NDOA YA FARAJA KOTTA AIBU TUPU risasi mchanganyiko
Tukio hilo ambalo ni nadra sana kutokea katika sherehe za watu maarufu liliwashangaza waaalikwa na kuwafanya washindwe kuamini macho yao.
Vinywaji vilivyokuwepo katika sherehe hiyo ni maji, ‘wine', na soda pekee.
"Huwezi kuamini kilichotokea katika hafla hii ya mheshimiwa kwani vinywaji vilivyokuwa vikigawiwa, vilikwisha katikati ya sherehe hali iliyosababisha ndugu wa bwana harusi kumtonja MC Godwin Gondwe kukatisha baadhi ya vitu vilivyo kwenye ratiba ili mambo yasije yakaharibika zaidi," kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kwa kuhofia aibu zaidi ambayo ingeweza kuwapata waandaaji wa sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na vigogo mbalimbali wa serikali, Gondwe aliamua kukata mambo mengine yaliyoainishwa kwenye ratiba ambayo yangelazimu sherehe hiyo kuchukua muda mrefu huku hali vinywaji vikiwa vimeisha, jambo ambalo lingeleta fedheha.
Katika fufunika funika ya mambo ukumbini hapo Gondwe alijikuta akilazimika kurukia kipengele cha mwisho cha ratiba ambacho kilikuwa kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samuel Sitta kwenda mbele ya ukumbi kuongea machache kwa wanandoa hao.
Akiwa amelamba suti ya nguvu, Spika aliitakia maisha mazuri ndoa hiyo na kumuagiza mbunge Nyalandu kwenda naye bungeni mkewe ili kumtambulisha rasmi kama kanuni ya bunge inavyoagiza.
Kwa mujibu wa Spika Bunge, mbunge yeyote anapooa au kuolewa anatakiwa kumpeleka mkewe au mumewe kwenye vikao vya bunge viwili mfululizo ili kumtambulisha kwa wabunge.
Baada ya Spika wa bunge kumaliza kutanabaisha wasaa wake kwa wanandoa hao, alirudisha kipaza sauti kwa Gondwe ambaye naye bila kufanya ajizi alitangaza kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa sherehe hiyo, ndipo wageni waalikwa walipoanza kuinuka na kuondoka ukumbini hapo.
Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam
siku hiyo hiyo ya sherehe.
SOURCE;RISASI ...SHIGONGO