Kuna mambo humu yananichanganya aisee hizo pepa sita tunafanya once?? Cc MTAZAMO
hapo wameweka wepesi kidogo hii inapunguza mzigo wa kubeba masomo mengi kwa wakati mmoja
Wamekupa option ya kufanya pepa upendavyo hata moja moja....na sasa wanaruhusu kurekodi kila unalofaulu ila lazima umalize hiyo stage within 3 years otherwise unafutiwa masomo yote uliyofaulu na kuanza upya stage yote.After six years ukishindwa kumaliza hiyo stage unakuwa deregistered.......
mjue pia ukikamatwa moja unarudia na lingine ulilofaulu, mfano ukifanya mitano ukafaulu minne ukakamatwa moja utafanya ulilokamatwa na lingine moja
Khee kama nikifanya pepa mbili nikakamatwa moja so nitarudia zote 2 ?
EXACTLY, ukifanya sita ukakamatwa moja au mbili, utafanya ulizokamatwa na moja uliyofaulu utakayochagua. KOMAA MKUU.
Hadi sasa tumefika 5645 toka mwaka 1975 ukitoa waliokufa, kuhama nchi, kufungiwa au kuacha kazi ya uhasibu tunabaki kama elfu nne
Kafanye ACCA kama mfuko unaruhusu