Hatimaye Mo Dewji anamalizia mwaka kwa azimio la kutowavumilia wanaomtolea lugha za matusi kwenye mitandao ya kijamii kwa mwaka 2021

Hatimaye Mo Dewji anamalizia mwaka kwa azimio la kutowavumilia wanaomtolea lugha za matusi kwenye mitandao ya kijamii kwa mwaka 2021

Wewe ndiye uliyeanza kutoka nje ya mada na kujadili biashara za familia ya MO na kumkejele kua biashara ni ya familia na hata fedha anazotoa kwa Club kwasasa ukakejeli,au ulikua unaandika huku ukiwa usingizini?
Okey... hebu niambie.. kuna uongo gani? Mbona unakua na uchungu sana juu ya mwanaume mwenzako? Nimedhihaki wapi? Biashara ni za familia ama si za familia? Biashara zake hazina uhusiano na simba ama hazina?
Yuko ndani ya mkataba ama hayuko?
Acha kuwa na uchungu hivi juu ya mwanaume mwenzako.
 
MO yuko sahihi sana.

Unamtukanaje mtu halafu uhesabiwe haki ?
Wengi mnaobisha inamaana mnataka mruhusiwe kumtukana bila sababu ?

MO fanya kweli.
Ni sawa kabisa. Hata wewe hupaswi kutukanwa na yeyote hata ungekua muokota makopo.

Ila utani kama kawaida. Mtani huyo. Lazima tumtaniere. Na tunawaombea bundi atue hapo mkuu[emoji23][emoji23] bakuli litembezwe
 
Ameyataka mwenyewe, watz ni wazuri sana kwenye black mailing and bullying na hii yote ni wivu , chuki na roho mbaya

Sidhani watamuogopa, the best way is to keep personal life private..
Anapenda jina, matajiri wenzie kila business ina ID yake,
Yeye ndio simba, yeye ndio mo energy yeye ndio mo juice...

Atulie a deal na kizazi kisicho na ajira na mashabiki wasiojielewa

Bakhresa, Rostam huwez waona na hizo mambo
Hata hawa waliotangulia mbele za haki hawakuwa hivi
Mengi
Mufuruki
Subash Patel etx
Kumfananisha mo na uliowataja ni kukosa heshima kwa mo

Mo ni tajiri pekee aliyajiweka humble na watu wote kinahotokea ni side effekti tu hao wengine unaona wako safe kwaajiri wamejitenga sana

Kivyovyote ngumu kumfollow subash na wengine hata hawamjui hadi amefariki ila siku atapokufa mo ni phenomenal
 
Achana naye huyo. Steresi za maisha tu labda. Watu tupo hata tunataniana tu kama ilivyo kawaida yeye mishipa ya shingo imemtoka kisa Mo kataniwa. Angekuwa mwanamke ningesema labda anamtamani Mo...

Kuna watu wana uchungu nyie[emoji23][emoji23]
Nimesikitika zaidi kwakua ni mwanaume. Ila tumuache.

Hivi ile mil 300 mo aloomba michango imeshakamilika?
Honestly katika vitu ambavyo naona ni ngumu sana kuwekeza huu ukanda wetu ni soka. Yaan naona ni hasara tupu. Labda kama tungekua huko klabu bingwa huko tungekua tunafanya la maana. Wanaofaidika nadhan ni hawa middle men. Maana sasa hela zinaenda wapi miaka yote hiyo jaman. Bora hata nikalime tu
 
Ni sawa kabisa. Hata wewe hupaswi kutukanwa na yeyote hata ungekua muokota makopo.

Ila utani kama kawaida. Mtani huyo. Lazima tumtaniere. Na tunawaombea bundi atue hapo mkuu[emoji23][emoji23] bakuli litembezwe
Tunakataa matusi, Kejeri, maneno ya Kibaguzi na mambo kama hayo.
Kama utani ni sawa ila isivuke mipaka ya utani.
Kuna watu wanamtukana MO matusi ya nguoni kabisa bila sababu.

Hii haikubaliki katika jamii ya waliostaarabika
 
Sitavumilia- MO
-
Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ( @moodewji ) amesema mwaka 2021 hatowavumilia wale wote wanaotoa lugha za matusi na kumvunjia heshima.

Mo ametoa onyo hilo jana kupitia ujumbe wake mrefu wa kufunga mwaka 2020 aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Azimio langu kwa mwaka ujao humu mtandaoni ni kutovumilia wale wenye lugha za matusi na kunivunjia heshima mimi binafsi.

"Nitalazimika, japo kwa shingo upande na moyo mzito sana, kuwa-block, ku-report na ikibidi, kuchukua hatua za kisheria. Naamini kutumia lugha ya matusi na kudhalilisha dhidi ya mtu katika hadhara si ustaarabu wetu Watanzania, si maadili ya dini zetu na si uungwana pia.

"Sote tuna maisha nje ya mtandaoni. Wengi wetu ni wazazi, tunao pia wazazi, wategemezi na watu wengine muhimu kwetu ambao tunawaheshimu, wanatuheshimu na wana matarajio juu yetu," amesema Mo na kuongeza kuwa;

"Haipendezi kuwakwaza na kuwaumiza hao wanaotuthamini na kutuheshimu kwa figisu za maisha yetu ya mtandaoni.

"Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza mtandaoni katika mwaka huu unaoishia. Nami nimesamehe wale wote ambao walinikwanza kwa namna moja au nyingine," amesema Mo

Kuhusu Simba

Aidha, kuhusu Klabu ya Simba, Mo amesema; "Tunapomaliza mwaka, nawashukuru wote humu mtandaoni kwa kunikosoa, kunijenga na kunishauri mengi mimi binafsi na klabu yetu ya @SimbaSCTanzania.

"Mawazo yenu, michango yenu na matani yenu yamenifanya kufurahia uwepo wangu humu mtandaoni.

"Nawashukuru kwa daima kusimama nami katika nyakati zote na majira yote. Iwe heri, iwe shari, mmenionyesha upendo usio kifani.

"Naahidi kuendelea kuwa mtumiaji mwaminifu, mtiifu na mvumilivu wa mtandao huu mwakani," amesema MO.

Taarifa: mtanzanianews
Tatizo ni zile bilioni 20 anazodaiwa na Simba SC!
 
Okey... hebu niambie.. kuna uongo gani? Mbona unakua na uchungu sana juu ya mwanaume mwenzako? Nimedhihaki wapi? Biashara ni za familia ama si za familia? Biashara zake hazina uhusiano na simba ama hazina?
Yuko ndani ya mkataba ama hayuko?
Acha kuwa na uchungu hivi juu ya mwanaume mwenzako.
Huna akili wewe na wala hujui hata unajadili nini,unaruka ruka tu kama Kuku aliyekatwa kichwa kisha akaachiwa ghafla,una umasikini wa fikra.
 
...Je watu wanapoulizia kuhusu Bilioni za timu ambaxo hajazilipa...hili atakuwa analiweka katika kundi gani?
Kashfa?
Matusi?
In ajabu kwamba katika taatifa take yote Ndeefu hajaligusia hili LA no Mini atazitoa Bilioni Mbili anazodaiwa! [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Sitavumilia- MO
-
Mfanyabiashara na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ( @moodewji ) amesema mwaka 2021 hatowavumilia wale wote wanaotoa lugha za matusi na kumvunjia heshima.

Mo ametoa onyo hilo jana kupitia ujumbe wake mrefu wa kufunga mwaka 2020 aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

"Azimio langu kwa mwaka ujao humu mtandaoni ni kutovumilia wale wenye lugha za matusi na kunivunjia heshima mimi binafsi.

"Nitalazimika, japo kwa shingo upande na moyo mzito sana, kuwa-block, ku-report na ikibidi, kuchukua hatua za kisheria. Naamini kutumia lugha ya matusi na kudhalilisha dhidi ya mtu katika hadhara si ustaarabu wetu Watanzania, si maadili ya dini zetu na si uungwana pia.

"Sote tuna maisha nje ya mtandaoni. Wengi wetu ni wazazi, tunao pia wazazi, wategemezi na watu wengine muhimu kwetu ambao tunawaheshimu, wanatuheshimu na wana matarajio juu yetu," amesema Mo na kuongeza kuwa;

"Haipendezi kuwakwaza na kuwaumiza hao wanaotuthamini na kutuheshimu kwa figisu za maisha yetu ya mtandaoni.

"Nachukua fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza mtandaoni katika mwaka huu unaoishia. Nami nimesamehe wale wote ambao walinikwanza kwa namna moja au nyingine," amesema Mo

Kuhusu Simba

Aidha, kuhusu Klabu ya Simba, Mo amesema; "Tunapomaliza mwaka, nawashukuru wote humu mtandaoni kwa kunikosoa, kunijenga na kunishauri mengi mimi binafsi na klabu yetu ya @SimbaSCTanzania.

"Mawazo yenu, michango yenu na matani yenu yamenifanya kufurahia uwepo wangu humu mtandaoni.

"Nawashukuru kwa daima kusimama nami katika nyakati zote na majira yote. Iwe heri, iwe shari, mmenionyesha upendo usio kifani.

"Naahidi kuendelea kuwa mtumiaji mwaminifu, mtiifu na mvumilivu wa mtandao huu mwakani," amesema MO.

Taarifa: mtanzanianews
....Mikwara Mbuzi tu hiyo! Alipe Bilioni anazodaiwa ununuzi feki was timu yetu a one kama Luna MTU atakuwa na shughuli naye!

Hivi sisi Watanzania ama Waafrika tumerogwa?
MTU anatoka chumbani kwake na kutangaza kununua litimu letu likubwa, halipi hela anayotakiwa kulipa lakini anakabidhiwa litimu loote na kulifanya apendavyo!
Tuna akilii, matope?
 
Back
Top Bottom