mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Japo watu wengi walikuwa wanafahamu kuwa lengo la Urusi tangu mwanzo ilikuwa ni kuidhoofisha Urusi kiuchumi na kijeshi Walikuwa wanafanya kama siri fulani. Kwa sasa wanasema kwa wazi lengo hilo, kama mkuu wa majeshi ya marekani alivyokiri hilo lengo. Ila hawakuwa tayari kuingia wao binafsi katika vita na urusi ya ana kwa ana.
Lakini wakaichochea Ukraine ili ing'ang'anie kuomba kujiunga na NATO na wao Marekani wakasema watayakubali kwa haraka maombi ya Ukraine kujiunga na NATO. Marekani walikuwa wanajua kuwa suala la Ukraine kujiunga NATO ni mstari mwekundu kwa Urusi. Kwa hiyo walikuwa na uhakika kuwa LAZIMA URUSI ITAIVAMIA UKRAINE.
Walipoona Ukraine inakusanya majeshi wakajua kwa uhakika kuwa ukraine itavamiwa kwa hiyo WAKAFURAHI sana kuwa wamefanikiwa kuiingiza mkenge Ukraine ili ivamiwe na Urusi.
Kimsingi Marekani na washirika wake wa NATO ndio wako vitani na Urusi kwa kutumia DAMU ya Wa-ukraine kama askari wao wa kukodiwa katika vita hii. Inafahamika kuwa ukiwa na askari wa kukodiwa wewe ndio unawajibika kuwagharimia kila kitu wawapo vitani. Ndio maana nchi za magharibi HAZIONI TAABU kuwapatia ukraine silaha na pesa za kujikimu kipindi hiki cha vita.
Wasichotaka kusikia ni mapatano ya amani kabla lengo lao la kuidhoofisha Urusi kijeshi na kiuchumi halijafanikiwa. Wanatumia vikwazo vya kiuchumi zaidi ya 6,000 kuidhoofisha kiuchumi na wanataka vita idumu kwa muda mrefu ili kuidhoofisha urusi kijeshi na kiuchumi. Kinachowakera mabeberu wa magharibi ni kuona uchumi wa urusi haujateteleka kama walivyotarajia.
Nchi za magharibi wanaamini kuwa kwa kuwapatia silaha kali wa-ukraine kila wakati, zikiharibiwa wanapeleka zingine, zikiharibiwa wanapeleka zingine na mwisho wa siku wanaamini urusi ataishiwa silaha zake zinazoharibu misaada yao kisha watafanikiwa malengo yao. Ngoja tuone je watafanikiwa? Ila mpaka sasa inaonekana bado wanatwanga maji kwenye kinu.
Leo pesa ya urusi ruble imepanda thamani kufikia kiwango cha miaka miwili iliyopita! Na kwenye uwanja wa vita imeshambulia reli na vituo vya reli vingi vinavyotumika kuingizia silaha nzito na imeshambulia vituo vya kijeshi vinavyohifadhi silaha hizo. Hii ni nukuu ya mkuu wa majeshi ya marekani iliyonukuliwa na chombo cha habari cha marekani CNN:
"At the end of the day, what we want to see, what I think the policy of all of the governments together is a free and independent Ukraine, with the territory intact and their government standing," he said. "I think that's going to involve a weakened Russia."
He added that the unity among western countries is key.
"The unity of the West and the unity of NATO, and indeed, the unity of the globe has probably never been stronger than it is in the face of this unprovoked aggression. That's where we're heading."
Lakini wakaichochea Ukraine ili ing'ang'anie kuomba kujiunga na NATO na wao Marekani wakasema watayakubali kwa haraka maombi ya Ukraine kujiunga na NATO. Marekani walikuwa wanajua kuwa suala la Ukraine kujiunga NATO ni mstari mwekundu kwa Urusi. Kwa hiyo walikuwa na uhakika kuwa LAZIMA URUSI ITAIVAMIA UKRAINE.
Walipoona Ukraine inakusanya majeshi wakajua kwa uhakika kuwa ukraine itavamiwa kwa hiyo WAKAFURAHI sana kuwa wamefanikiwa kuiingiza mkenge Ukraine ili ivamiwe na Urusi.
Kimsingi Marekani na washirika wake wa NATO ndio wako vitani na Urusi kwa kutumia DAMU ya Wa-ukraine kama askari wao wa kukodiwa katika vita hii. Inafahamika kuwa ukiwa na askari wa kukodiwa wewe ndio unawajibika kuwagharimia kila kitu wawapo vitani. Ndio maana nchi za magharibi HAZIONI TAABU kuwapatia ukraine silaha na pesa za kujikimu kipindi hiki cha vita.
Wasichotaka kusikia ni mapatano ya amani kabla lengo lao la kuidhoofisha Urusi kijeshi na kiuchumi halijafanikiwa. Wanatumia vikwazo vya kiuchumi zaidi ya 6,000 kuidhoofisha kiuchumi na wanataka vita idumu kwa muda mrefu ili kuidhoofisha urusi kijeshi na kiuchumi. Kinachowakera mabeberu wa magharibi ni kuona uchumi wa urusi haujateteleka kama walivyotarajia.
Nchi za magharibi wanaamini kuwa kwa kuwapatia silaha kali wa-ukraine kila wakati, zikiharibiwa wanapeleka zingine, zikiharibiwa wanapeleka zingine na mwisho wa siku wanaamini urusi ataishiwa silaha zake zinazoharibu misaada yao kisha watafanikiwa malengo yao. Ngoja tuone je watafanikiwa? Ila mpaka sasa inaonekana bado wanatwanga maji kwenye kinu.
Leo pesa ya urusi ruble imepanda thamani kufikia kiwango cha miaka miwili iliyopita! Na kwenye uwanja wa vita imeshambulia reli na vituo vya reli vingi vinavyotumika kuingizia silaha nzito na imeshambulia vituo vya kijeshi vinavyohifadhi silaha hizo. Hii ni nukuu ya mkuu wa majeshi ya marekani iliyonukuliwa na chombo cha habari cha marekani CNN:
Top US general: We want to see a free Ukraine and a "weakened Russia"
US Chairman of the Joint Chiefs Gen. Mark Milley told CNN that the policy of governments supporting Ukraine is to see the embattled country free and independent and a "weakened Russia.""At the end of the day, what we want to see, what I think the policy of all of the governments together is a free and independent Ukraine, with the territory intact and their government standing," he said. "I think that's going to involve a weakened Russia."