Hatimaye kiungo Novatus Miroshi amefaulu kupata namba ya kudumu kwenye timu yake na leo kafunga tena

Hatimaye kiungo Novatus Miroshi amefaulu kupata namba ya kudumu kwenye timu yake na leo kafunga tena

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
679
Reaction score
870
Beki wa Tanzania anayecheza nchini uturuki akiwa na timu ya Goztepe SK, Novatus Dismas Miroshi amefaulu kujinasua kutoka kifungo cha kukalia benchi na kuanza kuaminiwa kuanza.

Leo amefunga goli la pili katika mchezo ambao wamepoteza 3-2 na Fenerbahce inayonolewa na Jose Morinho.

Hii kwake ni mechi ya 9 mfululizo akiwa mchezaji anayeanza kikosini cha kwanza...akiwa kafunga jumla ya magoli 3 toka ajiunge na timu hiyo mwaka jana

Beki kufunga sio lelemama jamani.

Ni jambo linalovutia sana kuona wachezaji wetu sasa wanaanza kuaminiwa kucheza first 11 huko nje na kuwapga benchi wazungu wakiwa kwao.

Nafurahi kusikia hata Kelvin John naye panga pangua humtoi nje kwny timu yake ya Aaliborg, ligi kuu Denmark

Mwingine sijui nani, yupo Newcastle Jets ya ligi kuu ya Australia.nasikia amesajiliwa jana

Wengine nipeni taarifa kama wapo...
 
Huko anacheza kiungo. Anakimbiza mwizi kimya kimya. Watanzania wakijua tu wataenda kumuharibia kwenye page ya timu yake.

Wabongo nuksi sana.
Hakika Bora hata hii taarifa isingekuja
Eeh Mola mlinde Miroshi wabongo wasi follow account ya hiyo team
Hasa vijana wa hovyo wa tabata ilala na kinondoni bila kuwasahau wa kariakoo
 
Ndio mkuu, ikitokea siku hajacheza wanajazana kwenye page kumtukana kocha wake.

Mbongo wa kuwa naye makini sana.
Ni mengi mno yatatokea matusi kejeli fujo dharau nikikumbuka Aston villa hadi Samatta akatoka kuomba waache ila wapi ikawa ndio kaweka mafuta kwenye moto hadi Leo hana ham na watz
 
Ngoja nitengeneze account fake ya miroshi mabongo niyapige hela
 
nimeangalia hii mechi mwanzo mwisho sema yule mmorocco (En Nesyri) Foward wa Fenerbahce anajua mpira aisee
 
Huko anacheza kiungo. Anakimbiza mwizi kimya kimya. Watanzania wakijua tu wataenda kumuharibia kwenye page ya timu yake.

Wabongo nuksi sana.
Kwenye page walishaanza jana,wabongo wanatia sana aibu
 
Uliangalizia channel ipi mkuu
Hizi mechi sometimes zinaonyeshwa kwenye kile kifurushi cha mwisho cha Azam cha 35,000 kama siko pale chini ya azam sport 4 HD zili channel mbili zinazofuata. Pale sometimes wanaonyeshe ligi ya scotland, Netherlands,Turkey,NBA ya marekani,na ligi ya Switzerland
 
Ni mengi mno yatatokea matusi kejeli fujo dharau nikikumbuka Aston villa hadi Samatta akatoka kuomba waache ila wapi ikawa ndio kaweka mafuta kwenye moto hadi Leo hana ham na watz
Mambo ya nje ya uwanja yanawapaje pressure kocha na timu kwa ujumla wake..
 
Back
Top Bottom