Hatimaye moyo wa Nay wa Mitego wadondokea kwa mtoto mzuri wa Kiethiopia

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


Miezi michache tu baada ya staa wa Hip Hop Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kuripotiwa kutoka na msichana anayejulikana kama Chaga Baby, hivi sasa yupo na mrembo raia wa Ethiopia (Mhabeshi) anayejulikana kwa jina la Addi na ameapa kufunga naye ndoa.

Nay na mwanadada huyo ambaye ni msanii wa filamu, kwa sasa wanapoelekea ni pazuri tofauti na wapenzi wengine waliopita, kwani huyu humzungumzia kila wakati.

“Nimesharukaruka vya kutosha, sasa nimetulia na mchumba wangu huyu Addi tuliyekutana uwanja wa ndege huko Afrika Kusini wakati nikiwa narudi Bongo na yeye anarudi kwao, tangu hapo tulianza uhusiano na tunae-ndelea vizuri.

“Sija-wahi kusema kuhusu kuoa, lakini kwa huyu ndiye mke wangu ajaye maana tulipofikia ni pazuri, anawapenda sana watoto wangu, sitaki Wabongo wamzoee maana wataniharibia na maneno yao,” alisema Nay.

Staili ya kukutana kwa wapenzi hao, inafanana na ilivyokuwa kwa Diamond na Zari, ambao pia walikutana ndani ya ndege nchini humo, lakini wenyewe wakiwa na uelekeo mmoja wa Dar es Salaam.

Pamoja na hayo Nay amewachana katika video mastaa kadhaa wa kike wa Bongo Movie na Bongo Fleva kuwa wamezidisha kudandia vitoto wanavyovizidi umri.


Source: Bongo Movie
 
kuhusu wolper,wema na shilole ni kweli kabisa.tafadhari afute kauli ya "natania"
 
Dah! Nay kaniwahi kuopoa mtoto wa kihabeshi!!!
Watoto wazuri sana hawa ngozi matata kila kitu swadakta kabisa!!
Hongera NeyTrueBoy!
 
huyu jamaa ninachomkubali ni kuwa yupo real.
 
Ukiopoa mhabeshi lazima uape, amini nakwambia.
 
Huyu kapata mkimbizi anadhani... aende kwenyewe kuna wakali haswa... huyu anafanana na wa Eritrea wa kawaida sana mbona
 
Mwambie Ney Wa mitego watoto wakiethiopia balaa,kwa wale waliokwenda Ethiopia ukifika unaambia Hapa kuna utapeli Wa mapenzi kuwa makini,mwambieni akikubali kwenda kwao basi Nguo na pesa aweke akiba airport
 
mkuu cjui ni mimi tu ndo cjakuelewa!kwani we mwenzangu unaelewa ulichokiandika?
Talentboy gani huwezi kung'amua mambo!!!!! watoto wa kihabeshi ni wazuri mno ukiwapata lazima uape kuoa.
 
Talentboy gani huwezi kung'amua mambo!!!!! watoto wa kihabeshi ni wazuri mno ukiwapata lazima uape kuoa.
tatizo sio utalent wangu,tatizo ujenzi wako wa sentensi ndo unachanganya,hilo neno "uape" lilikosa kikamilishi chake "kuoa"...basi bora hata ungeandika "lazima ule yamini".ungeeleweka mapema sn ila nashukuru kwa ufafanuzi wko mkuu...swali kdg,mkuu kwn we ushawahi kuwabanjua hawa wahabeshi coz I have a dream too!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…