianza siku ya kuapishwa anaanza kumnanga Uhuru palepale kuwa wameifilisi serikali

Siku nyingine namsikia akiwaambia wananchi wa kabila la Wakamba kuwa aligombana na Ruto kuteua waziri kutoka kwenye kabila lao maana walipigia kura upinzani

Juzi nimesikia tena akimuambia Ruto amuachie Raila ili aonyeshe namna ya kumnyoosha 🤣

Jamaa akiwa kanisani huko Mlima Kenya nafikiri, akaanza kuwananga waliompigia kampeni Raila, mara akamfokea mwanamuziki anaitwa Ben Gitae kwa kumuimbia nyimbo Raila

Kisha akasema kamsamehe na kuagiza palepale apewe kazi Ikulu, jamaa kama vile Ikulu ni kioski chake binafsi vile🤣

Halafu jamaa ana mind sana watu wa kabila lake kuwa upande wa Raila, anaona kama usaliti wa hali ya juu

Screenshot_20230123-231236.png


Screenshot_20230123-231443.png

Screenshot_20230124-082809.png
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]huyu mtata, picha lilianza siku wanaapishwa tu. Anataka maneno yake aseme

Sasa kama anataka maneno yake kuna haja gani ya kuhapishwa [emoji23][emoji23][emoji23] make nicheke
 
Sijakuelewa, kwamba hao wakenya unaowazungumzia walitamani Magufuli awe rais wao, kisa mapungufu yake? Sio mafanikio yake, wala mambo mengine ya maana ambayo aliweza kuyafanikisha? Jombaa, sisi wakenya sio wanafik wa sampuli hiyo.
Eti alikuwa msema kweli, asiyechuja maneno
 
Magufuli atabaki kuwa ni Magufuli, aliyofanya kwa ajili ya nchi, ni kumbukumbu tosha kwa vizazi na vizazi, ukibisha, kamwambie mbowe alopoke kwenye hadhara kumhusu JPM ama chama chochote kile waone watakavyoadhibiwa"
Si nasikia alisemwa Mwanza...wafuasi wake mlifanyaje?
 
Kijana wa Mau Mau huyo hana kupindisha maneno. Raila lazima anyooke hakuna serikali ya nusu mkate
 
Eti alikuwa msema kweli, asiyechuja maneno
Sasa hapo DP Rigathi amesema ukweli upi, au amefichua siri ipi hiyo? Mimi naona akitania upinzani na msanii wa nyimbo za injili Ben Githae. Sidhani kulikuwa na ulazima wa kutumia jina la Kenya, wakenya wala Naibu Rais Gachagua kumponda rais wenu. Ambaye tayari ni mwendazake, huo ni unafik maandazi.
 
Sasa hapo DP Rigathi amesema ukweli upi, au amefichua siri ipi hiyo? Mimi naona akitania upinzani na msanii wa nyimbo za injili Ben Githae. Sidhani kulikuwa na ulazima wa kutumia jina la Kenya, wakenya wala Naibu Rais Gachagua kumponda rais wenu. Ambaye tayari ni mwendazake, huo ni unafik maandazi.
Mimi sijamponda, hii ni compliment
 
Back
Top Bottom