Hatimaye Marekani yashindwa kubaki Afghanistan

Hatimaye Marekani yashindwa kubaki Afghanistan

Hujui kuwa lengo lao kwenda huko ilikuwa ni kuvunja network ya Al-Qaida, hawakwenda kutawala. Je leo hii umeshamsikia Bin laden au Ayman Al_Zawahir tena, au hata tamko tu lolote lile la Al-Qaeda?
Ahaa kwa hio taliban si ishu kwa au sio na haikua sababu ya wao kwenda
 
Urusi inalipiza kisasi. Siku zile Marekani waliwapa Taliban silaha wawaondoe Urusi na kweli waliwaondoa na hatimae Urusi kusambaratika moja kwa moja mpaka alipokuja Putin. Sasa Urusi inafanya kama vile.Sijui hatima ya Marekani itakuwaje.
Kwa hiyo Marekani inaenda kusambaratika kisa imeondoka Afghanistan?
 
Ahaa kwa hio taliban si ishu kwa au sio na haikua sababu ya wao kwenda
Hiyo haikuwa primary mission yao mzee. Walikwenda kwa vile Al-Qaeda walikuwa wanapanga mission za kuihujumu marekani wakiwa huko. Hata mashambulizi ya 9/11 waliyapanga wakiwa huo. Marekani iliiambia serikali ya Taliban iwatoe viongozi wa al-Qaida ili waje washitakiwe Marekani, lakini serikali ya Taliban ikasema haitaweza kuwatoa bila kupewa ushahidi wa kutosha kuwa kweli ni Al-Qaida ndiyo walioshambulia world trade center. Serikali ya marekani ikajibu kuwa msipowatoa, tutakuja kuwachukua kwa nguvu, na hiyo ndiyo ikawa mwazo wa vita ile. Wao kuendelea kuwapo kule kwa miaka 20 yote kulikuwa na sababu kadhaa; mojawapo ilikuwa ni kutaka kujenga influence kwenye eneo lile, pili terrain ya nchi ile ilionekana kuwa training ground nzuri kwa askari wa miguu wa Army- hivyo wakaendelea kuitumia. Sababu ya tatu hawakutaka kuiacha Afghanstani kama failed state kama ilivyokuwa Somalia; effect ya failed state ni kujenga terrorists wengi!
 
Hujui kuwa lengo lao kwenda huko ilikuwa ni kuvunja network ya Al-Qaida, hawakwenda kutawala. Je leo hii umeshamsikia Bin laden au Ayman Al_Zawahir tena, au hata tamko tu lolote lile la Al-Qaeda?
Hivi Kuna uhusiano wowote Kati ya alqaida na Taliban?
 
Watalebani wanapewa siraha na Iran pamoja na Urusi marekana wamenyosha mikono wameamua kukimbia baada ya kuamriwa na watalebani kuwa waondoke ,walienda kuwasambaratisha wanamgambo wa Talebani lakini wameahindwa wanaamua kuondoka
Acha mihemko ya kishabiki na habar za kwenye kawaha Una uhakika na unachosema?
Weka link tuone
 
Kwa hiyo Marekani inaenda kusambaratika kisa imeondoka Afghanistan?
Ni sawa hiyo.
Huko kusambaratika kumeanza kitambo na Trump ndiye aliyeletwa kupiga muhuri. Si unaona Marekani imekosa ubavu kumuondoa Bashar Al Assad pamoja na ahadi zao zote.Wamekuja maraisi wa Marekani na kuondoka Bashar yuko pale pale.Mfano mwengine ni Venezuela na Korea Kaskazini.
Hii ya Afghanistan inafanana na ile ya Vietnam.
 
Hujui kuwa lengo lao kwenda huko ilikuwa ni kuvunja network ya Al-Qaida, hawakwenda kutawala. Je leo hii umeshamsikia Bin laden au Ayman Al_Zawahir tena, au hata tamko tu lolote lile la Al-Qaeda?
Ule ulikuwa usanii tu wa Marekani kuitawala dunia na kuutokomeza uislamu. Kwa sababu hata hapo tulipokuwa tukiwasikia ilikuwa sio wao akina Bin Laden.Ilikuwa tunaangalia picha zao na kusikiliza propaganda za Pentagon.Wenyewe walikwisha kufa zamani. Na walipotaka kulizika jina la Osama Bin Laden ndio wakatengeneza mchezo mwengine wa Abortabad kwa kushirikiana na vibaraka wao wa Pakistan.
Dunia huwa inapata maendeleo ya kiteknolojia hatua kwa hatua.Nadhani kwa wakati huu propaganda kama ile haifanyi kazi tena.
 
yashindwa ama imeamua kusepa?

ni jambo zuri maana imekula pesa za walipakodi sana. na walipa kodi wamarekani kwa kweli ni wa kipekee maana inshu zingine wanapiga kelele ila wakipigwa tu 'tunapambana na magaidi' hua watulia. kuna wazee kwenye jeshi matajari leo kutokona na hivi vita!

wasiwasahau tu wale wakalimani waliokuwa wanawasaidia maana sasa watawindwa wakiamua kuwaacha!
Umeangalia na soko la silaha limeingiza kiasi gani kwa hapo pekee?
 
Conventional warfare ni vita ngumu sana ila wabishi wengi na naiona Afghanistan ikirudi kwa hawa wapashtun wa Taliban ndani ya miezi tu maana Majeshi ya Afghanistan yanayotumia Malori ya TATA hawataweza kufua dafu kama Mmarekani anaetumia magari ya kisasa ya Deraya MRAP ameshindwa katika muda wa miaka 20 kuliangamiza kundi hilo
 
Back
Top Bottom