Hatimaye Marekani yashindwa kubaki Afghanistan

Hatimaye Marekani yashindwa kubaki Afghanistan

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Baada kuleta hasara kubwa ya maisha ya watu na kuharibu mali kwa miaka takriban 10,Hatimae Marekani imeamua kuondoka nchini Afghanistan ikiwa ni sharti muhimu katika makubaliano yake na wanamgambo wa Taliban.

Kiukweli Marekani kwa namna flani wamefanikiwa kusupress mashambulizi ya talebun hasa nyumbani lakini kwa Afghanistan wameshindwa hii moja, mbili taleban bado Wana nguvu kubwa katika baadhi ya majimbo nchini mwao ( us wameshindwa kuwaondoa)
Tatu, kwa fikra zangu za kawaida haitachukua mwezi wataleban watakua Kabul Kama watawala wapya endapo tu matakwa yao ya kimkataba na Kabul hyatazingatiwa ipasavyo ( wanawajua)
Nne Ni wazi wamarekani wameshindwa Tena Vita dhidi ya vijana wasioshindwa Vita dahari kwa dahari katika historia.
Tano nawapongeza wamarekani kwa kuondoka na kuacha wafu wazikane
 
yashindwa ama imeamua kusepa?

ni jambo zuri maana imekula pesa za walipakodi sana. na walipa kodi wamarekani kwa kweli ni wa kipekee maana inshu zingine wanapiga kelele ila wakipigwa tu 'tunapambana na magaidi' hua watulia. kuna wazee kwenye jeshi matajari leo kutokona na hivi vita!

wasiwasahau tu wale wakalimani waliokuwa wanawasaidia maana sasa watawindwa wakiamua kuwaacha!
 
Ni malengo gani ambayo yamefikiwa ndg? Mbona taleban bado wana nguvu kama awali?
taleban hawana nguvu sana kama zamani, ila bado wapo. Urusi ilikimbia Afghanstan baada ya muda mfupi sana lakini Marekani amehimri miaka 20; minataka aendelee miaka 20 tena? Hashindwi kufanya hivyo kwani Afghanistan ni training ground nzuri sana ya jeshi la ardhini (Army) ya Marekani
 
Nguvu gani??
Hii ndiyo nguvu ya Taliban.nchi ipo kama chujiyo kwa jinsi ilivyo
11april2021_Afghanistan_map_2-scaled.jpeg
 
Imeshindwa vipi kubaki Afghanistan? Kwani haujamsikia Blinken amesema wamefikia malengo waliyokuwa wameyaweka? Au unamaanisha nini kusema "washindwa kubaki"?
Washeshindwa vibaya sababu lengo lilikuwa kuwafuta wanamgambo wa Taliban kitu ambacho kimewashinda
 
Watalebani wanapewa siraha na Iran pamoja na Urusi marekana wamenyosha mikono wameamua kukimbia baada ya kuamriwa na watalebani kuwa waondoke ,walienda kuwasambaratisha wanamgambo wa Talebani lakini wameahindwa wanaamua kuondoka
Urusi inalipiza kisasi. Siku zile Marekani waliwapa Taliban silaha wawaondoe Urusi na kweli waliwaondoa na hatimae Urusi kusambaratika moja kwa moja mpaka alipokuja Putin. Sasa Urusi inafanya kama vile.Sijui hatima ya Marekani itakuwaje.
 
Baada kuleta hasara kubwa ya maisha ya watu na kuharibu mali kwa miaka takriban 10,Hatimae Marekani imeamua kuondoka nchini Afghanistan ikiwa ni sharti muhimu katika makubaliano yake na wanamgambo wa Taliban.

Marekani wana vituko, Mwanzo waliingia vitani kupambana na magaidi na washirika wake, sasa hivi wanaondoka baada ya kuwekewa sharti na magaidi hao hao, kuwa ukitaka amani hapa Afghanistan ondoka tuachie nchi yetu
 
taleban hawana nguvu sana kama zamani, ila bado wapo. Urusi ilikimbia Afghanstan baada ya muda mfupi sana lakini Marekani amehimri miaka 20; minataka aendelee miaka 20 tena? Hashindwi kufanya hivyo kwani Afghanistan ni training ground nzuri sana ya jeshi la ardhini (Army) ya Marekani
Sa si ndo kashindwa mzee au hio miaka 20 alikua anafanya nini ssa kama anaondoka hajatimiza lengo
 
Sa si ndo kashindwa mzee au hio miaka 20 alikua anafanya nini ssa kama anaondoka hajatimiza lengo
Umeongea vyema. Hawana nguvu Kama zamani lakini wataleban wanatawala kibabe eneo kubwa Sana la Afghanistan I na US wamefeli kuwaondoa..
Marekani wamefanikiwa tu kuwatoa mjini Kabul walipokua wametengeneza serikali yao mwaka 2002...
 
Yani kuna watu ni haiwaingii akilini kua US kafail..sijui kwa nini au hawahisi kama hata yeye anaweza fail
Umeongea vyema. Hawana nguvu Kama zamani lakini wataleban wanatawala kibabe eneo kubwa Sana la Afghanistan I na US wamefeli kuwaondoa..
Marekani wamefanikiwa tu kuwatoa mjini Kabul walipokua wametengeneza serikali yao mwaka 2002...
 
Urusi inalipiza kisasi. Siku zile Marekani waliwapa Taliban silaha wawaondoe Urusi na kweli waliwaondoa na hatimae Urusi kusambaratika moja kwa moja mpaka alipokuja Putin. Sasa Urusi inafanya kama vile.Sijui hatima ya Marekani itakuwaje.
Sidhani kama Ni kweli kwamba wataleban wanapewa silaha na Iran .. but Iran inawataja wataleban Kama Magaidi.. pia kuthibitisha hili Iran Wana kundi kinzani dhidi ya wataleban huko Afghanistan. Kikundi hicho Cha militia men Cha kishia huitwa "Fatmiyoun"
 
Yani kuna watu ni haiwaingii akilini kua US kafail..sijui kwa nini au hawahisi kama hata yeye anaweza fail
Itabidi wakubali then wakitoka hapo wakasome vyema kuhusu watu wa Afghanistan Ni watu wa namna gani?
 
Back
Top Bottom