FineForever
JF-Expert Member
- Apr 12, 2017
- 1,777
- 2,356
Mungu si Athuman!! Na uzuri wake, hachelewi wala hawahi. Yeye anapoamua kumwinua kiumbe chake "haters" ni nani hadi wakwamishe maamuzi yake?.Nataka huu mzuka waende nao kwenye World Cup wafanye final push tuone mwisho wao utakuwaje.
Tuombe uzima 2, wanaweza kufika fainali pia hasa ukizingatia kwamba wameshaukata mzizi wa mikosi na kwamba hawatakuwa na pressure kama waliyokuwa nayo kufuatia ukame wa kushindwa kutwaa Mataji licha ya kufika fainali kibao.
Hivyo, nawaona wakienda Qatar 2022 wakiwa na morali na confidence yakutosha!!! Ngoja tusubiri Mkuu.