Hatimaye Meya Jerry Silaa anunua gari la ndoto yake

Hatimaye Meya Jerry Silaa anunua gari la ndoto yake

IFRS

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2014
Posts
2,915
Reaction score
5,233
Meya Jerry Silaa akiwa anafungua gari lake aina ya Toyota IST alilofanikiwa kulinunua hivi karibuni tu ambalo limegharimu muda mrefu kulipata gari hilo ambapo anasema lilikuwa ni ndoto yake muda mrefu kwani amekuwa hana gari na amekuwa akitumia gari la serikali na kwa muda mwingine inamlazimu kutembea nalo katika shughuli zake binafsi.

Lakini sasa Meya Silaa Amesema amejiskia mwenye furaha sana baada kupata gari linalotumia mafuta kidogo na linalotumia gharama ndogo itakayomwezesha kuishi maisha ya Furaha.

Swali: Je, ni unamjua kiongozi mwingine wa kisiasa na kijamii kama meya Jerry Silaa mwenye gari la aina hii na zuri hivi
?

silaa.jpg

silaa2.jpg
 
kwani amekuwa hana gari na
amekuwa akitumia gari la serikali na
kwa muda mwingine inamlazimu
kutembea nalo katika shughuli zake
binafsi.


hapo kwenye red ndio sababu maccm yanatakiwa yaondoke madarakani mara moja.
alivyo kiazi anaongea tu as if kutumia gari la serikali kufanya shughuli binafsi sio kuvunja sheria!!!!!
 
dah.huruma sana sisi watanzania..hivi huyu jery slaa hanatuonaje watanzania kutudhihaki kiasi hiki?
 
Lakini ana mashamba makubwa Handeni na mifugo ya kutosha ukimwona kwenye daladala utafikiri hana kitu.Halafu usisahau kusema ni wa CDM haa ha ha ha haa.

Bora hata Jerry amejitahidi.
Mimi diwani wangu wa Kata ya Engutoto Ndg.Elibariki Malley hana hata baiskeli.
 
Nampongeza kwa hilo....anaonesha mfano. Kibongo bongo mtu ukiwa muadilifu maendeleo huja kidogo kidogo kama hivyo, nachelea kusema inawezekana Jerry ni muadilifu na anatumia anachopata kihalali tu.
 
Nilikuwa nataka kuuliza swali hili pia...

Mbona hii namba ya gari ni ya siku nying? CSX huenda ya mwezi wa saba mwaka jana sio mwaka huu. Tangu mwaka jana mwishoni namaba zilishaenda D...
 
Mbona watu wanamkandia badala ya kumpongeza?
Au angenunua Hammer ndio ingekua poa.
Jamaa kafanikiwa kununua gari aliyokuwa anaipenda, thats good.
Pia kanunua gari ambayo ni environmentally friendly, which is also good.
Congrats Jombaa kwa kufanikisha ndoto zako.
Sio kama michalii ya Chuga wakishika mill 100 wanakimbilia kununua ma VX mkweche bora tu waonekana nao wanasukuma Pakti.
 
Hilo gari amenunua kwa mtu(third hand)maana naona plate number inaanzia na C,au mleta mada umeamua kukurupuka tuu
 
Back
Top Bottom